Katika upofu wangu

Sitachoka

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
3,030
1,303
Kwanza ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mungu wangu ambaye naamini amekuwa ndio mlinzi na kiongozi wa kila nyayo ninayotaraji kuikanyaga na kunifanya niweze kuifurahia dunia kwa miaka ishirini na sita niliyopata kuishi.

Nikianza kwa kuonyesha dhamira yangu juu ya tafsiri ya neno upofu kwa kawaida neno hili hutumika kuwakilisha mtu asiye na nuru ya kuona, hivyo uhafifu wa kuweza kuona mambo ambayo akili huhitaji kuchanganua vilevile neno hili hutumika .

Siku ya leo najaribu kuangazia mambo makuu manne ambayo ni serikali, dini, taifa la marekani na demokrasia.

Mwanaharakati na mchekeshaji maarufu wa nchini marekani anayefahamika kwa jina la Dick Gregory amewahi kusema, "Sijui kwa nini
marekani inafikiria kuitawala dunia kulazimisha watu wafuate njia zake kwa bunduki, kama una kitu kizuri huna haja ya kulazimisha watu".

Nikigeuza macho kwa dini, serikali, marekani na demokrasia ni vitu ambavyo vingi vimekuja kwa njia ambayo ni ya kulazimishwa na katika upofu wetu tumeyakuta na kuona ni kawaida.

Wengi tunateseka lakini hatujui hivyo tunaejenga donda litakalo umiza vizazi vijavyo.

Harakati za marekani katika kupambana na ugaidi ambayo ni njia moja wapo ya kukuza sera yake ya demokrasia idadi kubwa sana ya watu wamepoteza maisha yao ukianzia afghanstan, Pakistan, Iraq na maeneo mengine ikiwamo Somalia.

Wanaharakati wengi walitakiwa kuuwawa kwa kuwa walikuwa na mtazamo tofauti mfano Patrice Lumumba.

George bush alitoa angalizo kwa dunia kwamba sasa dunia ina vita dhidi ya ugaidi pasipo makubaliano na mataifa yote na kuonya kuwa "be with America or with terrorist", kwa haraka hakuna taifa litaloafiki kuwa chini ya ugaidi.

Mitazamo hii inatufanya tuangalie hata katika dini tunazosali ambazo kauli mbiu kubwa ni fanya tusemavyo au utaenda motoni, je ni nani anayependa kuungua milee?

Nako serikali inasema fanya tutakavyo au utaenda jela, nani aliyeradhi kwenda jela?

Tunazidi kujionea kundi la watu likitajirika bila kutazama maskini wengi walioko chini kupitia dini, kupitia serikali na sasa wamekuwa na uwezo hata wa kununua si haki tu bali hata uhai wa mtu bila kuhofu upande wowote, hii inatoa picha ya baadae itakavyokuwa kama leo uhai wa watu uaweza kununuliwa na mtu bila hofu na mmea huu ndo unaanza kuota vipi kwa kizazi kijacho ambapo mmea huu utakuwa umekomaa?

Tulia, ondoa malisho ya makuzi yako fikiria kwa kina na fanya maamuzi hata kwa fikra si lazima vitendo maana itakuwa ni chachu ya
mabadiliko kwa vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom