Katiba Mpya: Ushauri Kuhusu Muundo wa Serikali ya Muungano

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,452
3,150
Ndugu Wanajamii Forum,
Wakati tukiendelea na maandalizi ya kupata katiba mpya (na sio marekebisho ya katiba) ningependa kushadidia yafuatayo (baadhi ya watu walishayagusia).

1. Hoja ya muundo mpya kabisa wa serikali yetu ya muungano. Hoja ni kwamba tuwe na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania bara na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania visiwani. Rais wa Muungano awe ceremonial leader (asiwe rais mtendaji). Na urais wa Muungano uwe wa kupokezana kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Kwa hiyo Waziri mkuu wa Tanzania Bara atachaguliwa na Wabara tu. Waziri Mkuu wa Zanzibar atachaguliwa na Wanzanzibar tu. Hakuna haja ya Makamu wa rais, ila tuwe na naibu waziri mkuu bara na naibu waziri mkuu zanzibar. Kwa hiyo rais atakuwa mmoja tu na area yake ya influence ni eneo lote la muungano.

Ukiuangalia vizuri huu muundo utaona kwamba utatenda haki kwa namna fulani kwa Zanzibar kuwa na hakika ya kuongoza Muungano km rais kila baada ya kipindi cha miaka kumi. (Niwa kumbushe tu kwamba Nyerere angekuwepo leo Salim Ahmed Salim ndiye angekuwa rais wa Tanzania leo. Tamaa ya Kikwete kungangania urais na kuondoa ule utamaduni Nyerere alioucha wa kupokezana na zanzibar inachangia kwa kiasi kikubwa vuguvugu iliyopo sasa hivi ya Zanzibar kuhisi wanaonewa - CCM hawana namna ya kukwepa lawama hizi.

Kwa kuanzia basi katiba hii iwe zamu ya Zanzibar kuwa rais wa Muungano. Pia muundo huu utapunguza gharama za uendeshaji serikali. Ofisi ya makamu wa rais itaondolewa kwa pande zote. Huu utakuwa muungano wa serikali mbili lakini zote zikiwa zimerenounce sovereignity yake kwa Muungano ambao kimsingi hautakuwa na serikali yake.

Remember: Rais wa Muungano sio rais mtendaji! Interaction ya serikali hizi mbili itakuwa wapi? Bunge ndio litakuwa sehemu ya kuziunganisha serikali hizi mbili. Zanzibar iwe na majimbo ya uchaguzi ambapo wabunge wake wanaingia moja kwa moja kwenye Bunge la Muungano na wawe na wajibu wa kuzungumzia masuala ya zanzibar kwenye bunge la Muungano.

(Lakini baadhi ya majimbo ambayo ni madogo sana hasa upande wa UNGUJA YAUNGANISHWE: Majimbo ya uchaguzi ya Pemba sio tatizo sana. Yana ukubwa ambao ni reasonable). CCM imegawa Unguja katika vijimbo vidogo vidogo kisiasa ili iweze kuwa na viti vingi vya wawakilishi hasa wakati CUF ilipokuwa inatishia salama ya CCM kubaki madarakani.

Wakati huo huo mambo yenye utata kwenye muungano huu yaendelee kupatiwa ufumbuzi wa haraka kabla ya muundo huu kuwa effective yaani November, 2015.
Mnaonaje muundo huu?

email yangu 17441668@sun.ac.za.
 
Ndugu Wanajamii Forum,
Wakati tukiendelea na maandalizi ya kupata katiba mpya (na sio marekebisho ya katiba) ningependa kushadidia yafuatayo (baadhi ya watu walishayagusia).
1. Hoja ya muundo mpya kabisa wa serikali yetu ya muungano. Hoja ni kwamba tuwe na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania bara na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania visiwani. Rais wa Muungano awe ceremonial leader (asiwe rais mtendaji). Na urais wa Muungano uwe wa kupokezana kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. Kwa hiyo Waziri mkuu wa Tanzania Bara atachaguliwa na Wabara tu. Waziri Mkuu wa Zanzibar atachaguliwa na Wanzanzibar tu. Hakuna haja ya Makamu wa rais, ila tuwe na naibu waziri mkuu bara na naibu waziri mkuu zanzibar. Kwa hiyo rais atakuwa mmoja tu na area yake ya influence ni eneo lote la muungano.

Ukiungalia vizuri huu muundo utaona kwamba utatenda haki kwa namna fulani kwa Zanzibar kuwa na hakika ya kuongoza Muungano km rais kila baada ya kipindi cha miaka kumi. (Niwa kumbushe tu kwamba Nyere angekuwepo leo Salim Ahmed Salim ndiye angekuwa rais wa Tanzania leo. Tamaa ya Kikwete kungangania urais na kuondoa ule utamaduni Nyerere alioucha wa kupokezana na zanzibar inachangia kwa kiasi kikubwa vuguvugu iliyopo sasa hivi ya Zanzibar kuhisi wanaonewa - CCM hawana namna ya kukwepa lawama hizi.

Kwa kuanzia basi katiba hii iwe zamu ya Zanzibar kuwa rais wa Muungano. Pia muundo huu utapunguza gharama za uendeshaji serikali. Ofisi ya makamu wa rais itaondolewa kwa pande zote. Huu utakuwa muungano wa serikali mbili lakini zote zikiwa zimerenounce sovereignity yake kwa Muungano ambao kimsingi hautakuwa na serikali yake. Remember: Rais wa Muungano sio rais mtendaji! Interaction ya serikali hizi mbili itakuwa wapi? Bunge ndio litakuwa sehemu ya kuziunganisha serikali hizi mbili. Zanzibar iwe na majimbo ya uchaguzi ambapo wabunge wake wanaingia moja kwa moja kwenye Bunge la Muungano na wawe na wajibu wa kuzungumzia masuala ya zanzibar kwenye bunge la Muungano. (Lakini baadhi ya majimbo ambayo ni madogo sana hasa upande wa UNGUJA YAUNGANISHWE: Mjimbo ya uchaguzi ya Pemba sio tatizo sana. Yana ukubwa ambao ni reasonable). CCM imegawa Unguja katika vijimbo vidogo vidogo kisiasa ili iweze kuwa na viti vingi vya wawakilishi hasa wakati CUF ilipokuwa inatishia salama ya CCM kubaki madarakani.

Wakati huo huo mambo yenye utata kwenye muungano huu yaendelee kupatiwa ufumbuzi wa haraka kabla ya muundo huu kuwa effective yaani November, 2015.
Mnaonaje muundo huu?

Kwanini Watanganyika milioni 40 wakubali kubadilishana uraisi na Wanzanzibar milioni 1 ? demekrasia iko wapi hapa tunatoka kwenye demokrasia tunaenda kwenye katiba ambayo sio watu wanachagua bali ni katiba! kama katiba inapigiwa kura hiki ni kitu ambacho sicha haki. Hakuna mambo ya kupokezana kwani italeta michafuko ileile kwamba Bara wanatoa zaidi inatakiwa kuwa demokrasia.
 
Personaly nafikiri chimbuko la tatizo hili ni tafsiri ya lugha. Kiukweli nchi hizi mbili hazikuungana na hakuna muungano wowote. Muunguna unaopigiwa kelele haupo. Na nashindwa kuelewa ni kwa namna gani watanzania wanashindwa kuelewa hili. Kilichokuwepo ni makubaliano tu ya kushirikiana katika baadhi ya mambo. Ni kawaida kwa nchi au majirani kukubaliana mambo fulani fulani ya kuendesha shughuli mbalimbali.
Kwa mfano mimi na jirani yangu tumekubaliana yeye anapeleka watoto wetu shule na mimi nawafuata watoto wetu kuwarudisha nyumbani. Tumekua tukifanya hivi kwa miaka 3 na tunaenda vizuri. Hii haina maana mji wake na wangu imeungana. kila mtu ana mji wake na taratibu zake, isipokua swala la kupeleka watoto shule.

Nionavyo mimi Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar ni Zanzibar ikila moja ina rais na serikali yake, la kuna mambo walikubaliaba kuyaendesha kwa pamoja mfano swala la ulinzi, Fedha na mambo ya nje.

Na haya maswala hayakutoka mbinguni. Kwa nini tusikae meza moja tujadiliane upya nini tushirikuane na kwa namna gani. Mazingira yamebadilika na hivyo nidhahiri tunahutaji kupitia upya mashirikiano yetu.
 
Ukiwa na Waziri Mkuu mtendaji ina maana nchi hii inaweza kutawaliwa na Malkia. Kule Unguja malalamiko khusu Muungano ni kwamba watu wanasema they were not consulted. Mimi sielewi vizuri kwa nini katiba ilibadilishwa bila referendum,kwa sababu Waaustralia,Wajamaica,na wengine wanabadili katiba kwa referendum ili kuwa Republic. Kwa sababu kuna matatizo,kwa mfano ya sheria,hakuna mtu hapa amepelekwa mahakani akatamani kwamba ni bora angekuwa anahukmiwa kwa sheria za Uingereza au Marekani.
Kwa mfano,mtu anaua anapewa life sentence;ambayo mara nyingi ina maana anafungwa halafu anaachiwa baada ya muda.
 
Kuwa na Rais asiyekuwa na madaraka (ceremonial) na Mawziri Wakuu watendaji ni lugha nyingine ya kusema tuwe na Serikali tatu. Rais awe na madaraka kamili ya utendaji katika nchi nzima na awe na wasaidizi (Makamu) wawili- mmoja kila upande wa Muungano. Umuhunyari
 
Kusema nchi hizi hazikuwahi kuungana ni upotoshaji wa hitoria. Huwezi kuwa na kitu kwa miaka 50 ghfla unaibuka na kudai kuwa kitu hicho hakijawahi kuwapo. Mtu hawezi kuishi na mwanamke kwa zaidi ya miaka hamsini kisha akadai hajawahi kumuoa. Muungano halisi wa Tanzania (kutokana na nchi za Tanganyika na Zanzibar) ni halisi ila unapotoshwa na watu wenye uchu wa madaraka na ukaidi wa kutotambua Mapinduzi ya Zanzibar. UMUHUNYARI (0754910015)
 
Ndugu Wanajamii Forum,
Wakati tukiendelea na maandalizi ya kupata katiba mpya (na sio marekebisho ya katiba) ningependa kushadidia yafuatayo (baadhi ya watu walishayagusia).

1. Hoja ya muundo mpya kabisa wa serikali yetu ya muungano. Hoja ni kwamba tuwe na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania bara na waziri mkuu mtendaji kwa Tanzania visiwani. Rais wa Muungano awe ceremonial leader (asiwe rais mtendaji). Na urais wa Muungano uwe wa kupokezana kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Kwa hiyo Waziri mkuu wa Tanzania Bara atachaguliwa na Wabara tu. Waziri Mkuu wa Zanzibar atachaguliwa na Wanzanzibar tu. Hakuna haja ya Makamu wa rais, ila tuwe na naibu waziri mkuu bara na naibu waziri mkuu zanzibar. Kwa hiyo rais atakuwa mmoja tu na area yake ya influence ni eneo lote la muungano.

Ukiuangalia vizuri huu muundo utaona kwamba utatenda haki kwa namna fulani kwa Zanzibar kuwa na hakika ya kuongoza Muungano km rais kila baada ya kipindi cha miaka kumi. (Niwa kumbushe tu kwamba Nyerere angekuwepo leo Salim Ahmed Salim ndiye angekuwa rais wa Tanzania leo. Tamaa ya Kikwete kungangania urais na kuondoa ule utamaduni Nyerere alioucha wa kupokezana na zanzibar inachangia kwa kiasi kikubwa vuguvugu iliyopo sasa hivi ya Zanzibar kuhisi wanaonewa - CCM hawana namna ya kukwepa lawama hizi.

Kwa kuanzia basi katiba hii iwe zamu ya Zanzibar kuwa rais wa Muungano. Pia muundo huu utapunguza gharama za uendeshaji serikali. Ofisi ya makamu wa rais itaondolewa kwa pande zote. Huu utakuwa muungano wa serikali mbili lakini zote zikiwa zimerenounce sovereignity yake kwa Muungano ambao kimsingi hautakuwa na serikali yake.

Remember: Rais wa Muungano sio rais mtendaji! Interaction ya serikali hizi mbili itakuwa wapi? Bunge ndio litakuwa sehemu ya kuziunganisha serikali hizi mbili. Zanzibar iwe na majimbo ya uchaguzi ambapo wabunge wake wanaingia moja kwa moja kwenye Bunge la Muungano na wawe na wajibu wa kuzungumzia masuala ya zanzibar kwenye bunge la Muungano.

(Lakini baadhi ya majimbo ambayo ni madogo sana hasa upande wa UNGUJA YAUNGANISHWE: Majimbo ya uchaguzi ya Pemba sio tatizo sana. Yana ukubwa ambao ni reasonable). CCM imegawa Unguja katika vijimbo vidogo vidogo kisiasa ili iweze kuwa na viti vingi vya wawakilishi hasa wakati CUF ilipokuwa inatishia salama ya CCM kubaki madarakani.

Wakati huo huo mambo yenye utata kwenye muungano huu yaendelee kupatiwa ufumbuzi wa haraka kabla ya muundo huu kuwa effective yaani November, 2015.
Mnaonaje muundo huu?

email yangu 17441668@sun.ac.za.

Itakuwa kichwani kwako kuna matatizo., kama Waziri mkuu Zanzibar ataiwakilisha Zanzibar kwenye muungano na Tanzania bara Waziri Mkuu awaikilisha Tz Bara kwenye Muungano.,, swali: Huo muungano utaitwaje na ni wa nchi ngapi? na muundo uliopendekeza ni serikali 2? au Kule Tanzania bara wao wataishia shughuli zao kwenye Muungano tu? mana kule Zanzibar serikali yao ya Mapinduzi lazima iwepo.
 
Pamoja na maoni yako lakini:
1. Ikulu ihamie zanzibar
2.Bunge lihamie zanzibar
3.kodi wakusanye zanzibar
 
Mwarobaini wa muungano ni NCHI 1 SERIKALI 1. Serikali 2,3,4 ................ ni kuahirisha tu matatizo ya muungano. Huu UKWELI MCHUNGU hakuna mtu ambaye yuko tayari kuusema.
 
Mwarobaini wa muungano ni NCHI 1 SERIKALI 1. Serikali 2,3,4 ................ ni kuahirisha tu matatizo ya muungano. Huu UKWELI MCHUNGU hakuna mtu ambaye yuko tayari kuusema.

Nakuunga mkono 100% waasisi wetu walisema serikali 2 kuelekea 1, hivi ni kwanini watu wamekuwa wagumu sana wa kuelewa hilo na kulikubali? sasa hivi kuna sehemu Tanzania bara ambayo wazanzibar hususani wapemba hawaishia na kuendesha shughuli zao? suala la kufananisha nchi nyingine zilizounga halina maana kwani watz na wazenj ni ndugu kabisa. kwa nini turudi nyuma na kugaanyika kiinchi?kama si laana ni nini? Tusijifanye kizazi hiki tuna akili sana za kuona mbele kuliko waasisi wetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom