Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,513
- 113,643
Wanabodi,
Kwa Maslahi ya Taifa, Nipashe ya Leo.
Wiki ijayo nitaendelee na ile mada ya wiki iliyopita ya usuluhishi ambao pia itaona jinsi Rais wa JMT, Samia Suluhu Hassani anavyoitumia dhana hii ya usuluhisi na maridhiano kulitibu taifa letu majeraha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Wasalaam.
Paskali
Kwa Maslahi ya Taifa, Nipashe ya Leo.
- Leo ilikuwa niendelee makala ya wiki iliyopita kuhusu upatikana wa haki kupitia dhana ya Usuluhishi, lakini kwa vile makala ya wiki iliyopita ilibeba kichwa cha habari Je Wajua, Mhimili wa Mahakama Usipotenda Haki Unaweza Kushitakiwa?. Pongezi Jaji Mkuu wa Kusisitiza Usuluhishi na Sio Kukimbilia Kufungua Kesi!.” Makala hiyo imeleta sintofahamu kubwa ikiwemo kuushitusha kidogo Mhimili wa Mahakama na mimepokea simu nyingi zikiwemo za kutoka kwa waheshimiwa Majaji wastaafu, kuniulizia ni vifugu gani vya katiba vinavyo ruhusu mahakama kushitakiwa?. Hivyo wanasubiria kwa hamu sehemu hii ya pili ya mwendelezo wa makala hiyo, hivyo naomba leo nisiendelee na hoja ya Usuluhishi, tumalizane kwanza na hili la kuishitaki Mahakama isipotenda haki kwa Watanzania.
- Tangu mwaka huu umeanza, nimejikita zaidi kwenye katiba kwa kusema nitafanya mambo mawili. 1 kutoa elimu ya katiba ili wananchi waifahamu vizuri katiba yao, na katika utoaji wa elimu ya katiba, ( hii kazi nimeianza hapa
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=SSU8Ix5ZjQZEV3
Na katika kuifanya kazi hii, nitalinyeshea mvua paa la nyumba yetu kwa upande wa katiba yetu, ili tujue pale panapovuja, kwa kuyaangazia matundu na matobo ya ukosekanaji wa haki ndani ya katiba yetu, hivyo hapa naendelea kuonyesha baadhi ya matundu na matobo ndani ya katiba, ili hata kama hatuwezi kutandua paa letu lote na kuezeka paa jipya la katibampya, basi angalau, tuyazibe haya baadhi ya matundu na matobo, yanayovuja kwenye paa letu, tusiendelee kuvujiwa na kuloweshwa !. - Serikali inapokosea, Inaweza kushitakiwa mahakamani, hivyo serikali inashitakika, lakini Je Bunge na Mahakama, zinapowakosea Watanzania kama Bunge letu na Mahakama yetu, ilinavyowokosea Watanzania kwenye kuwanyima haki hii muhimu ya kuchagua na kuchaguliwa, hawa tunawashitaki wapi?!.
- Sasa kabla sijaendelea na hii ya Mhimili wa Mahakama usipotenda haki, wananchi wanaweza kuushitaki”, naomba kukiri kuwa haya sii maneno yangu, na hii sii kauli yangu!, hii ni kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, CJ mwenyewe Prof. Ibrahim Hamisi Juma, aliyoitoa Siku ya Sheria nchini mbele Rais Samia aliyekuwa mgeni rasmi, nilichofanya mimi ni kitu kinachoitwa kwa Kiingereza “paraphrasing” kauli ile kwa sentensi moja, hiyo hili la wananchi wanakosa haki kuishitaki mahakama, sio langu, hili ni la Jaji Mkuu mwenyewe, kitu ninachoweza kufanya, ni mimi kama mwanahabari, kumtafuta Jaji Mkuu kwa ufafanuzi.
- Kwa mujibu wa Katiba yetu, nchi yetu inaendeshwa kwa mihimili mitatu, Serikali Bunge na Mahakama. Mihimili hii kila mmoja una nguvu zake na mamlaka yake, inayojitegemea, "independent powers" lakini kila mhimili pia ni mwangalizi wa mhimili mwingine usikiuke mamlaka yake na kupitiliza, kupitia kanuni ya Kiingereza ya "The Doctrine of Separation of Powers, Checks and Balance" ambapo Bunge litaidhibiti serikali na Mahakama, Serikali italidhibiti Bunge na Mahakama, na Mahakama italidhibiti Bunge na Serikali.
- Udhibiti huu unafanyika kwa Serikali ndio inatunga miswada ya sheria na kulipelekea Bunge ndilo lenye mamlaka ya kutunga sheria, Mahakama ndio inatafsiri sheria na kutoa haki na serikali ndie mtekelezaji wa hukumu za mahakama. Serikali ikipendekeza sheria mbaya, Bunge haliipitishi. Serikali inapanga bajeti na kuliomba Bunge kuiidhinisha, kisha Bunge linapelekewa taarifa ya CAG kujiridhisha na matumizi ya serikali. Bunge linaweza tuu kutunga sheria, lakini sheria zinazotungwa na Bunge, haziwi sheria mpaka Mkuu Mhimili wa Serikali atakapo saini sheria hizo. Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, Jaji Mkuu, anateuliwa na Mkuu wa mhimili wa Serikali, na Mtendaji Mkuu wa Bunge, Katibu wa Bunge pia anateuliwa na Mkuu wa Mhimili wa Serikali.
- Bunge ndilo linatunga sheria, lakini Mahakama nayo inatunga sheria, kupitia kitu kinachoitwa "presedents" na serikali pia inatunga sheria kupitia executive orders, na halmashauri zinatunga sheria ndogo by laws, hivyo mtunga sheria sio Bunge Pekee!.
- Mahakama ndio mtafsiri sheria na mhukumu, lakini serikali nayo kupitia mamlaka zake mbalimbali za udhibiti, zinasikiliza mashauri na kutoa hukumu, quasi judicial bodies, na Bunge nalo, linaweza kujigeuza mahakama kupitia kitu kinachoitwa quasi judical bodies, ile kamati ya Bunge ya Kinga na Madaraka ya Bunge inaweza kumuita mtu yoyote, kumhoji na kumfunga hadi kifungo cha miaka 3 jela!.
- Hiyoi hizi kanuni kama za independent powers, na the doctrine of separation of powers, checks and balance, ni kiini macho tuu, Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of "Separation of Powers" Nothing, Just a Myth! ni kuwa ile kauli ya JPM (Mungu amuweke mahala pema peponi, na ameisha muweka maana JPM yuko ...) kuhusu Mhimili uliojichimbia chini zaidi, ni kweli, serikali ndio kila kitu!.
- Wakuu wa mihimili hii yote mitatu, wakienda kinyume cha majukumu yao, wanaadhibika kwa kuondoshwa madarakani, Ibara ya 46A, Bunge linaweza kumuadhibu rais anapofanya makosa kwa kumuondoa Mkuu wa Mhimili wa Serikali madarakani, Bunge pia kupitia ibara ya 53A, linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na waziri Mkuu akaondolewa madarakani, Bunge pia linaweza kumuondoa Spika madarakani kupitia Ibara ya 87 ya Katiba ya JMT, ya mwaka 1977. Na Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, Jaji Mkuu, akifanya makosa, anaweza kuadhibiwa kwa kuondolewa madarakani kwa mujibu wa Ibara ya 110 ya Katiba. Hivyo wakuu wote wa mihimili wasipotimiza wajibu wao, wanaweza kuadhibiwa, kuwajibishwa na kuondolewa madarakani.
- Serikali licha ya kuwa ndio kila kitu, inapofanya makosa ya ukiukaji wa haki za wananchi, inaweza kushitakiwa mahakamani, lakini sio kwa serikali kuwajibishwa, bali kwa serikali kuamriwa na mahakama kutenda haki kwa lazima kupitia amri 6 za kimahakama za certiorari, mandamus, prohibition, (zuio), harbea corpus, quo warranto na procedendo, mtanisamehe amri hizi nyingine zote hazina majina ya Kiswahili wala ya Kiingereza, ni Kilatini tuu!.
- Lakini Bunge lisipotenda haki, na mahakama isipotenda haki, kwa mujibu wa katiba yetu, bado hakuna utaratibu wowote wa kuishitaki mahakamani au popote au kulishitaki Bunge popote!, na ndio maana Bunge letu limekuwa linekuwa linaletewa miswada batili na kinyume cha katiba,
lenyewe linaitunga kuwa sheria wakati ni batili!, yaani Bunge lile lilikuwa kama Bunge puppet kama la mazuzu vile kwa kututungia sheria batili hadi mahakama kuzibatilisha tuu bila Bunge kuwajibishwa!. - Mfano mzuri ni Sheria yetu ya Uchaguzi, yenye kipengele batili cha kulazimisha wagombea kudhaminiwa na chama cha siasa, Mchungaji Mtikila akafungua Kesi No. 5 ya mwaka 1993 kupinga sheria hiyo, Mahakama Kuu ya Tanzania.
- Baada ya Mahakama Kuu kutangaza kipengele hicho ni batili, serikali yetu ya wakati huo, ilifanya mambo mawili makubwa ya ajabu!, kwanza ilikata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu kuibatilisha sheria hiyo!. Sheria ikiishatamkwa na mahakama kuwa ni batili kwa kwenda kinyume cha Katiba, ubatili huo unaanza pale pale baada ya hukumu kwakuwa ubatili huo unakuwa ni umebatilishwa na katiba yenyewe!.
- Kitu cha pili cha ajabu ambacho serikali yetu ni kupeleke Bungeni kwa hati ya dharura, Sheria No. 34 ya mwaka 1994 na kufanya mabadiliko ya 8 ya katiba ya JMT ya mwaka 1977 kuliomba Bunge, likichomekee kipengele hicho batili ndani ya katiba yetu, na kweli Bunge letu tukufu likauchomekea ubatili huo ndani ya katiba yetu!.
- Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri jingine No. 10 la mwaka 1999 kupinga mabadiliko hayo ya 8 ya katiba, na Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutamka mabadiliko hayo ya katiba, kuchomekea kipengele batili kilicho kinyume cha katiba, ni batili.
- Serikali ikakata rufaa kupinga uamuzi huo, na Mahakama ya Rufaa ikakaa chini ya majaji 7, (inaitwa full bench) ikatoa uamuzi wa ajabu kuwahi kutokea Tanzania, ambao pia uliwakosea sana Watanzania, kwakusema “The Court is not the custodian of the will of the people”, ukimaanisha Mahakama sio mlinzi wa katiba ya wananchi!. Mahakama ya Rufani, ikalirudisha jambo hilo kwa Bunge lili lile la mazuri, eti lenyewe ndio lirekebishe kuuondoa ubatili ule!, na matokeo yake mpaka hivi sasa ninapoandika makala hii, sheria batili hiyo bado ipo kwenye sheria zetu, kipengele hicho batili kinachokwenda kinyume cha katiba bado kipo na kinatumika kuwanyima haki ya kuchanguliwa Watanzania mpaka kesho, na ubatili huu uliochomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu, bado upo!, hii maana yake, Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, imechomekewa ubatili ambao ungali upo!.
- Nilisema makala hizi pia zitaangazia matobo ndani ya katiba yetu!. Kama katiba ndio kila kitu.
- Ibara ya 13.- (2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake. Shurti la kudhaminiwa na chama ni shurti baya kabisa la kuwabagua Watanzania wasio na vyama kugombea nafasi za uongozi, na kuwalazimisha Watanzania, wakitaka kugombea uongozi ni lazima wajiunge na vyama hata kama vyama hivyo ni vya hovyo na vinafanya mambo ya hovyo!.
- wananchi, hii maana yake nchi ya Tanzania ni mali ya wananchi wa Tanzania!, Wananchi ndio wenye nchi, ndio wenye katiba, hivyo serikali ni mali ya wananchi, Bunge ni mali ya Wananchi na Mahakama ni mali ya wananchi, vyombo hivi vinapofanya makosa dhidi ya wananchi, lazima kuwepo namna ya wananchi kuviwajibisha, ikibidi kuvishitaki na kuviadhibu kwa kuviwajibisha!.
Wiki ijayo nitaendelee na ile mada ya wiki iliyopita ya usuluhishi ambao pia itaona jinsi Rais wa JMT, Samia Suluhu Hassani anavyoitumia dhana hii ya usuluhisi na maridhiano kulitibu taifa letu majeraha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Wasalaam.
Paskali