Katibu Mwenezi CCM atuhumiwa kumbaka binti yatima………..!!!!!!!!!!!!!!

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
Katibu Mwenezi CCM atuhumiwa kumbaka binti yatima………..!!!!!!!!!!!!!!

30 Dec 2011 asubuhi,Katibu mwenezi wa ccm kata ya Bilele anatuhumiwa kubaka mtoto yatima wa umri chini ya miaka 18 katika eneo la Hamugembe Bukoba,baada ya mtoto huyo kwenda kwake kumshitaki kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana aliyeaminika kutaka kumpiga, unyama gani huu jamani.Badala ya Katibu huyo kutoa msaada wa kumwepushia binti huyo kipigo toka kwa kijana huyo yeye akamzawadia kumbaka na kumsababishia maumivu makali yatima huyo masikini ya Mungu. Cha kusikitisha zaidi mpaka leo hii hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa kwa Katibu huyo mbakaji,Polisi wamejitetea kuwa hawakumtia mbaloni mapema kwa sababu taarifa za tukio hilo zilichelewa kuwafikia,mimi na wewe hatujui kama ni kweli hawakupata Taarifa. Sasa Taarifa wanazo tungoje na tuone je hatua zitachukuliwa au ndiyo siasa zitachukua nafasi huku yatima huyu akiumia?

Wale walio karibu na eneo hilo nawaombeni mjaribu kuhakikisha tatizo la yatima huyo linashugulikiwa na vyombo vya sheria na mtuhumiwa anaadhibiwa kwa unyama alioutenda.:juggle::A S 465:
 
Hiyo kawaida yao angekuwa wa cdm ungewaona tu humu wachangiaji wangetiririka na makashfa na mbwembwe kibaoo.

Yaani hawa ccm rushwa imewakaa sana unaweza ukaona mtoto huyo baada ya kushtaki malalamiko yake jidume hilo likaomba rushwa bint alivyo sema hana likaamua kumduu kisha ndipo ayashughulikie malalamiko yake.

Hiki chama kina laana zaid ya shetan
 
Baada ya viungo vya albino kuwa ngumu kuvipata wamepewa maasharti mapya ya kubaka kutoka kwa wataalam wao (vigagula)
 
Kama akikutwa na hatia, sheria itachukua mkondo wake. Hamna mtu aliye juu ya sheria.
 
miaka 18 anabakwa nini sasa...kajichanua mwenyewe bana

acha kukurupuka wewe kama mtu awashwaye na masaburi kusoma hujui hata kufananisha rangi nako zero??

Kwani chini ya miaka 18 ni miaka mingapi???

Wadau hizi ndiyo type za viongozi wa ccm bila shaka wewe ni kimburumatari wa ccm
 
Ukweli ni kuwa wabakaji wengi tu huachiwa huru,hii inaumiza sana,hakutakiwa kuwa nje ya gereza sasa...pengine ashamwambukiza magonjwa,au mimba,kisaikolojia ndo kabisa kashamuharibu mtoto wa watu....sheria ina wenyewe inaowalenga, ila mbele za haki kwa Mungu kila mtu atapokea sawasawa na matendo yake. Imeniuma sana!
 
Katibu Mwenezi CCM atuhumiwa kumbaka binti yatima………..!!!!!!!!!!!!!!

30 Dec 2011 asubuhi,Katibu mwenezi wa ccm kata ya Bilele anatuhumiwa kubaka mtoto yatima wa umri chini ya miaka 18 katika eneo la Hamugembe Bukoba,baada ya mtoto huyo kwenda kwake kumshitaki kijana mmoja ambaye jina lake halikupatikana aliyeaminika kutaka kumpiga, unyama gani huu jamani.Badala ya Katibu huyo kutoa msaada wa kumwepushia binti huyo kipigo toka kwa kijana huyo yeye akamzawadia kumbaka na kumsababishia maumivu makali yatima huyo masikini ya Mungu. Cha kusikitisha zaidi mpaka leo hii hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa kwa Katibu huyo mbakaji,Polisi wamejitetea kuwa hawakumtia mbaloni mapema kwa sababu taarifa za tukio hilo zilichelewa kuwafikia,mimi na wewe hatujui kama ni kweli hawakupata Taarifa. Sasa Taarifa wanazo tungoje na tuone je hatua zitachukuliwa au ndiyo siasa zitachukua nafasi huku yatima huyu akiumia?

Wale walio karibu na eneo hilo nawaombeni mjaribu kuhakikisha tatizo la yatima huyo linashugulikiwa na vyombo vya sheria na mtuhumiwa anaadhibiwa kwa unyama alioutenda.:juggle::A S 465:

Hawa ndio wanachafua sifa za chama chetu inatakiwa tuwe na kifungu cha sheria mahali kwamba hata ukituhumiwa tu unaachia ngazi YA UONGOZI sasa leo hii yuko arumeru anatutafutia kiongozi mwadilifu KAZI KWELI
 
Back
Top Bottom