Kauli ya Membe yaanza kumtesa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMAPILI, JULAI 22, 2012 09:32 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM


KAULI iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe kuwa kuna watu 11 wanayumbisha Serikali, ineonakana kuanza kumtesa.

Wiki iliyopita, Waziri Membe alitoa kauli hiyo, wakati akihojiwa katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisen cha ITV cha mjini Dar es Salaam.

Baada ya kauli hiyo, MTANZANIA Jumapili, iliamua kuwatafuta baadhi ya wabunge ili kupata maoni yao, ambao walisema Waziri Membe ama hajui anakichosema au anatafuta maarufu wa kisisasa tu.

Wabunge hao, wameonyesha waziwazi kutoridhishwa kauli ya kiongozi ambaye ameshika nafasi nyeti serikalini.

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), alisema kitendo cha Waziri Membe kudai kuna watu 11 wanaiyumbisha Serikali, hakitakiwi kufumbiwa macho kwa kuwa kinagusa mamilioni ya Watanzania.

"Huyu Membe aache maneno, wiki hii alisema kuna watu anawafahamu wanahusika na mauzo ya rada, sasa anakuja na suala jingine la watu 11 wanaoyumbisha nchi, tumweleweje huyo… hajui kama yeye ni kiongozi aliyeshika nafasi nyeti serikalini,

"Kama kweli anawaelewa… kwa nini asiwataje, wananchi wanataabika halafu yeye anakuja na siasa zake…simwelewi, labda ninyi nao mwambieni awataje," alisema Mpina.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (CHADEMA), alisema Membe anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuwa ana kitu anachokitafuta.

"Huyu tumemzoea, kama unakumbuka hivi karibuni aliibuka na kusema awatambua wahusika wa rushwa juu ya ununuzi rada, lakini cha ajabu hawajahi kuwataja… sasa unafikiri anataka nini,

"Kama kweli hao watu wapo mbona ameshindwa kuwataj, atuletee majina…nadhani huyo amekwisha tambua kuna wenzake wanataka kumwamisha asigombee urais 2015… anapaswa kujitafakari kwanza," alisema Wenje.

Naye Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan (CCM), alionyesha kutoridhishwa na kauli ya Waziri Membe na kusema hakumwelewa hata kidogo katika madai yake.

"Mimi nilimwangalia kwenye luninga akizingumza… nilipomsikia nilishindwa kumuelewa kwa sababu alichokuwa akisema hakiendani na madaraka yake.

"Sasa kama kweli anawajua watu hao, kwa nini asiwataje, atutajie ili hata wananchi waendelee kuimamini Serikali yao," alisema Azan.

Katika kipindi hicho, Waziri Membe aligusia mambo mengine, fedha za mkopo, Dola za Marekani milioni 20 zilizowahi kutolewa na Serikali ya Libya, enzi za utawala wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, hayati Kanali Muamar Gaddafi.

Alisema baada ya Serikali ya Libya kuikopesha Tanzania, nchi hizo zilikutana na kukubaliana fedha hizo zikopeshwe kwa kampuni yoyote itakayozihitaji.

"Baadaye Serikali ya Libya na Tanzania kukutana na kukubaliana fedha hizo zikopeshwe kwa kampuni yoyote itakayotaka kukopa izikope na makubaliano haya yako kwenye maandishi.

"Baadaye ikaja kampuni moja ya (Meize), kwa ajili ya kujenga kiwanda cha saruji kule Lindi na wakati wa kampeni tukawaahidi wananchi wa Lindi kwamba kiwanda hicho kitajengwa.

"Wakati tunaahidi hivyo, kumbe Kampuni ya Mohamed Enterprises, ilikuwa inashirikiana na ofisa mmoja wa ubalozi wa Libya ili apate fedha hizo na hapo ukawa ugomvi.

"Pamoja na hayo, mimi nilisimamia ili kuhakikisha kiwanda hicho cha saruji kinajengwa Lindi kama sehemu ya kumbukumbu yangu. Lakini baadaye wananunue wakabadilisha lugha, wakasema nimewapa marafiki zangu, jamani fedha hizi ni makubalino ya nchi mbili na mimi ni ‘share holder'.

"Sasa nakwambia fedha hizi ziko benki ya TIB, nendeni kwa meneja mkamuulize… huu ujinga gani huu unaozungumzwa, kwanza hata hizo Dola milioni 20 hazitoshi kujenga kiwanda bali zinatakiwa Dola milioni 60.

"Sasa nataka niwaambie wananchi wa Lindi, kwamba kiwanda cha simenti kitajengwa Lindi, hivi vituko vinavyotokea nitavigonga vyote … ipo siku nitawaanika wote, lazima watu hao wajue kwamba, ukikaa juu ya nyoka, ipo siku atakugonga tu.

"Hili nawaachia Watanzania waamue, lakini kuna watu 11 wakiwamo waandishi wawili wa habari, nitawatwanga kweupe, nyie suala la urais 2015 subirini tu, nitawaanika peupe bungeni tena kwa majina," alisema Waziri Membe.

Alipoulizwa kama atagombea urais mwaka 2015, alishindwa kuweka wazi msimamo wake kwa kile alichosema kuwa hajaoteshwa juu ya nafasi hiyo.

"Ole wao nioteshwe, ipo siku nitaoteshwa, najua nchi hii ina watu wanaoivuruga na hawataki kuona mafanikio, ukisema unataka kujivua gamba utaona wana uwezo wa kuchonga uongo, hao wanatumia vyombo vya habari kuchonga uongo.

"Kwa mfano, unawakaribisha vijana kama wa Chadema nyumbani kwako, unawapa chakula baadaye wanageuza mambo, we waache tu.

"Siku moja nitawatoa kwenye magazeti kila mmoja dozi yake, nitakuja kuwatandika kila mmoja na kinachoniudhi ni kwamba, hao watu wako ‘smart' wana fedha na wanataka kutawala hata kama hawana madaraka. Ukiona mtu anaanza kudharau wakati hana madaraka, ujue hapo kuna tatizo.

"Kuhusu uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema chama hicho kina nafasi ya kujiimarisha kupitia uchaguzi huo.

 
Jamani mimi sijaelewa hapa mwandishi wa taarifa hii anaelewaje kauli ya Membe imeanza kumtesa. Acheni ushabiki wa. Kijinga nani ambaye hajui kwamba gazeti hili la Mtanzania ni la Rostam Aziz na nani hajui ukaribu wa Rostamu Aziz na EL. Ni vema tukajadili hoja kuliko opinion zingine zenye ushabiki wa kisiasa. Ikumbukwe kuwa wakati Membe alipozikomalia pesa za Radar kurejeshwa Tanzania toka uingereza, gazeti hili la Mtanzania liliandika taarifa kwamba Membe anawaandama wapinzani wake bila kungalia hoja na maslahi ya nchi. Gazeti hili limegua Wabunge Watatu kuwakilisha
 
smart, wana fedha, na wanadharau walio kwenye madaraka na wanataka kutawala wakati wakiwa hawana madaraka....sounds like EL to me na vijana wake akina Balile
 
Mbona anafuka sana huyu kama mti mbichi kwenye moto. Ngumi hazijaanza analamimika ngumi chini ya mkanda. Zikianza si atajitoa.
 
Mi nadhani Hawa jamaa wa Mtanzania na mabosi wao wana haraka sana ya kuwafanya watu waamini kwamba na wao wamo kwenye kiwanda cha chuki dhidi ya wanasiasa kama Membe. Kwa maoni yangu wala hawana haja ya kujaribu kuwatumia Wanunge kama kinga. Membe ana historia ya kuwalipua watu hata kwenye Bunge. Nawashauri wasubiri walipuliwe alafu ndo tuanze kujadili hoja. Of all the newspapers, agazeti la Mtanzania linalomilikiwa Rostamu Aziz na Huseein Bashe liwe la kwanza kuomba oridha itajwe? Ama kweli watanzania wakati mwingine tuna chezewa michezo ya kitoto.
 
Jamani Wandugu, Ben K. Membe hata akipewa jahazi aliongoze, i.e nchi hii HAIWEZI, bora hata ya JK mara mia moja. Chukua mzani, Mweke DR Slaa Wilbroad Na Membe, ita watanzania waulize wanamtaka nani watakwambia.
 
Kupita kwa huu upepo...nachelea nisije haribu mpito huu wa kimbunga, ila nchi hii haiendi kwa akina Ben tena.
 
Katika hiyo orodha ya maadui wake kama bashe na rostam hawamo basi mhe membe atakuwa kashauriwa vibaya sana
 
Mi nadhani Hawa jamaa wa Mtanzania na mabosi wao wana haraka sana ya kuwafanya watu waamini kwamba na wao wamo kwenye kiwanda cha chuki dhidi ya wanasiasa kama Membe. Kwa maoni yangu wala hawana haja ya kujaribu kuwatumia Wanunge kama kinga. Membe ana historia ya kuwalipua watu hata kwenye Bunge. Nawashauri wasubiri walipuliwe alafu ndo tuanze kujadili hoja. Of all the newspapers, agazeti la Mtanzania linalomilikiwa Rostamu Aziz na Huseein Bashe liwe la kwanza kuomba oridha itajwe? Ama kweli watanzania wakati mwingine tuna chezewa michezo ya kitoto.


mlagha umenena.wenye chuki dhidi ya wanasiasa kwa kutumia magazeti yao wanadhan wanaweza kuwachezea watanzania wenye akili kama wanajaribu kuuchezea mtandao huu.
Ukweli unabaki pale pale kuwa kuna watu kwenye nchi hii wanaobuni na kutengeneza chuki na kuzipenyeza kwenye vyombo vya habari na wao wakijificha kwenye migongo ya vyombo hivi...kibaya zaidi kama ulivyosema mlagha wanadhani wanaweza kuwatumia wabunge makini kuvuruga ukweli huu,kwann wasisubiri? Hoja hapa ni kumsaidia Membe kueleza maadui wa kisiasa alionao nje ya hao 11.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom