Katiba ya mwaka 77, haiji-contradict kuongelea suala la Tume Huru ya Uchaguzi na hapo hapo kumruhusu Rais kuteua viongozi na watendaji wa tume hiyo?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,115
144,590
Hebu tusome hii ibara ya 74 ya katiba inaohusu Tume ya Uchaguzi alafu tuone kama katiba hii haiji-contradict kwa kumpa mamalaka Raisi wa nchi ambae anatokana na chama cha siasa kuteua viongozi na watendaji wa hii Tume(Ibara ya 74(1) na wakati huo huo katiba hiyo hiyo inaongelea swala la tume hiyo kuwa idara huru(ibara ya 74(7).

Panapotokea mgongano kama huu wa kikatiba,(iwapo niko sahihi kimtazamo),njia gani hutumika kumaliza tatizo hili la vipengele vya katiba vinavyopingana?

Je,huu si ushahidi mwingine kuwa katiba hii haifai kutumika katika mfumo wa vyama vingi na kwamba bado ina vipengelee vinavyofaa kutumika katika mfumo wa chama kimoja?

74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-

(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi yaani-
(a) Waziri au Naibu Waziri;
(b) mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwa mahsusi na sheria iliyotunga na Bunge kwamba ni mwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;
(c) Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madaraka ya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya aya ya (g) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii. (d) Kiongozi wa chama chochote cha siasa.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote katika ya mambo yafuatayo-
(a) Ukimalizika muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa; au
(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.

(5) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.
(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa ni-
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge;
(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge;
(d) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani; (e) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.

(8) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.
 
Hebu tusome hii ibara ya 74 ya katiba inaohusu Tume ya Uchaguzi alafu tuone kama katiba hii haiji-contradict kwa kumpa mamalaka Raisi wa nchi ambae anatokana na chama cha siasa kuteua viongozi na watendaji wa hii Tume na wakati huo huo katiba hiyo hiyo inaongelea swala la tume hiyo kuwa tume huru(ibara ya 74(8).

Panapotokea mgongano kama huu wa kikatiba,(iwapo niko sahihi kimtazamo),njia gani hutumika kumaliza tatizo hili la vipengele vya katiba vinavyopingana?

Je,huu si ushahidi mwingine kuwa katiba hii haifai kutumika katika mfumo wa vyama vingi na kwamba bado ina vipengelee vinavyofaa kutumika katika mfumo wa chama kimoja?

74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-
(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge. (
2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi yaani-
(a) Waziri au Naibu Waziri;
(b) mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwa mahsusi na sheria iliyotunga na Bunge kwamba ni mwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;
(c) Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madaraka ya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya aya ya (g) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii. (d) Kiongozi wa chama chochote cha siasa.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote katika ya mambo yafuatayo-
(a) Ukimalizika muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa; au
(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.
(5) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.
(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa ni-
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
58
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge;
(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge;
(d) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani; (e) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.
(8) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.
Kuna tofauti kati ya Tume ya uchaguzi na Tume Huru ya uchaguzi........NEC ni tume ya uchaguzi!
 
Soma vizuri ibara ya 74(1) na ile ya 74(7).

74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-

(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

74-(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.

Nafikiri,kama inawezekana,wapinzani wafungue kesi ya kikatiba waiombe mahakama itoe tafsiri sahihi ya tume/idara hii kuwa huru huku watendaji wake ni wateule wa raisi na pia watumie mifano ya nchi zingine zenye tume huru kuhoji iwapo tume huru katika nchi hizo,mfano Kenya,watendaji wake wote ni wateule wa Raisi(waangalie namna wenzetu walivyopata tume huru katika nchi zao).

Pia, hukumu ya hivi karibuni ya kupinga ma-DED kuw wasimamizi wa uchaguzi nayo inaweza kutumika kujenga hoja maana m-DED ni wateule wa Raisi na baadhi wameonyesha ukada wao wazi wazi.
 
Hebu tusome hii ibara ya 74 ya katiba inaohusu Tume ya Uchaguzi alafu tuone kama katiba hii haiji-contradict kwa kumpa mamalaka Raisi wa nchi ambae anatokana na chama cha siasa kuteua viongozi na watendaji wa hii Tume(Ibara ya 74(1) na wakati huo huo katiba hiyo hiyo inaongelea swala la tume hiyo kuwa idara huru(ibara ya 74(7).

Panapotokea mgongano kama huu wa kikatiba,(iwapo niko sahihi kimtazamo),njia gani hutumika kumaliza tatizo hili la vipengele vya katiba vinavyopingana?

Je,huu si ushahidi mwingine kuwa katiba hii haifai kutumika katika mfumo wa vyama vingi na kwamba bado ina vipengelee vinavyofaa kutumika katika mfumo wa chama kimoja?

74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:-

(a) Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye atakuwa mwenyekiti;
(b) Makamu Mwenyekiti ambaye atakuwa mtu anayeshika, aliyewahi kushika au anayestahili kuteuliwa kushika madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu au Jaji wa Mahakama ya Rufani;
(c) wajumbe wengine watakaotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge.

2) Rais atamteua Makamu wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kwa kufuata kanuni kwamba endapo Mwenyekiti ni mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano, Makamu wake atakuwa ni mtu anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.

(3) Watu wafuatao hawataweza kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi yaani-
(a) Waziri au Naibu Waziri;
(b) mtu mwenye madaraka ya aina yoyote iliyotajwa mahsusi na sheria iliyotunga na Bunge kwamba ni mwiko kwa mtu mwenye madaraka hayo kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi;
(c) Mbunge, Diwani au mtu mwingine mwenye madaraka ya aina yaliyotajwa na sheria iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa masharti ya aya ya (g) ya ibara ndogo ya (2) ya ibara ya 67 ya Katiba hii. (d) Kiongozi wa chama chochote cha siasa.

(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi atakoma kuwa Mjumbe litokeapo lolote katika ya mambo yafuatayo-
(a) Ukimalizika muda wa miaka mitano tangu alipoteuliwa; au
(b) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mjumbe wa Tume, lingemfanya asiweze kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi.

(5) Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe.
(6) Majukumu ya Tume ya Uchaguzi yatakuwa ni-
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
(a) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(b) kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge;
(c) kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge;
(d) kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura na uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani; (e) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

(7) Kwa madhumuni ya utekelezaji bora wa majukumu yake yaliyoainishwa katika ibara hii, Tume ya Uchaguzi itakuwa ni idara huru inayojitegemea, itafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao, na mtendaji wake mkuu atakuwa ni Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye atateuliwa na kufanya kazi kwa mujibu wa masharti ya sheria iliyotungwa na Bunge.

(8) Bunge laweza kutunga sheria kwa ajili ya kuweka masharti ya kuweka utaratibu wa kusimamia uchaguzi wa Wabunge wanaowakilisha majimbo ya uchaguzi.
Tatizo hata kama hoja yako ikikubalika mahakamani Bunge (la for CCM) ndilo linatakiwa kuanzisha mchakato wa kubadili vipengele husika vya Katiba.
Lazima tukubali kwamba Nyerere aliisuka hii Katiba 'kiujanja' sana. Haifumuliki!
 
Jw,wajumbe kuanzia mwenyekiti na makamu wake hawajawahi kuwa viongozi kwenye vyama au waziri na naibu waziri mf.Ramadhani Mapuri?
 
Hivi kwanini katiba iko hivyo? Kwanini huku inakubali, mbele inakataa au ndio utaratibu wake.
 
Back
Top Bottom