Katibu mwenezi wa CHADEMA kata ya Themi hatufai

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
11,741
14,639
Katika kipindi hiki ambacho tunapambana na changamoto kubwa kisiasa,tunahitaji kuwa na watu makini wenye ushawishi na uwezo wa kujenga hoja, na zaidi ni kuwa na uwezo wa kutumia kila fursa inayojitokeza ili kujenga chama bora, chenye ushindani na utayari wa kuongoza dola.

Nimesikitishwa sana na katibu mwenezi wetu wa kata ya Themi kujipa likizo binafsi, nimejitahidi kuwahamasisha wafanyakazi wenzangu ili kutuunga mkono kwenye harakati za kuleta mabadiliko, hatimaye bila shaka yoyote wamekubali kuungana nasi, ila nilipowapeleka kwa katibu wetu huyu ili akamilishe utaratibu wa kuwaelimisha zaidi,na kuwakabidhi kadi,yeye alidai kuwa huu ni wakati wake wa kupumzika kwani kazi za uenezi hufanyika kipindi cha uchaguzi na si sasa!

Kwa kweli kauli hii imenivunja nguvu na kufikiri upya uwepo wetu ndani ya jamii, hapana! Ni wakati sasa wa kutafuta watu sahihi kwa kazi sahihi! Kumbuka kuwa kata yetu haina mbunge, diwani wala mwenyekiti, nafikiri huu ndio wakati sahihi wa kusambaza elimu ya uraia kwa wengi walioikosa, kujenga misingi imara ya chama kwenye ngazi hizi za chini nk, ila kwa mwendo huu wa katibu wetu huyu mwendo utakuwa mrefu.

Naomba sana tumtazame ndugu yetu huyu ili tujiridhishe kama kweli anafaa kuwepo kwenye nafasi hiyo, niliwahi kumuuliza kuhusu utata wa uanachama wa mwenyekiti aliyevua gamba na kuvaa gwanda ndugu Subira mwanga, alinijibu kuwa kweli haelewi kama subira ni mwanachama halali wa CDM ila atajua mwenyewe (Subira) kama yupo kwetu au CCM, hii siyo kauli njema kutoka kwa mwenezi wetu, hakika anastahili kutazamwa.
 
Mimi nadhani huyu katibu anatatizo la kutoa majibu sahihi. Sio tatizo/kosa kwenda likizo, lakini ofisi huwa haiendi likizo! Anawekwa mtu anakaimu hadi atakaporudi. Majibu yake ni upuuzi na hakuna dawa zaidi ya kumpiga chini kwenye uchaguzi ujao. Tahadhari yangu ni kwamba usikute mna personal conflict maana hamkawii kutuvurugia chama!
 
Mimi nadhani huyu katibu anatatizo la kutoa majibu sahihi. Sio tatizo/kosa kwenda likizo, lakini ofisi huwa haiendi likizo! Anawekwa mtu anakaimu hadi atakaporudi. Majibu yake ni upuuzi na hakuna dawa zaidi ya kumpiga chini kwenye uchaguzi ujao. Tahadhari yangu ni kwamba usikute mna personal conflict maana hamkawii kutuvurugia chama!

Ndugu nafikiri taratibu za chama zipo ungezitumia hizo ukaona hazikusaidii sasa ndo ule humu jf
 
Ndugu nafikiri taratibu za chama zipo ungezitumia hizo ukaona hazikusaidii sasa ndo ule humu jf

Kutumia taratibu za chama ni hatua ya juu zaidi ya kuomba mwongozo kwa watu kama nyie,NB ofisi ipi?themi hakuna diwani wala mwenyekiti wa chama chochote,zaidi ya katibu wetu huyu.
 
report kwa mh mbowe na dokt slaa etc no ya mbowe 0784779944 asilete ujinga watu wanapoteza mda kujenga chama yeye analeta uhun:drama:
 
CHADEMA ngazi ya wilaya, Mkoa, au hata Taifa wanayo jukumu la kutoa mafunzo kwa viongozi wa chama, inawezekana huyo anajua ama kwa utashi wake aliamua kukujibu hilo si tatizo, maadam CHADEMA wanafanya kazi kama timu moja kuanzia ngazi ya msingi mpaka taifa.
Ungemuuliza huyo katibu kama anayo katiba ya chama, inawezekana siyo kosa lake, bali hajawahi kuisoma katiba ya chadema na kujua jukumu lake kama katibu mwenezi wa chama!
 
Nafikiri hapa siyo mahali pake tumia mikutano na vikao halali vya vyama kuwasilisha kero zako.Usiwape faida wasema hovyo!
 
umekosa nidhamu ya hali ya juu kabsa chadema kama chama kina muundo wa utawala kwanini usifuate taratibu hizo kiofisi badala ya kuja hapa ,pamoja na kwamba pengine kuna ukweli ndani yake ila tatizo ni wewe mwenyewe.kaa chini ujiangalia ulipotoka na unapoenda .
 
mimi nadhani huyu katibu anatatizo la kutoa majibu sahihi. sio tatizo/kosa kwenda likizo, lakini ofisi huwa haiendi likizo! Anawekwa mtu anakaimu hadi atakaporudi. Majibu yake ni upuuzi na hakuna dawa zaidi ya kumpiga chini kwenye uchaguzi ujao. Tahadhari yangu ni kwamba usikute mna personal conflict maana hamkawii kutuvurugia chama!

yeye hajaenda likizo ya kawaida, ameacha kufanya kazi za chama hadi ifike kwenye uchaguzi ndo ataonekana tena kurudi kufanya kazi za chama. Ndo mleta hoja anasema kajipa likizo.

Any way, themi iko wapi?
 
umekosa nidhamu ya hali ya juu kabsa chadema kama chama kina muundo wa utawala kwanini usifuate taratibu hizo kiofisi badala ya kuja hapa ,pamoja na kwamba pengine kuna ukweli ndani yake ila tatizo ni wewe mwenyewe.kaa chini ujiangalia ulipotoka na unapoenda .

uwazi na ukweli, kwani kamuonea?
 
nafikiri hapa siyo mahali pake tumia mikutano na vikao halali vya vyama kuwasilisha kero zako.usiwape faida wasema hovyo!

ati wasema ovyo!!!!!!!!!!! Ndiyo gharama ya democrasia mkuu wangu. Alichosema kakerwa, kama tungefuata taratibu kwa kila jambo, ingekula kwetu na baadhi ya mambo tusingeyaokoa.
 
Back
Top Bottom