Katazo la serikali kuhusu matangazo ya tiba asili/mbadala

pamoja tunashinda

Senior Member
Aug 22, 2015
131
32
Serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia watoto na wazee imetangaza kuanzia leo ni marufuku kwa vyombo vya habari vyote, social media na njia zingine za kupashana habari kutangaza matangazo ya aina yoyote yanayohusu tiba mbadala au tiba asilia.

Nini maoni yako?
 
Naunga mkono. Ijipange kwanza jinsi ya kuweza kudhibiti makanjanja, Tiba mbadala ni nzuri lakini matapeli wamekuwa wengi kuzidi proffessionals, maisha ya watanzania yako hatarini. Nashauri waangalie pia makanisa yanayotangaza uponyaji na miujiza kuliko hata habari za uzima ambayo ndio core issue yao.
 
Serikali kwa namna moja ama nyingine inakosea.

Ingeanza na usajiri wa watoa tiba lishe na baada ya hapo ingeagiza kila mwenye tangazo ni lazima.alipitishe wizarani ila kuhakikiwa.

Hawa jamaa sometimes wanamafundisho mazuri ambayo kupitia kwayo tunajitibu na tunajiepusha na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ya kuambukiza pia
 
Hi serikali haina kichwa wala miguu si bure,duniani kote tiba asili zipo.badala ya kuweka mazingira ya kutotoa vibali feki eti wanapiga marufuku
kwani hivyo vidonge vya western chanzo chake ni nini ?
 
imeshindwa kuzuia mwenge unaomaliza pesa bila sababu za msingi wameamua kuzuia matangazo ya tiba asilia,hawaoni kama wanakosea na maamuzi yao hayana msingi kwani sioni hasara yoyote iliyoletwa na matangazo ya tiba asilia.
 
Mwenge unahukanaje tiba asilia igusa afya za watu na hawa watu wamekuwa wengi sana na wamekuwa wakijieleza kama madaktari
 
Pamoja na nia nzuri ya serikali katika hili lakini kuna mengi ya kufanya na inahitaji kuwa very precisely kwenye hili la Sivyo serikali itajikuta kwenye mkanganyiko mkubwa sana
Iweke wazi ni matangazo ya namna gani hayaruhusiwi? Isikurupuke kama lile tangazo la level seat kwenye daladala
 
Hii ni siri kali sio serikali. Mbona akili zaidi ni kuweka mazingira salama ya kuepusha hao matapeli wanaowakudia kuwa knock out.. Matokeo yake wananchi wananyimwa haki ya msingi.

Kama kule ulaya viongozi huwa wanalelewa tokea shule kwa watoto wanaoonesha vipaji vya uongozi na uwezo wa kufikiri yaliyo sahihi huku kwetu ili uwe kiongozi uwe mdau wa chama tu hata kama akili ipo jinga. Hizo ndio products zake..
 
Serikali kupitia wizara ya afya, maendeleo ya jamii jinsia watoto na wazee imetangaza kuanzia leo ni marufuku kwa vyombo vya habari vyote, social media na njia zingine za kupashana habari kutangaza matangazo ya aina yoyote yanayohusu tiba mbadala au tiba asilia.

Nini maoni yako?
Hiki ndio inachoweza kufanya si zaidi ya hapo halafu wao hao hao ndio wanakimbilia tiba asili za wachina na wahindi
Badala ya kurekebisha makosa ili tuweze kuwa na cha kwetu wenyewe wao wanapiga marufuku kabisa

Jr
 
Back
Top Bottom