KATIBU WA CCM AUAWA KWA KUCHOMWA NA KISU OFiSINI

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Na Mwandishi wetu, Mwanza

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Isamilo wilayani
Nyamagana mkoani Mwanza, Bahati Stepahano (50) amefariki dunia baada
ya kuvamiwa ofisini kwake na kuchomwa kisu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa polisi mkoani
Mwanza, Simon Sirro alisema katibu huyo alivamiwa ofisini kwake katika
Mtaa wa Nera jijini Mwanza na mtu ambaye hivi sasa anashikiliwa na
polisi. Kata ya Isamilo ni kata anayotoka Meya wa Jiji la Mwanza
Leonard Bihondo.

Ilielezwa kuwa mvamizi huyo, alifika katika ofisi za CCM akitaka
kuonana na katibu huyo kwa madai ya kuwa na shida za kiofisi na baada
ya kuruhusiwa kuonana naye alisikika wakibishana naye na baadaye
alionekana akitoa kisu na kumchoma. Kamanda Sirro alisema tukio hilo,
lilitokea saa 6:30 mchana.

“Kwa mujibu wa mashuhuda baada ya kuona mabishano hayo waliamua
kufuatilia na kumuona kijana huyo akitoa kisu na kumchoma katibu huyo,
upande wa titi la kushoto na tumboni, baada ya kufanya hivyo inadaiwa
alitoka mbio kutaka kutokomea, lakini wasamalia wema wakiwemo
wafanyakazi wenzake na marehemu wamkimbiza na kumkamata akitaka
kujitosa ziwani” alisema Kamanda Sirro.

Alisema polisi wameanza uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kukusanya
taarifa za awali kwa watu walioshuhudia tukio hilo.

Alisema kwa kuwa wamemkamata mtuhumiwa watatumia mbinu za kijeshi
na kikachero kutambua chanzo cha mauaji hayo.

Kufuaia kifo hicho, habari zimesikika kwamba mauaji hayo yanatokana na
masuala ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao kwa vile alikuwa
haelewani na mwanasiasa mmoja ambaye mara kadhaa alikuwa akitaka
katibu huyo ahamishwe katika kata yake kutokana na kutokubaliana na
masuala yake ya kuhujumu wagombea wanaokuja kupingana naye.

“Hii ni ishara kuwa siasa za sasa zimeanza kuchafuka, kwa vyoyote vile
kifo hiki kinahusu masuala ya siasa, Mwanza tunaijua imekuwa na
matukio ya mauaji hasa kwa watu wanapoguswa sana katika maslai yao .
Siku chache kabla ya katibu huyo kuuawa kiongozi mwingine wa siasa
katika kata hii amewahi kutishiwa kuuawa na kesi yake kumalizwa
kinyemela na ofisa wa polisi,” alisema mmoja wa wanachama wa CCM.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mwangi Kundya Rajabu amepokea kwa
masikitiko kifo hicho na kusema kwa sasa chama kinasubili uchunguzi wa
jeshi la polisi ili kubaini sababu za mauaji ya mtumishi wake.

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akizungumza na gazeti hili,
alisema amestushwa na kwamba katibu alifarikia dunia wakati
akipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
 
Malipo ya dhuluma ni mauti... na ole wao wanaodhania kuwa kumuua mtu mmoja kutawawezesha kupenyeza mambo yao maovu... Haki huvunja milima
 
Back
Top Bottom