Katibu Mkuu TAMISEMI, Mussa Iyombe atoa sababu za wakuu wa wilaya na wakurugenzi kutenguliwa hizi hapa

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhandisi Mussa Iyombe, ametaja sababu za wakuu wa wilaya na wakurugenzi ambao uteuzi wao ulitenguliwa hivi karibuni.

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza na wakuu wa wailya katika kikoa hicho.
Akizungumza jana katika kikao kazi cha wakuu wa wilaya 26 walioteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni, Iyombe alisema miongoni mwa sababu za kutenguliwa huko ni kutojiheshimu.

Alisema wakuu wa wilaya wengi waliondolewa ni kutokana na kugombana na wabunge au wakurugenzi wa halmashauri.

"Unamnyang'anya gari dereva unaendesha wewe au wewe kazi yako ni kugombana tu na wabunge, wakati wewe una kazi zako na mbunge ana kazi zake. Niwaambie tu ukweli wengi walioondoka ni kwa sababu hiyo. Sasa wewe kila siku unagombana na mbunge, serikali gani hiyo ambayo inagombana tu na wawakilishi wa wananchi,"alisema.

Katibu mkuu huyo alisema wakuu hao wa wilaya wanatakiwa kutengeneza mazingira ya haki ni haki na sheria ni sheria na si kuwaweka ndani ovyo watu.

"Umepewa mamlaka hayo lazima uyatumie vizuri maana ukimweka ndani inapaswa kesho umfungulie mashtaka ya kijinai na ni lipi sasa? Unaweza kukuta labda tulikutana huko. Tuligombana enzi hizo, sasa kwa kuwa umepata ukuu wa wilaya unasema ndio atanikoma," alisema.

Iyombe aliwataka kujiepusha na vitendo hivyo na kutunza heshima ya Rais kwa kuwa ana imani sana na wao na anakasirishwa na hali hiyo.

"(Rais) ana vyombo vingi vya kukuangalia wewe. Kwa hiyo mnatakiwa kuwa waangalifu kwenye hizi nafasi zenu. Niwaombe sana nyie muwe ‘model’ (mfano). Kama kuna mtumishi amekosea kuna mamlaka ya nidhamu, iagize tu. Usiende pale ukamweka ndani kwani kuna sheria zinazomlinda huyo si mwanasiasa," alisema.

Alibainisha kuwa kama hajawajibika kuna mamlaka ya nidhamu ya kushughulikia ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo.

"Serikali ina taratibu zake usiziruke na kujiamulia. Angalia imekulinda kisheria, taratibu zimefuatwa hata kama wewe ni mkono wa Rais," alisema na kuongeza kuwa mengi aliyoyaona kwa wakuu wa wilaya waliokuwa wameteuliwa yalikuwa yanatia aibu.

"Wewe mkuu wa wilaya unaitisha kikao vizuri, unaenda saa saba wakati kikao ni saa nne sasa unajenga heshima gani hapo? Unataka uwafundishe nini uliowaita? Nimewatahadharisha haya mambo ya kiutendaji tendaji," alisema huku akiwataka kutunza heshima ya Rais na wanatakiwa kuwa mfano.

Akifungua kikao hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani, Jafo alisema akienda wilayani anakuta mkuu wa wilaya ki vyake, mkurugenzi, mwenyekiti wa halmashauri, mbunge wilaya nzima inafanya kazi kivyake.

"Ukiacha wilaya ambazo nafasi zilizokuwa wazi, hizi zingine zote ukifika uliza utaambiwa kulikuwa na hali gani na maeneo mengi pale utakuta yule aliyeondoka aliyestaafishwa au kuondolewa kuna suala kubwa la uhusiano,"alisema.

Jafo alitaka wakajenge uhusiano na kufanya kazi na kuwatii viongozi wao kwa kuwa maeneo mengine mkuu wa mkoa hataki mkuu wa wilaya aonekane anafanya kazi na analijua hilo.
 
Si kweli, labda tangu wapewe madaraka hawajawahi kuuadhibu/kuuonea/ kuwakejeli wapinzani. Hawajawahi wafanyia unyama wapinzani ndio sababu!
 
Ni jambo jema, ila yule mkurugenzi wa Kinondoni uchache wa mapato umemponza akahamishiwa porini.
 
Wakurugenzi walioondolewa wanaendelea kula mshahara wa ukurugenzi au ndo wameachishwa kazi moja kwa moja?

Kama alitoka mtaani mfano alikuwa mfanyabiashara au alikuwa mtaani tu au Katibu wa Chama cha siasa, baada ya nafasi ya DED kutoka, naye anaishia hapo

Kama alikuwa Mtumishi wa Umma, anarudi kwa RAS wa Mkoa wake au TAMISEMI kwa Katibu Mkuu kupangiwa majukumu mengine BUT mshahara wa DED anaendelea kuwa nao isipokuwa stahiki ndio zinaondolewa.
 
Katika uteuzi wa ma DC hivi karibuni, serikali imewatosa baadhi ya ma DC kwa kukiuka matumizi ya madaraka waliyopewa na utovu wa nidhamu.
Haya yamesemwa na mhandisi Musa Iyombe , Katibu Mkuu TAMISEMI, alipokuwa akiongea na kuwaasa ma DC wapya mjini Dodoma.
Kumekuwepo na abuse ya madaraka ya kuwaweka ndani masaa 48 wananchi ambao ma DC au viongozi wengine wanaona wamekosa.

Tunakumbuka hivi karibuni kitendo cha waziri mdogo wa Maji kuwasweka ndani makandarasi.

Vile vile hata DC Mjema majuzi kumsweka ndani Diwani wa CHADEMA kwa kupishana lugha.

Tukumbuke kuwa Rais alitoa madaraka hayo, na ameona sasa yanatumika vibaya.

Katibu Mkuu Iyombe amesema ma DC wengine wamekuwa "wakiwafanyizia" watu wenye ugomvi nao na hata kutumia vibaya na isivyo ruhusa mali za serikali mfano magari.
Serikali sikivu.
Ref. Nipashe leo 15/08/2018
 
Kumbe ndio hivyo!!!!
Hiyo kauli itamtokea puani......

Hivi anajua kuwa hao maDC na maRC wanapata kiburi hicho cha kuwanyanyasa wawakilishi wa wananchi kutoka kwa Jiwe mwenyewe??

Hivi anajua aliyekuwa Waziri wa ndani, Mwigulu Nchemba, alipotezaje "kibarua" chake??

Ni kwa ajii tu ya kumwajibisha yule msajili wa makanisa, Bi Komba, wakati kumbe ule waraka aliouandika kwa makanisa ili wakanushe ule waraka wa Pasaka, alikuwa amepewa "blessings" na Jiwe!
 
Mimi huwa nadhani Mawaziri hawaoni au wanakubaliana na upumbavu wa wakuu wa wilaya? Sasa mbona matukio yanajirudiarudia kama yanakemewa gizani?
 
KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhandisi Mussa Iyombe, ametaja sababu za wakuu wa wilaya na wakurugenzi ambao uteuzi wao ulitenguliwa hivi karibuni.

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza na wakuu wa wailya katika kikoa hicho.
Akizungumza jana katika kikao kazi cha wakuu wa wilaya 26 walioteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni, Iyombe alisema miongoni mwa sababu za kutenguliwa huko ni kutojiheshimu.

Alisema wakuu wa wilaya wengi waliondolewa ni kutokana na kugombana na wabunge au wakurugenzi wa halmashauri.

"Unamnyang'anya gari dereva unaendesha wewe au wewe kazi yako ni kugombana tu na wabunge, wakati wewe una kazi zako na mbunge ana kazi zake. Niwaambie tu ukweli wengi walioondoka ni kwa sababu hiyo. Sasa wewe kila siku unagombana na mbunge, serikali gani hiyo ambayo inagombana tu na wawakilishi wa wananchi,"alisema.

Katibu mkuu huyo alisema wakuu hao wa wilaya wanatakiwa kutengeneza mazingira ya haki ni haki na sheria ni sheria na si kuwaweka ndani ovyo watu.

"Umepewa mamlaka hayo lazima uyatumie vizuri maana ukimweka ndani inapaswa kesho umfungulie mashtaka ya kijinai na ni lipi sasa? Unaweza kukuta labda tulikutana huko. Tuligombana enzi hizo, sasa kwa kuwa umepata ukuu wa wilaya unasema ndio atanikoma," alisema.

Iyombe aliwataka kujiepusha na vitendo hivyo na kutunza heshima ya Rais kwa kuwa ana imani sana na wao na anakasirishwa na hali hiyo.

"(Rais) ana vyombo vingi vya kukuangalia wewe. Kwa hiyo mnatakiwa kuwa waangalifu kwenye hizi nafasi zenu. Niwaombe sana nyie muwe ‘model’ (mfano). Kama kuna mtumishi amekosea kuna mamlaka ya nidhamu, iagize tu. Usiende pale ukamweka ndani kwani kuna sheria zinazomlinda huyo si mwanasiasa," alisema.

Alibainisha kuwa kama hajawajibika kuna mamlaka ya nidhamu ya kushughulikia ni lazima kufuata sheria na taratibu zilizopo.

"Serikali ina taratibu zake usiziruke na kujiamulia. Angalia imekulinda kisheria, taratibu zimefuatwa hata kama wewe ni mkono wa Rais," alisema na kuongeza kuwa mengi aliyoyaona kwa wakuu wa wilaya waliokuwa wameteuliwa yalikuwa yanatia aibu.

"Wewe mkuu wa wilaya unaitisha kikao vizuri, unaenda saa saba wakati kikao ni saa nne sasa unajenga heshima gani hapo? Unataka uwafundishe nini uliowaita? Nimewatahadharisha haya mambo ya kiutendaji tendaji," alisema huku akiwataka kutunza heshima ya Rais na wanatakiwa kuwa mfano.

Akifungua kikao hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Selemani, Jafo alisema akienda wilayani anakuta mkuu wa wilaya ki vyake, mkurugenzi, mwenyekiti wa halmashauri, mbunge wilaya nzima inafanya kazi kivyake.

"Ukiacha wilaya ambazo nafasi zilizokuwa wazi, hizi zingine zote ukifika uliza utaambiwa kulikuwa na hali gani na maeneo mengi pale utakuta yule aliyeondoka aliyestaafishwa au kuondolewa kuna suala kubwa la uhusiano,"alisema.

Jafo alitaka wakajenge uhusiano na kufanya kazi na kuwatii viongozi wao kwa kuwa maeneo mengine mkuu wa mkoa hataki mkuu wa wilaya aonekane anafanya kazi na analijua hilo.
Solution ni rigorous vetting,kuepuka upendeleo na kuchagua watu wenye experience.Vijana watatuangusha sana,tuwaache wapate uzoefu as they rise up in the employment ladder, baadae wakishakuwa mature ndio wakabidhiwe uongozi.In short let's go back to the basics of appointing leaders.
 
Well said Mkuu, na hapo tatizo kubwa ndo linapoanzia, wewe mtu hata utumishi wa Umma haujui, unampa u DED,RAS,DC utegemee kuwa atafanya vizuri!
 
Siku moja baada ya kukemea tabia ya baadhi ya wakuu wa wilaya kutumia vibaya mamlaka waliyonayo na kuwaweka watu ndani, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amewageukia wakurugenzi watendaji wa halmashauri.

Amewataka wakurugenzi wapya kuepuka kujiingiza katika ugomvi wa kisiasa utakaokuwa chanzo cha kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Jafo akizungumza na wakurugenzi watendaji wapya wa halmashauri jijini Dodoma jana, aliwataka kuepuka kujiingiza katika makundi ya kisiasa na ugomvi usioeleweka ambao utawafanya kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Wakurugenzi hao jana walikula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa watumishi wa umma.
“Simamieni mipaka yenu ya kazi, kila mtu akisimamia mipaka yake kutakuwa hakuna migongano. Ninyi mnaenda huko kwa ajili ya utekelezaji wa ilani ya CCM na hakuna mjadala mwingine,” alisema.

Waziri Jafo alisema, “Msiende kujiingiza katika makundi ya kisiasa na magomvi yasiyoeleweka inawezekana huko mnakokwenda kuna makundi ya kisiasa yanayogombana. Inawezekana huko mnakoenda kuna watu wanagombana simamieni ilani.

“Leo hii unaenda katika halmashauri unamkuta mkurugenzi kivyake, mwenyekiti wa halmashauri kivyake, mbunge kivyake, wakuu wa wilaya kivyao.”

Alisema jambo hilo linafanya halmashauri nayo kwenda kivyake, hivyo utekelezaji wa ilani kuwa mgumu. Alisisitiza uhusiano mwema kazini na ushirikiano akisema, “Kuna baadhi ya watumishi wewe umefika pale ni mgeni, mtu mwingine anakupiga dozi ya sumu iliyokolea hata wengine huwajui kwa sura unaanza kuwachukia.”

Aliwaagiza kutenda haki kwa watu wote na kusimamia miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zinajibiwa kwa wakati.

Juzi, Jafo alikemea tabia ya baadhi ya wakuu wa wilaya kutumia vibaya mamlaka waliyonayo na kuwaweka watu ndani, akisema inasababisha wananchi kuichukia Serikali.

Akizungumza wakati wa kikao kazi na wakuu wa wilaya 27 walioteuliwa hivi karibuni kilicholenga kuwapa maelekezo, aliwataka kuhakikisha wanasoma na kuzielewa sheria zinazowaongoza ili kufanya kazi kwa weledi. “Msiende kuwa vyanzo vya migogoro kwenye wilaya zenu, tumekuwa tukishuhudia migogoro baina ya wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wenyeviti wa halmashauri, makatibu tawala na wabunge. Hatuwezi kwenda hivi, katengenezeni Serikali,” alisema Waziri Jafo.

Ujumbe wa katibu mkuu

Jafo akisema hayo, Katibu Mkuu wa Tamisemi, Mussa Iyombe aliwataka wakurugenzi hao kuhakikisha wanatenga muda wa kuzungumza na watumishi badala ya kuwaachia maofisa utumishi ambao wamekuwa wajeuri.

“Tunapata tabu sana, mkurugenzi haingii ofisini. Ukimtafuta humpati sasa wewe umepewa halmashauri halafu unatafutwa na waziri hupatikani, unatafutwa na katibu mkuu hupatikani, unafanya kazi gani sasa?” alihoji.

“Katika muda wote niliokaa hapa, wakurugenzi hawana urafiki na watumishi. Wanaishia kwa maofisa utumishi, maofisa utumishi wajeuri kwelikweli wanawaharibia sifa lazima mkawaangalie.”

Alisema hali hiyo imewafanya watumishi kusafiri safari ndefu kwenda kumuona waziri wa Tamisemi wakati shida zao zingeweza kumalizwa na mkurugenzi.
 
Naomba kuuliza ni kipengele kipi cha ilani ya chama inatekelezwa mpaka sasa. Labda nmekuwa sielewi vema ilani niisomapo!!
 
..... Akiwa ni mbunge wa Wilaya ya Kisarawe, tunaona juhudi zake za kididimiza vijiji vilivyo chini ya UKAWA, barabara zinazoelekea vijiji hivi hazijawahi kufanyiwa ukarabati huu ukiwa ni mwaka wa tatu ingawa Road Fund wanatoa pesa za matengenezo mara mbili kwa mwaka, makalivati ya kupitisha maji ya mvua barabarani yamevukunjwa, zahanati na shule hazifanyiwi ukarabati, ukweli matatizo ni mengi sana jimboni kwake.
 
Back
Top Bottom