Movement: Tunataka Katiba Mpya Tanzania

National "ethos" Ndilo jambo la msiingi kwanza kabla ya maoni. What makes us proud Tanzanian? What makes us different from kenyas etc. Mambo gani ya msingi tunataka yaongoze taifa hili? ambayo kila Kiongozi atafuata?. The frame of reference "paradigm" is wrong and it gives wrong results.....
 
Unaweza vipi kukana kudai serikali tatu, wakati unatoa maoni yanayodai kuwapo kwa mamlaka huru ya Zanzibar, mamlaka huru ya Tanganyika na mamlaka ya Muungano yaliyowekwa wazi maeneo, uwezo, nguvu, utendaji na mipaka ya kila mamlaka? Wanaokataa, wanakataa wanachokubali,


Waanabodi ninakerwa na jambo hili naomba tujadili. Hivi serikali ni nani? Nilidhani ni wananchi ambao wanawakilishwa na bunge?

Kutokana na majadiliano yanayoendelea bungeni kuhusu mikataba ambayo serikali haitaki ijadiliwe sisi kama wananchi ambao tumewachagua wabunge hawa tunapenda kuonyesha msimamo wetu kwa kufanya maandamano ya amani na mkutano mkubwa kutoa msimamo wetu. Mikataba yote ipelekwe bungeni. Sisi wananchi ndio tunasema.

Tanzania kweli ni nchi ajabu sana duniani. Ni kama nchi isio na watu wenye uchungu nchi yao. Jamani mawaziri mnasafiri sana nchi za watu na kuona maendeleo yao. Hivi kweli mna vision kuwa kuna siku Tanzania itaendelea? Ni lazima mfike mahali pa kuona wivu wa maendelo ya nchi siyo yenu binafsi tu. Tafadhali mheshimiwa Mbowe tunaomba uandae mkutano huo na kutoa tamko. Aliye karibu na mheshimiwa tafadhali mpelekee salamu. Msisubiri mpaka wakati wa uchaguzi tu.

" KWA MTAJI HUU NDOTO YA KUWALETEA WATANZANIA WOTE MAISHA BORA NA MEMA HAIWEZEKANI KABISA - IT IS NOT POSSIBLE FULLSTOP"

Sauti za wabunge hawa zisipuuzwe

KAMA kweli wabunge ndio wawakilishi wa wananchi, serikali sasa itaondoa pamba masikioni, itawasikiliza na kutekeleza wanachopendekeza.

Kwa siku nyingi sasa, kilio cha wabunge kuhusu mikataba ya madini na mikataba mingine mikubwa, kimezidi kiwango.

Kilio chao kimevuka mipaka ya kawaida. Kimewagusa hata wale ambao hawakuwa na shauku ya kukisikia.

Wabunge wanataka mikataba ipitiwe. Wanataka kujua kilichomo kwenye mikataba hiyo. Serikali haiwakilishi wananchi. Bunge ndicho chombo cha wananchi.

Wabunge wanapojadili jambo lenye manufaa kwa nchi, wanafanya hivyo kwa niaba ya wananchi wao.

Haiwezekani wabunge wapige kelele za kutaka kupitiwa mikataba, lakini serikali iendelee kuwa jeuri.

Awamu ya Tatu ya uongozi wa taifa hili ilitamba kwa kaulimbiu hewa ya uwazi na ukweli. Hapakuwa na uwazi wala ukweli.

Mikataba ilisainiwa. Wageni wakamilikishwa mali za taifa. Mikataba mingi ya kipuuzi kabisa ikasainiwa. Mzigo wa mikataba hiyo sasa unabebwa na walipa kodi wa nchi hii.

Serikali haikuwa wazi. Ilipuuza maoni ya wananchi, na hata ikafikia hatua ya kuwatisha wabunge waliosimama kidete kuhoji uoza fulani fulani.

Inasikitisha, na kwa kweli inakasirisha, kumsikia leo Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, akiunga mkono kupitiwa upya kwa mikataba ya madini!

Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kuponda wote waliohoji mikataba hiyo, hata akafikia hatua ya kuwaita waliohoji kuwa ni wavivu wa kufikiri.

Waandishi wa habari walioandika au kuhoji mikataba hiyo, walionekana si wazalendo, na ni watu wasiokuwa na maarifa yoyote.

Serikali ya Awamu ya Tatu ilijaa ujuaji na ubabe. Net Group Solution walipingwa mno. Watanzania wengi walisimama kuipinga kampuni hiyo na hata wakurugenzi wake ambao wengi walikuwa vihiyo.

Lakini kilichofanywa na serikali ni kuwaita FFU wenye bunduki na gesi za kutoa machozi, kuwasindikiza Wazungu hao hadi ofisini.

Kimsingi yamefanyika mambo mengi ya ajabu katika nchi hii. Ndiyo maana tunasema kilio hiki cha wabunge sasa, lazima serikali ikifanyie kazi.

Miktaba ya kipuuzi, kwa mfano ya kuukodisha Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwa dola 1,000 kwa mwaka, ni laana isiyosameheka mbele ya Mola.

Hivi kweli Tanzania kwa utajiri wake ina sababu ya kuomba misaada mingi kama ilivyo sasa? Je, kwa ukwasi uliopo, kuna sababu ya watu kufa kwa magonjwa kama malaria?

Laana ya Tanzania ni nini? Je, si kweli kwamba laana ya Tanzania ni viongozi jeuri na wasioambilika? Kama kweli sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, basi sauti hii ya wabunge lazima iheshimiwe. Serikali ipeleke mikataba bungeni.

Katiba yenyewe hii hapa:


Download your copy
 
Mzeewabusara, kama na mimi ningekuwa mmojawapo wa wale wanaoing'ata kwa madaha keki ya Taifa, sijui kama ningekuwa mdomo wazi kupiga kelele!!!

upo msemo wa kikwetu unaosema hakuna mchwa asiyekula fito za nyumba lakini akila nguzo za nyumba amekufa
:pizza: kula kipande wabakishie wenzio
 
Tusikate tamaa, tukazane kwan ni kwa faida zetu na ndugu zetu kwan hizo mali wataziacha hakuna atakae fukiwa na mali zake.
 
Watanzania bana ukweli tunafaa kushukuru kwanza hii hoja ya katiba mpya imekuja mezani nikiwa na maana iko jikoni inashuhughulikiwa lakini nadhani kuna vipengele vingi sana vina faa marekebisho halafu hii system ya wenyewe kwa wenyewe wanakaa kwenye system ya serekali kama sio mtoto wa mjomba basi mtoto wa shangazi watanzania tuko milioni 42 sasa kama sijakosea kuna makabila zaidi ya 120, kwanini hakuna uwiano wa haki sawa jamani kama baba yako alikuwa na bus basi utabaki tu stand kizazi chako chote hili swala mlitazame sana vizuri mungu ibariki Tanzania na watu wake amiiin
 
Swala lingine ambalo linakera sana hili la madawa ya kulevya haswa Mirungi nchi jirani ambayo ni jumuiya ya Afrika Mashariki ndio zao lao kubwa linalowanufaisha wananchi wake, sisi tunayo pia ukanda wote wa usambara mountain imejaa lakini ndio yamewekwa kwenye kundi la madawa ya kulevya, tunaomba hii katiba mpya ipitishe hii miraa kwasababu side effects zake sio sawa na pombe, sigara, ambazo hizo zote ndio zinaongoza kumaliza kizazi chetu pamoja na wanadai ndio wanaongoza kulipa kodi kitu imeandikwa kabisa uvutaji wa sigara inazuru Afya yako hiyo haitufai na pombe hauziwi ukiwa chini ya miaka 18 si kweli.

Ndugu zangu Watanzani wenye mliojaliwa na mungu kukaa huko Dodoma na kutupambania sisi wanyoge jaribu kuangalia haya maoni yetu nashukuru asante
 
Je serikali tatu ni ghali kuliko hizi mbili tulizonazo hivi sasa?
1) Sasa mawaziri wa serikali ya Muungano ambayo inajuisha
(wa Tanganyika)mawaziri waasio wamuungano.. ni Takriban 60.
2)Mawaziri serikali ya muungano
(Shirikisho) watakuwa 10 na wale serikali ya Tanganyika 15. Jumla 25

Je? 60 na 25 ipi ghali?
 
sometyme mcmamo sahihi ndio maamuzi sahihi,wanaokurupuka kutoa maamuzi na kutaka wanayotaka wao bila kujua wananchi tunahitaji nn wanaiuza nchi yao kwa kutumia madaraka yao
 
Muhimu maslahi ya watanzania na sio idadi ya serikali lakini maamuzi ya wananchi ni vyema yajahehimiwa
 
Fikra sahihi hujengwa na watu sahihi hatuna haja ya kukurupuka twende taratibu tutaipata katiba yetu tunayoihitaji. Tukumbuke pia wambili havai moja tumekua na changamoto nyingi katika serikali zetu hizi mbili ya muungano na ya mapinduzi ya z'bar kwahiyo kuongeza serikali ya tatu ni mzigo mwingine tunaoubeba huku akili zetu hazijawa tayari kwa hilo.

Nirahisi kusema twende huko kwenye serikali tatu, lakini je tuna watu sahihi waliojipanga kutupeleka huko binafsi siwaoni sio kutoka tz kwanza wala kutoka UKAWA so tufikirie kwanza majaliwa ya nchi kabla ya kuitumbukiza katika majanga tusiyoweza kujitoa tukumbueke kuwa problems can not be solved with the same level of thinking that cause the problem" kwa hiyo tukijiingiza huko wakututoa hata kuwepo.
 
wakishindwa kabisa kuipata katiba tuliyoitaka wananchi basi tunawaahidi tutaipata kwa hali nyngne. waache wavmbishe mitumbo yao ila siku yao nao inakuja.
 
Watanzania hiki ni kipindi muhimu kabisacha kuweka mshikamanona sio kulet uchonganishi katika huumcahakato wa kuipata katiba mpya kwa ajili yaustawi wa taifa letu
 
Bado katiba mpya wapitishe wanayo ipitisha lakini wajue niya ccm2.wala sio yawananchi kama wanataka muugano udumu selikali Tatu 3.haziepukiki kamwe.
 
Watanzania wachache mnataka kuiingiza nchi yetu ktk machafuko wakati hili jambo kwetu ni ndoto na haya yote yanasababishwa na uroho wa madaraka sasa kwa taarifa yenu nyie mnaojiita ukawa kuendesha nchi mstarajie hata chembe mtaishia kubwata kama mbwa alieuona mfupa wa nyama ccm ni ccm tu vyama vingine visubir kwanza
 
hawa ccm ni ebola kwa taifa letu tukufu na teule la tanzania hawana nia ya dhati ya kujenga nchi bali wanabomoa nchi yetu ila ipo cku watalia na kusaga meno mwanzo mwisho Sitta ni mnafiki ila ataumbuka tu.
 
Back
Top Bottom