Katavi: Ajinyonga chumbani kwa Watoto wake

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Eden Mwakipesile (49) mchimbaji mdogo wa madini ya dhahabu Mkazi wa Kijiji cha Ibindi Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa ndani ya chumba cha kulala watoto wake kwa kutumia Kamba.

Diwani wa Kata hiyo ya Ibindi Daniel Peter amesema kuwa tukio hilo la kujinyonga kwa mtu huyo limetokea usiku wa kuamkia tarehe 4 April nyumbani kwa marehemu huyo aliyekuwa akiishi na mke wake pamoja na watoto wake.

Amesema kuwa tukio hilo kwenye Kijiji ni la kwanza halija wahi kutokea na limewashitua watu wengi kwani ni nitukio la kusikitisha kwenye Kijiji hicho kwa kuwa huwa sio jambo la kawaida kutokea kwenye Kijiji hicho ambacho watu wake hujishughulisha na sghuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Mke wa marehemu huyo huyo Letiasia Deus ameeleza kuwa kabla ya tukio hilo yeye na marehemu walikuwa wamelala kwenye chumba chaokama ilivyokuwa kawaida yao kulala yeye na mume wake kwenye kitanda kimoja.

Kabla ya tukio hilo marehemu alifika nyumbani kwake akiwa ametoka matembezini majira ya saa tano na nusu usiku na alipofika nyumbani kwake alimwomba mkewe amkologee uji na alifanya hivyo ndipo ilipofika saa sita usiku waliingia ndani ya chumba chao kwa ajiri ya kulala.

Amebainisha kuwa wakati wakiwa wamelala kitandani yeye usingizi ulimpitia hivyo hakuweza kujua mume wake huyo ambae ni marehemu alitoka ndani ya chumba chake muda gani kwani aliposhituka kulikuwa kumekucha na hakuweza muona mume wake ndani ya chumba isipo kuwa alishangaa kuona watoto wao ambao bado umri wao ni mdogo wakiwa wamelala ndani ya chumba hicho.

Letisia ameeleza kuwa baada ya kutomwona mume wake aliamua kutoka nje na kufungua mlango wa chumba cha nyumba ya nje walikuwa wakilala watoto wake na aliweza kupata mshituko baada ya kumwona mume wake akiwa amejinyonga juu ya paa la nyumba kwa kutumia Kamba.
 
Back
Top Bottom