Katuni ipi ni bora zaidi kwa Watoto wa Pre - School?

Ipo moja ilitengenezwa na wafaransa, baadhi ya wapenzi wa katuni hiyo waliandamana eti ilikuwa imekosewa,

Nadhani watakuwa wanaiedit ikitoka nita-KUPM mkuu
Kwahio aendelee kuvuta subira, kweli jf ina utajiri wa comedians!
 
Dah, sijui tutanusurika vipi... Bahati mbaya watu wameshaona ndio usasa, ndio ujanja!

uwezekano wa kunusurika upo. Tumia kila njia kudhibiti mambo usiyotaka watoto wako waone.

TV weka parental control kama unaacha watoto nyumbani au isiwepo kabisa mpaka wafike umri fulani wa kuanza kuelewa kitu wakielezewa.

Si lazima kwenda na wakati kwenye kila kitu hasa linapokuja swala la maadili. Badala ya kuhangaika na katuni ipi ni bora mnunulie mtoto vitabu vya picha, vya kuchora na vya kusoma; soma naye, chora naye, korokocha nae na kumsomea. Mwachie muda bwerere wa kucheza kulingana na umri, fahamu rafiki zake wa jirani na shuleni, kuwa makini na mambo anayoyaongea ili uweze kugundua kama amemeza sumu au la.

Usisahau kuongelea maswala ya "sexuality" kulingana na umri wa mtoto. Hii si kinga thabiti ya kunusurika ila si sawa na kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom