Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,570
- 19,447
Hili ni jambo la muhimu sana. Kuna mawazo tuliwahi kuyatapanya huko nyuma kuhusu jambo la aina hii hii. Nitaorodhesha yale yaliyomo kichwani mwangu kwa wakati huu:
machache kwa leo. Kuna mambo mengine kama Muungano na udhibiti wa pesa za umma ambayo yanatakiwa kuwekwa bayana.
(a) Jambo la kwanza kubwa sana tunalotakiwa kufanya ni kupunguza madaraka ya rais; kwa sasa rais wetu ana madaraka makubwa mno. Ikiwa ni pamoja na kuteua baadhi ya wabunge, kuteua majaji, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya. Tumeshaona kuwa Rais anaweza kutumia madaraka hayo kuteua watu wa kumstarehesha binafsi bila kujali utendaji wao wa kazi.
(b) Wateule wote wa Rais wawe wanapitishwa na bunge. Waitwe bungeni wahojiwe kuhusu uwezo wao na ikionekana kuwa mteule hana ubavu wa jukumu analopewa asipistishwe, badala yake rais ashauriwe kuteua mtu mwingine.
(c) Rais asiteua mawaziri wake kutokana na wabunge. Kwa vile uchaguzi wa rais hautegemei wingi wa wabunge wa chama chake, inawezekana rais akatoka kwenye chama ambacho hakina mbunge hata mmoja. Vilevile kuwa na waziri ambao ni wabunge kunapunguza ukali wa bunge katika kufanya kazi yake ya kuisimami serikali.
(d) Kama nyongeza ya (c), Rais asiteue mbunge yeyote.
(e) Wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wasiteuliwe na raisi bali wagombee kama wabunge.
(f) Iundwe tume huru ya utumishi wa serikali ambayo itasimamia watumishi wa serikali wasie politicized. Tume hii isimamie pi vyombo vyote vya dola . Tume iwe inawajibika kwa bunge, siyo kwa rais.
(g) Mikataba yote inayofanywa na serikali iwe inapata baraka za bunge. Bile bunge kukubali mkataba usitekelezwe.