mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Ndugu Wanajamii Forum,
Wakati tukiendelea na maandalizi ya kupata katiba mpya (na sio marekebisho ya katiba) ningependa kushadidia yafuatayo (baadhi ya watu walishayagusia).
1. Hoja ya muundo mpya kabisa wa serikali yetu ya muungano. Hoja ni kwamba tuwe na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania bara na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania visiwani. Rais wa Muungano awe ceremonial leader (asiwe rais mtendaji). Na urais wa Muungano uwe wa kupokezana kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Kwa hiyo Waziri mkuu wa Tanzania Bara atachaguliwa na Wabara tu. Waziri Mkuu wa Zanzibar atachaguliwa na Wanzanzibar tu. Hakuna haja ya Makamu wa rais, ila tuwe na naibu waziri mkuu bara na naibu waziri mkuu zanzibar. Kwa hiyo rais atakuwa mmoja tu na area yake ya influence ni eneo lote la muungano.
Ukiuangalia vizuri huu muundo utaona kwamba utatenda haki kwa namna fulani kwa Zanzibar kuwa na hakika ya kuongoza Muungano km rais kila baada ya kipindi cha miaka kumi. (Niwa kumbushe tu kwamba Nyerere angekuwepo leo Salim Ahmed Salim ndiye angekuwa rais wa Tanzania leo. Tamaa ya Kikwete kungangania urais na kuondoa ule utamaduni Nyerere alioucha wa kupokezana na zanzibar inachangia kwa kiasi kikubwa vuguvugu iliyopo sasa hivi ya Zanzibar kuhisi wanaonewa - CCM hawana namna ya kukwepa lawama hizi.
Kwa kuanzia basi katiba hii iwe zamu ya Zanzibar kuwa rais wa Muungano. Pia muundo huu utapunguza gharama za uendeshaji serikali. Ofisi ya makamu wa rais itaondolewa kwa pande zote. Huu utakuwa muungano wa serikali mbili lakini zote zikiwa zimerenounce sovereignity yake kwa Muungano ambao kimsingi hautakuwa na serikali yake.
Remember: Rais wa Muungano sio rais mtendaji! Interaction ya serikali hizi mbili itakuwa wapi? Bunge ndio litakuwa sehemu ya kuziunganisha serikali hizi mbili. Zanzibar iwe na majimbo ya uchaguzi ambapo wabunge wake wanaingia moja kwa moja kwenye Bunge la Muungano na wawe na wajibu wa kuzungumzia masuala ya zanzibar kwenye bunge la Muungano.
(Lakini baadhi ya majimbo ambayo ni madogo sana hasa upande wa UNGUJA YAUNGANISHWE: Majimbo ya uchaguzi ya Pemba sio tatizo sana. Yana ukubwa ambao ni reasonable). CCM imegawa Unguja katika vijimbo vidogo vidogo kisiasa ili iweze kuwa na viti vingi vya wawakilishi hasa wakati CUF ilipokuwa inatishia salama ya CCM kubaki madarakani.
Wakati huo huo mambo yenye utata kwenye muungano huu yaendelee kupatiwa ufumbuzi wa haraka kabla ya muundo huu kuwa effective yaani November, 2015.
Mnaonaje muundo huu?
email yangu 17441668@sun.ac.za.