Kauli ya Dk.Slaa kuhusu malalamiko ya Rais Kikwete ya kukithiri kwa rushwa ndani ya CCM

Mungu ni Mwema matendo yake ni makuu! Kwani hana upendeleo! Namini hata katika hili atasimama!
 
Inategemea na mungu mwenyewe alomwachia,kwasababu miungu wako wengi, labda mungu wa kikwere!
 
Lakini sina uhakika kama hawa jamaa wana Mungu.

Kapotolo...hawa jamaa ndio wanaongoza kwa kutoa sadaka na michango kanisani na misikitini, hata kama hawana mungu...pesa yao (ambayo ni yetu, ila wanatusaidia kuitumia) ndio inaeneza neno la mungu nchi hii!
 
Huyo Mungu wa CCM unayemnukuu mbona anaonekana kusuport vurugu, mauaji na dharau!
 
Labda mizimu na sio Mungu wa kweli. Watoa kafara wakubwa hawa na wachawi wakubwa. Wangekuwa na Mungu wangetuibia rasilimali zetu? Wanakera sana.
 
Katika hali inayoonyesha kushindwa kwa Mwenyekiti wa CCM Rais JK, ameamua kumuachia Mungu matatizo yanayoikabili CCM hasa swala la rushwa. Akifungua mkutano mkuu wa UVCCM jana rais kikwete aliwaonya vijana kukataa kutumiwa na kuepuka kuchaguana kwa misingi ya rushwa. Alisema kama na nyinyi mtashindwa 'Mungu ibariki CCM'. Kwamba kama na vijana nao watashindwa kudhibiti rushwa, sasa aachiwe Mungu. Maoni yangu: Nadhani kwa CCM ilipofika JK hawezi kuirudisha kwenye mstari na ni kweli anatakiwa badala ya kufanya ziara nyingi za nje ashinde msikitini amwombe Mungu akinusuru chama hicho kinachokata roho. Pole JK.
Mungu hufanya kazi pamoja na wanadamu,hivyo kama viongozi wa chama wana sehemu yao ya kufanya.Tatizo ni chama kutokuwa tayari kuwachukulia hatua wale wote wanaothibitika kuwa wala rushwa.
 
Hana lolote mana ukweli kua kiongozi alietokana na rushwa sio rahisi kuiondoa rushwa kwani nani asiejua kua Ridhwan kua anatoa rushwa nani asiejua kua uchaguzi wa ccm hauwezi kushinda bila ya rushwa? Ikiwa wewe raisi umesema huwezi tena unamuachia Mungu. Kiongozi Jasiri hatakiwi kusema hivo
 
Nilishaandika hapa kuhusu hatua za mtu anaekaribia kufa, ziko so open kwa mtu yeyote, stage ya mwisho ni kukubali (Acceptance)
 
Kikwete na kauli zake bwana!

Yeye kila siku ni wa kushangaa,wa kusikitika, wa kulalamika na kwa kufanya hivyo anazidi kuonesha kuwa ni kiongozi dhaifu kuliko wote mpaka sasa.

Maji hufuata mkondo. Sasa kama wazazi wa hao UVCCM ni wala rushwa na wamepata uongozi kwa rushwa (tena mara nyingine kwa kuwashirikisha hao hao vijana) alitegemea tunda gani ktk mbegu hiyo?

Mi namnshangaa sana Kikwete kwa kauli na vitendo vyake dhaifu. Nasikitika sana kwamba ndiye Rais wa nchi hii niipendayo.
 
Jana nilimuonea huruma sana kaka mkuu. Maji yamezidi unga. EL keshapanga safu katika jumuiya zote, wilaya zote, mikoa yote. Kilichobaki ataanza kuonekana kwa nguvu katika majukwaa akigawa pesa yetu aliyotudhulumu. Majuzi tu alikuwa msikitini Same akaacha 10 ml, Juzi akawa kwenye Vikoba, nafikiri ijumaa ataonekana kwa wana uamsho akiwa ndani ya kanzu na barakhashia.

Mungu ibariki CCM
 
Hakika Rais Kikwete ni wa ajabu sana! Yeye ndiye M/Kiti wa CCM-Taifa, ambacho ni chama tawala. Mhe. sasa analalamika.....sisi tulio nje tusemeje?

Hii ni wazi na kweli kuwa pengine Rais wetu siyo mtu madhubuti na makini.....
 
Mimi nadhani anachotakiwa kufanya ni kuwavua madaraka wale wote waliochaguliwa kwa kutoa rushwa.Waliotoa rushwa wote wanafahamika,Sofia Simba,Mary Nagu n.k,awalazimishe waachie ngazi na si kulalamika.
 
Mimi nadhani anachotakiwa kufanya ni kuwavua madaraka wale wote waliochaguliwa kwa kutoa rushwa.Waliotoa rushwa wote wanafahamika,Sofia Simba,Mary Nagu n.k,awalazimishe waachie ngazi na si kulalamika.

Maana yake CCM uongozi wote kabisa wa CCM uachie ngazi. Si rahisi kumtaja ambaye hajatoa rushwa au kusaidiwa na wenzake kutoa rushwa.
 
JK amekosa moral authority ya kukemea rushwa kwa vitendo kutokana na michakato iliyomweka madarakani. Hivyo basi tuendelee kutarajia mahubiri mengi sana kuhusiana na rushwa kutoka kwake lakini kamwe tusitarajie atachukua hatua yeyote.
 
JK amekosa moral authority ya kukemea rushwa kwa vitendo kutokana na michakato iliyomweka madarakani. Hivyo basi tuendelee kutarajia mahubiri mengi sana kuhusiana na rushwa kutoka kwake lakini kamwe tusitarajie atachukua hatua yeyote.

Kwa kuwa Dunia yote iko chini ya Utawala wa Mungu nadhani yuko sahihi kumwachia Mungu, Maana yeye ndiye mtawala atajua aruhusu nani atawale.
 
Nadhani wanaohusisha CDM na udini wakapimwe akili. Wadini wanajaribu kutafuta njia nyingine. Kwani CDM wanamiliki Redio Imani. Hawa nawaohubiri udini ukiangalia ni wale waliokimbia elimu kuogopa kula nguruwe, wamekuta wenzao wako mbali. Mfano na uthibitisho halisi ni huyu binti aliyetaka kuuawa na TALIBANI Pakistan kisa elimu binti Malala miaka 14, Bokoharamu? Wote wanapinga elimu.SLAA MUNGU wa wapagani, wahindu, mashinto, mabuda, wakristu, watani zenu wa macca awe nae. Mtu hatari hawezi kuwa mwenyekiti wa Bodi, CCBRT. Hatari wako huko
 
usinitukane
pia mimi mbona ni mkristo mwenzio
bwana yesu hajatufunza ivoo..

Kwanza unamaanisha Yesu Kristu? na inaonyesha huu mkristu, kwanza kwa namna jina ulivyoliandika kama u mkristu huna adabu kwa jina hilo tukufu. Pili Yesu Kristu na mwokozi alipinga unafiki, na alikuwa mkweli. Lakini uongo unaouandika hapa nimesikitika sana. Unajua aliwatimua waliokuwa wanafanya hekalu la Mungu walilolitumia vibaya? Na Tanzania ikiwa ni nchi tunataka walioigeuza nyumba ya mafisadi, wanafiki na waongo
 
nakumbuka enzi za mkapa na katibu mkuu wake mheshimiwa MANGULA,Walipobaini rushwa imetumika kwenye uchaguzi wa kura za maoni pale MOROGORO,matokeo yakafutwa na wote waliohusika wakazuiwa kushiriki kwenye kura za maoni za marudio.sasa siku hizi mmmm..... kila mtu analalamika.
 
Join Date : 21st October 2012
Posts : 112
Rep Power : 323
Likes Received 8
Likes Given
8

:blabla::blabla::blabla::blabla::blabla::blabla::blabla:...
This is a result of small thinking ability. Great mind talks about strategies, visions ans ideas, simple mind talks about people
 
Back
Top Bottom