Katika vitu vilikuwa vinaogopwa enzi ya Nyerere.........!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Katika vitu Nyerere aliweka misingi ya maadili kwa raia wa nchii ilikuwa ni kuogopa vitu vya serikali!!Mfano ilikuwa ukikutwa na vitu hivi gereza utakalopelekwa utajuta mwenyewe kwa nini ulivigusa maana maadili yalikuwepo siyo sasa yamemomonyoka!!:-
  • Filimbi ya askari
  • Kikombe cha asikari TG
  • Chochote kilichokuwa na nembo ya (TG)
  • Sindano zakudungia ma Hospitalini
  • Dawa za Hospitalini
  • Pingu
  • Buti ya jeshi
  • Sare za asikari
  • Bendera ya Taifa
  • Kutosimama wakati bendera mbili zikishushwa ya CCM na Taifa
  • Kutoshiriki shughuli za ujamaa kama kuanzisha vijiji vipya!
  • Kupita kwenye Daraja linalolindwwa na asikari halafu wewe ukageuka nyuma utajuta!!!!
  • Kumiliki gobole kinyume cha sheria!!
  • Kubishana na serikali
  • Kuandamana bila ruhusa
  • UVCCM kuwavimbia wakubwa wao utajuta
  • Kujifanya mwana harakati!
  • Kujifanya wewe asikari kanzu
  • Kujitambulisha mimi Usalama wa taifa baa utajuta!
  • Kutishia watu unajua mimi nani??
Mengine endelezeni hapo!.................
 
>Kukopa vitu dukani.
>kuoa mke mwanajeshi.
>kutokuimba wkt wa mwenge za mbio.
>KUNYWA KAZI WAKATI WA POMBE.
>kuokolewa wkt unataka kujinyonga..utajuta.
>kwenda mererani na kujitambulisha kwamba ww ni askari.
>kuvaa kaunda suti wkt huna kazi yoyote.
>mtoto kuokota nyama wkt wa kula kabla ya wakubwa...yatakayomkuta mh.!
>kwenda hospitali na kumwambia muuguzi kuwa unaumwa na Edithi,(A.I.D.S)....atakimbia huyo....
 
Mkuu hiyo red nimeipenda sana!!
 
  • mwalimu kumfukuzia ada mwanafunzi
  • kuwa na pesa zisizo na maelezo
  • mama kufahamu mshahara wa mumeo
 
- Kumiliki 504 peugeot utajuta unashindana na rais
-Sinema iwashwe katikati ya wiki...utakoma
-Mfanyakazi wa Serikali kujenga...utachunguzwa pesa umetoa wapi
-Kula bar..bar zilikatazwa kupika watu wakale kwa wake zao
-Kwenda na msichana ambaye si Mkeo gesti...utaulizwa maswali mpaka ujikojolee
 
Kuandika habari zinazo kosoa serikali, ilikuwa unaweza ukanyongelewa mbali. Kipindi kama hicho ilikuwa vigumu sana kumkuta mtu kama Mwanakijiji na Saed Kubenea
 
Kutokuimba wimbo wa
Chama cha mapinduzi Tanzania ehhhh*2 na
Chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi*2
na ukimaliza kuhutubia katika mkutano wa chama usiposema
Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa Chama
 
1.Kunywa bia zaidi ya mbili baa lazima ufuatwe na watu wa usalama kujua umepata wapi hiyo pesa ya kunununa hizo bia
2.Kununua gari..Lazima kuwe na maelezo ya kutosha kama wewe unaweza kununa gari na pesa umepata kwa njia zipi.
3.Kila mtu kuheshimu dini ya mwenzake..
4.Mfanyakazi wa serikali ni lazima apande train(dar-mwanza,dar-kigoma,Dar-tanga,Dar-ARUSHA) kama anakwenda likizo labda kama kuna matatizo la ziada..

Nitakurudi ngoja nikasome vizuri kwenye kitabu changu cha kumbukumbu.
 
  • Kutojipanga foleni kwenye duka la kijiji, siku ambayo sukari inapatikana dukani hapo .... Utakoma kuwajua Mgambo!
  • Kukwepa kukimbia mchakamchaka... Lazima uonje joto la Kiranja.
  • Kuogea Lux, Roxanna.. Kutumia Colgate, kutafuna Big G (Bazoka), kuvaa raba za Bata.... Lazima jamaa wa mikingamo wakutafute
  • Kutumia Kimbo na mazagazaga mengine yoyote toka nje ya Tz!
 
Kutowanunulia watoto nguo za sikukuu-desember itakukost ndg...enzi hizo.. Thawaa!?
 
1.Kunywa bia zaidi ya mbili baa lazima ufuatwe na watu wa usalama kujua umepata wapi hiyo pesa ya kunununa hizo bia
2.Kununua gari..Lazima kuwe na maelezo ya kutosha kama wewe unaweza kununa gari na pesa umepata kwa njia zipi.
3.Kila mtu kuheshimu dini ya mwenzake..
4.Mfanyakazi wa serikali ni lazima apande train(dar-mwanza,dar-kigoma,Dar-tanga,Dar-ARUSHA) kama anakwenda likizo labda kama kuna matatizo la ziada..

Nitakurudi ngoja nikasome vizuri kwenye kitabu changu cha kumbukumbu.

Namba tatu nimeipenda
 
Sasa bora ipi? Ufisadi wa sasa au kutokuwa na ufisadi alafu mambo yawe kama hivyo
 
Back
Top Bottom