Kati ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, Wakili Kibatala anasimama na ACT Wazalendo

Na ndiyo maana, binafsi nawasihi saaaana CHADEMA, waelekeze nguvu zao kwa wananchi. Wananchi wanatakiwa wayajue vyema haya yote na ubabaishaji mwingi unaotumiwa na CCM kuwalaghai wananchi.
Bila wananchi kuamua, hakuna kitakachofanyika. CHADEMA na wengineo wanaotafuta haki wataendelea kukandamizwa tu, na CCM wakiendeleza ya kwao.
Ujumbe huu ufike kwa Wazalendo, WanaChadema na wote wanaolitakia mema taifa letu.

WANANCHI AMKENI! Usingizi wenu unatumika kwa faida ya wajanja wachache wanaoendekeza mikorogano ya Kikatiba inayozidi kututumbukiza kwenye mnyororo wa social dilemmas!
 
Simpo sana mbona... Ni kususpend tume iliyopo na kukasimu majukumu hayo kwa tume ya mpito.
Amin amin nawaambia... Tume Huru nje ya Katiba ni nia ovu zaidi! Kumbuka kuwa hiyo tume bado itateuliwa na Rais wa JMT ambaye ni mwenyekiti wa ccm isiyotaka Katiba Mpya.

Kuweni makini sana.
Kwa hiyonukisuspend itakuwa imeteuliwa na nani?

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Tume huru inatusaidia nini ikiwa bado Polisi wanakuja na mitutu na kuondoa mawakala vituo vya kupigia kura?

Hili nalo linahitaji Akili ya chuo kikuu?

Katiba mpya iwafanye watu wa stick kwenye viapo vyao.

Watu wa kusimamia haki wasimamie haki.

Tuache kiini macho.,
Na ikiwa hakutakuwa na Polisi kwenye vituo wananchi wakapinga kura na Tume ikatangaza matokeo tofauti kama ifanyavyo Sasa utakuwa na Jambo gani la kuizuia?

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Mtazamo wangu ni kuwa na Katiba mpya kwanza itakayojenga mifumo na taasisi huru ili tume huru iweze kufanya kazi kama ilivyotarajiwa. Kenya walifanya hivyo, Ghana wamefanya hivyo na S.Africa pia

Swali ambalo ACT-Wazalendo hawalijibu ni moja. Kwamba, wakati huo wakiwa CUF ya maalimu walikuwa na tume huru ikishirikisha CCM na CUF. Uchaguzi wa 2015 Jecha alibanwa na tumbo akachukuliwa na vyombo husika akatengenezewa mazingira husika hadi leo ni ''celebrate'

CUF hawakuweza kwenda Mahakamani, hawakuweza kupata haki yoyote ile kwasababu mifumo iliyopo bado inailinda CCM.

ACT wanapodai tume huru leo yale ya 2015 na Jecha wanatueleza nini?

Pili, Marhum Maalim Seif alitaka katiba mpya. VP Othman ni muumini hasa wa katiba mpya
Duni Juma, ni muumini wa katiba mpya na ndiye kiongozi wao kama Zitto

Nini kimewakumba leo hawaoni umuhimu wa katiba waliyoitaka miaka iliyopita kiasi cha kutaka tume na hata kujiunga na akina Mrema na Hamada ku sabotage jitihada za kudai katiba?

Yes, ku sabotage kwasababu ukikaa meza moja na Makada hawa wa CCM; Mkandala, Mutung' , Alhad, Hamad Rashid ni kuhalalisha dhulma tu kama ACT inavyojitahidi sasa hivi.

JokaKuu
Joka kuu Kamsikilize Kibatala maoni yake ya kisheria juu ya umuhimu wa Tume huru kabla ya Katiba utajua kwanini ni muhimu kuwa na Tume huru kwanza

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Na ikiwa hakutakuwa na Polisi kwenye vituo wananchi wakapinga kura na Tume ikatangaza matokeo tofauti kama ifanyavyo Sasa utakuwa na Jambo gani la kuizuia?

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Katiba mpya inatoa mipaka ya kila taasisi kiutendaji na nani atamuwajibisha nani.

Swali lako ulilouliza linaonesha dhahiri hufatilii siasa za nchi zingine ambako matokeo hupingwa mahakamani na michakato kusimama ili kupisha uchunguzi.
 
Joka kuu Kamsikilize Kibatala maoni yake ya kisheria juu ya umuhimu wa Tume huru kabla ya Katiba utajua kwanini ni muhimu kuwa na Tume huru kwanza

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Wewe umemsikiliza, lakini hata kuweka mhitasari tu wa alichosema huwezi?

Ni rahisi, tueleze hiyo Tume Huru itapatikana vipi?

Je, Tume Huru' itaweza kuwa huru ikiwa inafanya kazi zake ndani ya "mfumo" usiokuwa rafiki kwake? Elezea UHURU huo itaupata vipi!
 
Katiba mpya inatoa mipaka ya kila taasisi kiutendaji na nani atamuwajibisha nani.

Swali lako ulilouliza linaonesha dhahiri hufatilii siasa za nchi zingine ambako matokeo hupingwa mahakamani na michakato kusimama ili kupisha uchunguzi.
Bado tupo pamoja, licha ya kutaka kujuwa "umri" wangu, sijui kwa nini!
 
Kwa sasa Kuna mjadala wa kipi kianze Kati ya katiba ya wananchi na Tume huru ya Uchaguzi.

Mvutano mkubwa unaonekana katika vyama viwili vya ACT Wazalendo na Chadema.

ACT Wazalendo wanataka ianze Tume huru ya Uchaguzi katika kuiendea katiba mpya na Chadema wanataka katiba mpya kwenye kuiendea Tume huru.

Mawazo yao yamewaingiza katika uadui mkubwa huku upande wa ACT Wazalendo ukijenga hoja ya kwanini ni muhimu kuanza na Tume huru na Chadema wakiwangooshea vidole na kuwatukana wakati mwingine kuwa wanatumiwa na serikali kuihujumu

Katika hatua hii Kuna makundi ya watu wenye ushawishi wametoa maoni yao.

Miongoni mwao ni Maria Sarungi kupitia bunge la Space anayetaka katiba mpya kwa kuungana na Chadema

Lakini wote hao hawasemi wataifikia vipi katiba mpya kutoka katika kura za wananchi hadi tume ya Sasa yenye jukumu la kuhesabu kura za maoni zitakazopigwa.

Kwa upande wa ACT Wazalendo,mawazo yao yanaungwa mkono na wanasheria nguli wa Chadema, Peter Kibatala na Tundu Lissu kuwa ni muhimu kuanza na Tume huru kabla ya Katiba mpya huku wakielezea sababu zao.

Kibatala amesema katika moja ya mahojiano na Clouds Tv kuwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Jaji warioba inataja tume ya uchaguzi ya Taifa NEC na ZEC kuwa ndiyo watakaosimamia kura za maoni kwenye kuipata katiba mpya.

Anasema hiyo tume isipokuwa huru hata wananchi asilimia 98 wakiwa wamepigwa kura ya kuidhinisha katiba mpya tume hizo zinaweza kupindisha ukweli na wananchi wakapoteza haki zao.

Pia Tundu Lissu kwa mlango wa Nyuma amesema mchakato wa Katiba uanze na ikiwa itafikia Uchaguzi wa 2024-25 katiba ikiwa haijaakamilika basi iundwe Tume huru,itakayosimamia Uchaguzi huo.

Kauli yake hii ambayo kwa namna moja ama nyingine imebeba tahadhari zote za kuzuia ukosolewaji ndani ya chama inaashiria wazi tamanio lake ni kuanza na Tume huru kabla ya Katiba mpya.

Kwa hiyo utaona mitazamo ya ACT Wazalendo na hao wanasheria nguli kwa pamoja kwao muhimu ni TUME huru Kwanza kabla ya Katiba.

Na Kibatala amekuwa muwazi zaidi katika hili tofauti na Lissu,anayesema chaguo lake kwa kuzunguka

CHADEMA hawana budi kuwa realistic. Hawana uwezo wa kupata aina ya Katiba wanayoitaka wao, kwasababu hawatakuwa na representation ya kutosha kwenye Bunge la Katiba ambalo tunajua majority ya wajumbe wake ni wale wabunge wa Bunge la kawaida.

CHADEMA waking’ang’ana sana nchi itaishia kupata Katiba waitakayo wale walio na kura nyingi kwenye Bunge la Katiba (CCM).
 
..lakini kuwa confront ktk hilo haisadii ktk harakati za kupata katiba mpya.

..CCM wanataka vyama vya upinzani vipoteze muda kulumbana badala ya kupigania katiba mpya na tume huru.

..jambo la msingi na kupambania tume huru na katiba mpya kwa pamoja.
Kipi kianze sasa kati ya tume na katiba?
 
The state walimwambia mama aanzishe mchakato wa mwendelezo wa katiba mpya kuandikwa ndani ya mwaka jana Hadi mwaka huu!!!na sio tume huru!!Mama anataka kukwepesha mchakato wa katiba Ili imsaidie kupita hapo 2025!!!wenye nchi sio wajinga wanamwangalia tu anavodemka!!!Tena aliambiwa mchakato ukamilike Ili uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 ufanyike chini ya katiba Mpya!!NADHANI THE STATE WAMESHAJUA MAMA HANA MPANGO NA KATIBA ANALETA JANJA JANJA KAMA KAWAIDA YA MAKADA WA CCM WAKISHASHIBA HUWA WANAONA LOLOTE WANAWEZA FANYA !!NADHANI THE STATE WATACHUKUA HATUA ZINAZOSTAHILI!!!KWANI WE MAMA ULIZALIWA UWE RAISI TU NA SIO KINGINE!!??MBONA UNAHAHA SANA!!?FUATA MAELEKEZO WEWE!!!!
 
CHADEMA hawana budi kuwa realistic. Hawana uwezo wa kupata aina ya Katiba wanayoitaka wao, kwasababu hawatakuwa na representation ya kutosha kwenye Bunge la Katiba ambalo tunajua majority ya wajumbe wake ni wale wabunge wa Bunge la kawaida.

CHADEMA waking’ang’ana sana nchi itaishia kupata Katiba waitakayo wale walio na kura nyingi kwenye Bunge la Katiba (CCM).
Hujatoa mapendekezo unayoona wewe yanafaa, bali unawalalamikia CHADEMA, na sina hakika kama unaujua vyema msimamo wanaousimamia wao.
 
Hujatoa mapendekezo unayoona wewe yanafaa, bali unawalalamikia CHADEMA, na sina hakika kama unaujua vyema msimamo wanaousimamia wao.

Kwani hii hoja ina mapendekezo mangapi? Kama nimesema, kwa hali ilivyo sasa hivi, pursuit ya Katiba mpya sio viable, pendekezo lililobaki ni lipi?
 
The state walimwambia mama aanzishe mchakato wa mwendelezo wa katiba mpya kuandikwa ndani ya mwaka jana Hadi mwaka huu!!!na sio tume huru!!Mama anataka kukwepesha mchakato wa katiba Ili imsaidie kupita hapo 2025!!!wenye nchi sio wajinga wanamwangalia tu anavodemka!!!Tena aliambiwa mchakato ukamilike Ili uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 ufanyike chini ya katiba Mpya!!NADHANI THE STATE WAMESHAJUA MAMA HANA MPANGO NA KATIBA ANALETA JANJA JANJA KAMA KAWAIDA YA MAKADA WA CCM WAKISHASHIBA HUWA WANAONA LOLOTE WANAWEZA FANYA !!NADHANI THE STATE WATACHUKUA HATUA ZINAZOSTAHILI!!!KWANI WE MAMA ULIZALIWA UWE RAISI TU NA SIO KINGINE!!??MBONA UNAHAHA SANA!!?FUATA MAELEKEZO WEWE!!!!

Hakuna political will; kilichopo ni unafiki tu. Script itakayotumika ni ileile ya ngonjera ya JK. Na yeye wakati wa muhula wake wa pili ndiyo atasema kinafiki, “tunafufua mchakato wa katiba”. As usual, mchakato utabuma tena kwa disagreements kati ya CCM na Upinzani na maisha yataendelea!
 
Kwani hii hoja ina mapendekezo mangapi? Kama nimesema, kwa hali ilivyo sasa hivi, pursuit ya Katiba mpya sio viable, pendekezo lililobaki ni lipi?
Kwa akili yako, hapo unaona kuna pendekezo?
"Hali ilivyo sasa" ina maana gani, ni hali gani hiyo, na lini utapata hiyo itakayoruhusu "viability" unayoitaka?
 
Hakuna political will; kilichopo ni unafiki tu. Script itakayotumika ni ileile ya ngonjera ya JK. Na yeye wakati wa muhula wake wa pili ndiyo atasema kinafiki, “tunafufua mchakato wa katiba”. As usual, mchakato utabuma tena kwa disagreements kati ya CCM na Upinzani na maisha yataendelea!
Kwa hiyo maana yako ni kuwa watu waache kudai katiba mpya hadi hapo CCM watakapoamua, kwa hiari yao wenyewe kuwepo kwa katiba mpya?
 
Simpo sana mbona... Ni kususpend tume iliyopo na kukasimu majukumu hayo kwa tume ya mpito.
Amin amin nawaambia... Tume Huru nje ya Katiba ni nia ovu zaidi! Kumbuka kuwa hiyo tume bado itateuliwa na Rais wa JMT ambaye ni mwenyekiti wa ccm isiyotaka Katiba Mpya.

Kuweni makini sana.

Naomba kufahamishwa..

Kwa mujibu wa Katiba mpya... Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wanapatikanaje?
 
Back
Top Bottom