oba
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 310
- 65
Wajameni, katika pita pita yangu kwenye mtandao nimekutana na maoni yafuatayo ya mtanzania mmoja juu ya katiba mpya;
Yafuatayo ni maoni yangu;
1. Rais apunguziwe madaraka katika uteuzi wa viongozi waandamizi wa serikali au mahakama
2. Nafasi ya spika wa bunge iwe ni kwa mtanzania yeyote mwenye sifa na huyo mtu atume maombi kwenye kamati maalumu ya bunge, asiwe mbunge wa jimbo au chama chochote ili kuepusha mgongano wa maslahi wakati akitekeleza wajibu wake
3. Mawaziri wasiwe wabunge ili kurahisisha bunge kuisimamia serikali na kuondoa mgongano wa maslahi bungeni.
4. Ubunge wa viti maalum uvunjwe kwani kama mawaziri hawatakuwa wabunge, Rais hatakuwa na haja ya kuteua watu kadhaa kuwa wabunge ili wamsaidie kutawala.
5. Wakuu wa mikoa na wilaya wasiteuliwe na raisi, la ikiwezekana nafasi hizo ziondolewe.
6. Muungano wa Tanganyika na zanzibar uwe na serikali moja, Pemba liwe jimbo na unguja liwe jimbo katika serikali moja tu. Tanzania bara igawanywe pia katika majimbo. Kila jimbo liwe na seneta na utawala wa ndani na liluhusiwe kuwa na serikali kulingana na uhitaji wake. Serikali kuu iwe na wizara chache tu kama ulinzi, fedha, ndani, nje na afya nyingine ziendeshwe na majimbo husika kulingana na uhitaji wa kila jimbo
7. Kama serikali moja haiwezekani basi muungano uvunjwe; hakuna sababu ya kuwa na serikali tatu kwani zitaongeza mzigo kwa wananchi wa kuziendesha, serikali mbili zimeshindwa kuleta muungano halisi.
8. Wataalamu wa sekta mbalimbali wapewe vipaumbele na ikiwezekana wathaminiwe kuliko wanasiasa, hiyo itaongeza uzalendo kwa wataalamu hao ambao tunawahitaji zaidi kuliko wanasiassa.
9. Madiwani na wabunge wawe wasomi wa japo degree moja, hiyo itawawezesha kudadavua hoja zinazoletwa na wataalamu walio chini yao. Tofauti na sasa ambapo mbunge std VII anapewa jukumu la kuchallenge utalaamu wa injinia au daktari na ikiwezekana kuupinga huku uelewa wake ukiwa ni wa chini kwa ujumla au katika eneo lile.
10. Nchi hii haina dini na itabaki hivyo...suala la mambo ya dini fulani kama mahakama ya kadhi au mabaraza ya dini fulani yaachiwe waumini wa dini hiyo na serikali isijihusishe na mambo hayo. Itoe uhuru wa kila dini kuendesha mambo yanayoihusu bila kuathiri sheria za nchi wala usalama wa watu wa dini nyingine
Nitafurahi maoni yangu yakizingatiwa
My take; Tume husika inafuatilia mijadala hii kwa uhakika?