Katambi asema CHADEMA ni sawa na Mgambo JKT, kaamua kujiunga na JWTZ

Elimu nayo inachangia maana hyo mastaz kabebwa sana na jamaa yake anaitwa rchad kwaiyo tusimshangae anavolkpoka
 
Elimu nayo inachangia maana hyo mastaz kabebwa sana na jamaa yake anaitwa rchad kwaiyo tusimshangae anavolkpoka
 
Nilitegemea UVCCM kutumia platform yao leo kugusa valid issues kama uchumi,hali ya usalama(kupotea watu) ila wamegeuza mkutano wao kutoa vijembe kwa upinzani.
Vijana wamefundishwa siasa za hovyo kabisa. hiki ni kizazi cha ovyo kinatengenezwa.
 
Who is Katambi? Hana akili. Anadhani ni nani atakayemwamini msaliti. Leo hapa kesho pale.
Wanaoondoka mahali wanatoka kwalengo maalumu.
Wewe unatoka tu kwa kuwa unahamia jwtz baada ya kupata mafunzo bora chadema ambao ndiomgambo waliokufunza? Shame on you.
 
Patrobas Katambi (Mwenyekiti alieng'atuka BAVICHA) amesema kwa picha ya kijeshi jeshi CHADEMA ni sawa na MGAMBO (hawajaiva kisiasa) na CCM ni jeshi kamili (JWTZ) ndio maana amehamia.

Akizungumza hii leo katika mkutano mkuu wa UVCCM,Katambi amesema Upinzani umeshindwa kujenga Imani mioyoni mwa Watanzania.







Huyu kijana anaropoka hadi CCM wanamshangaa
 
Huyo inawezekana cdm ikamtumia kama shushushu , wanaccm wenzangu tuwe makini kwasababu hadi sasa hakuna cdm makin aliyetoka kule
Yani chadema hii itume shushushu ccm alafu wasijue?

Mkuu nakuhakikishia siku chadema wanatuma shushushu ccm watapata taarifa siku hiyohiyo
 
Huyo inawezekana cdm ikamtumia kama shushushu , wanaccm wenzangu tuwe makini kwasababu hadi sasa hakuna cdm makin aliyetoka kule
CDM hawafikia kiwango hicho. Kiwango chao ni hiki...
 

Attachments

  • Utapeli wa CHADEMA.jpg
    Utapeli wa CHADEMA.jpg
    54.5 KB · Views: 24
Patrobas Katambi (Mwenyekiti alieng'atuka BAVICHA) amesema kwa picha ya kijeshi jeshi CHADEMA ni sawa na MGAMBO (hawajaiva kisiasa) na CCM ni jeshi kamili (JWTZ) ndio maana amehamia.

Akizungumza hii leo katika mkutano mkuu wa UVCCM,Katambi amesema Upinzani umeshindwa kujenga Imani mioyoni mwa Watanzania.







Kama upinzani Tanzania umefikia hapa nani kaufikisha?Yeye kama sehemu ya viongozi wandamizi wa upinzani ameshiriki kwa 100% kuufanya uwe hivi ulivyo!Asijione sehemu ya wanasiasa malaika wakati anatumika na ccm kama mtaji.
Kuisimamia haki na kweli kwa mwanasiasa ni kama ardhi na mbingu siku zote wanasiasa wanasukumwa na maslahi ya utashi wao ndiyo maana pamoja na kelele zote hizo huwezi sikia haya kutoka kwenye kinywa chake
1.Uwepo wa katiba mpya hasa ile polepole alikuwa mshiriki kuiandaa.
2.Kamatakamata ya viongozi wa vyama vya upinzani na wafuasi wao
3.Sababu zipi zilipelekea kuzuia bunge live
4.Fungiafungia magazeti yaliyo na mitazamo tofauti na watawala huku wakiacha magazeti kama tazama,hoja,habarika yakiwatukana akina mbowe.
5.Haongelei tena haki za wafanyakazi wa umma ambao miaka yote 2 ya awamu ya 5 haki zao ziko likizo.
Ingetosha tu yeye kunyamaza maana wenye akili wanajua wanaondoka upinzani kwa ajili ya njaa au ulafi,wanaamini watapata uteuzi kama wa Anna Nghwira,Mrema,Kitila Mkumbo nk.
 
Huyu Jamaa ndo kwisha habari yake,Wanasiasa masilahi kama hawa ni hatari sana kwa taifa,Toka amehama Chama chake cha zamani chadema haimtoki kinyanyi ajifunze kwa Mzee Wasira,Waliohama Chadema ni wengi lakini mbona yeye tu kila akisimama chadema haimtoki au ndo anatembelea njia ya Sh*nza
 
Huyu bwana aangalie sana.....wenzake hawatokagi ivo.

Nimemkubali sana mama Mgwira alivotoka upinzani hajakashifu MTU
Huyu hajui kuwa anajichoresha. Katika huo mkutano hakuna asiyejua kuwa anachokifanya hapo ni unafki.

Anataka watu wapeleke ushahidi wa watu wanaonunuliwa. Inamana yeye clip ya Nasari hajaiona? Au anahisi waluomo kwenye huo ukumbi ni mazuzu na hawajaona ushahidi wa watu wakinunuliwa? Au ameamua kujisahaulisha?? Huyu mnafi huyu.

Anasema hakuna Mbunge aloweka Umeme jimboni. Hii nauli ya kitoto kabisa na haikupaswa kutolewa na mtu aliyeshika nafasi ya juu ktk siasa km yeye. Ni kazi ya Mbunge kusambaza Umeme?? Haoni kuwa anawatukana ccm na serikali yao kwa kutokuwajibika? Huyu alikuwa anagombea Ubunge, inamana km angepewa Angesambaza Umeme hapo shinyanga? Huyu bwana anaukilaza pia.
 
Huyu Jamaa ndo kwisha habari yake,Wanasiasa masilahi kama hawa ni hatari sana kwa taifa,Toka amehama Chama chake cha zamani chadema haimtoki kinyanyi ajifunze kwa Mzee Wasira,Waliohama Chadema ni wengi lakini mbona yeye tu kila akisimama chadema haimtoki au ndo anatembelea njia ya Sh*nza
Nadhan kaambiwa ili aongeze visibility kwa JPM ni lazma aishambulie CDM. Anapoteza muda mana hana uwezo wala sifa ya kuichafua chadema. Alishindwa Dr. Slaa, yeye nani???

Mziki wa CDM hata JPM anaujua na ndo mana wanaingiza had vyombo vya dola viwasaidie mana kwa haki bin haki asubuhi sana tunawapumzisha. Kama Katambi anajifanya haoni ni jinsi gani tunawachezesha CCM nusu uwanja basi atakuwa anafaa apimwe akili.
 
Akili za kushikiwa hizi. Kama mgambo huyo uchwara anahofia nini uchaguzi uwe huru na wa haki?

Anajua kwamba CCM itamfia mikononi mwake kwa kushindwa vibaya sana.

Patrobas Katambi (Mwenyekiti alieng'atuka BAVICHA) amesema kwa picha ya kijeshi jeshi CHADEMA ni sawa na MGAMBO (hawajaiva kisiasa) na CCM ni jeshi kamili (JWTZ) ndio maana amehamia.

Akizungumza hii leo katika mkutano mkuu wa UVCCM,Katambi amesema Upinzani umeshindwa kujenga Imani mioyoni mwa Watanzania.






 
Wanajamvi tumeshuhudia katika siku za karibuni wanasiasa kuhama vyama vyao walivyokuwa wakivitetea kwa muda mrefu na kukimbilia CCM.

Sitaki kuongelea wale wote waliokimbia kutoka upinzani isipokuwa huyu bwana Katambi (aliyekuwa Chairman wa BAVICHA) kwa kauli zake tata kila asimamapo katika jukwaa la CCM.

Miongoni mwa kauli zake ni ile ninamnukuu: "Katika CHADEMA vijana tunatumika kama karai" na nyingine, "CHADEMA ni mgambo mbele ya CCM ambao ni JWTZ".

Nimetafakari kauli za huyu mwanasiasa kijana (japo bado anahitaji kujifunza zaidi) na kugundua kuwa anasumbuliwa na 'KITAMBI' alichoota mara baada ya kuitwa kujiunga na CCM.

Kwanini?

Kwasababu; mosi, huyu kitaaluma ni mwanasheria (yampasa aende law school kama hajaenda bado). Pili, aliaminiwa na CHADEMA akapewa nafasi ya juu ya uongozi miongoni mwazo. Kwa kauli zake hizo inaonyesha Bw. Katambi anapambana ku-justify kuwa kuhama kwake kulikuwa muhimu lakini kumbe anatafuta kuota 'kitambi'. Bw. Katambi amekuwa mropokaji aso sitaha na kauli zisoweza kupigiwa mfano kwani hazina uhusiano wa kimantiki wala kihoja.

BAVICHA/wanaCCM, huyu Bw. Katambi alipokuwa Mwenyekiti wa BAVICHA alishindwa ku-deliver na kama mnakumbuka mara baada ya Tundu Lissu kuumizwa vibaya kwa risasi za moto na watu wasiojulikana alitoa rai kuwa angeongoza vijana wenzie kumwombea apate tahafifu kutoka kwa M/Mungu, lakini alishindwa kabisa kufanya hivyo licha ya marufuku ya Polisi.

Bw. Katambi, kwa sasa ungejikita kujifunza siasa hasa za upande huo kwasasa ili uive ulete hoja kama msomi wa sheria na kiongozi na kiongozi ambaye umewahi kukaa na Kamanda Mbowe. Achana na hoja finyu, kwani unajua kuwa Nchi ina vyombo vya kukamata mafisadi wote, viombe vyombo vya dola viwakamte mafisadi wote dhidi ya taifa letu.

Bw. Katambi, kitambi kinakusumbua, Chukua hatua stahiki..
 
Ni ushauri tu!

Patrobas Katambi wakati unaondoka CHADEMA na kuiacha ofisi ya CHADEMA ghafla kama umekimbizwa tena kwa kusingizia kua unauguliwa na mama yako mzazi, hukutumia busara zaidi yaushamba wa kisiasa uliokujengea taswira mbaya kabisa kulingana na nafasi uliyokua ukiitumikia awali.

Sijaelewa ni kwanini umeondoka CHADEMA na kuanza kutukana matusi ya ajabu, unaponda CHADEMA kama chama pamoja na viongozi wake bila hata kuheshimu viongozi waliokulea kwenye siasa kwa muda uliokuwepo CHADEMA. Bila CHADEMA hakuna aliyekua anakufahamu wewe, ungeondoka kwa heshima tuu bila matusi nafikiri ungejisitiri na kujitunzia heshima yako huko ulipo. Kutukana kote huku ndiko kunapowapa watu hofu kua umehamia ccm kwa kuhongwa na kukaririshwa maneno ya kusema. Huu ndio ukweli kwa namna moja ama nyingine.

Kinachoshangaza wengi ni kwamba baada ya wewe kuondoka CHADEMA, wale vijana wa BAVICHA wakiongozwa na aliyekua makamu mwenyekiti wako ndugu Ole Sosopi waliitisha press na media na kuongea kiuungwana kabisa kua wewe umeondoka kwa utashi wako binafsi na kwa kutumia haki yako ya kikatiba. Wale vijana walijipa moyo na kujitanabahisha kua BAVICHA ni taasisi kua haitatetereka. Sasa wewe ulikosa vipi ustaarabu kama ule wa wenzako viongozi wa BAVICHA badala yake umebaki kujibishana na vijana wa mitandaoni ambao haijulikani kua kweli ni wanachama wa CHADEMA au wafuasi tuu?

Jifunze sana kwa viongozi waliopita ambao waliondoka CHADEMA kwa ustaarabu.Aliondoka Dr Slaa Lakini sikusikia akimtukana Mbowe,aliondoka Zitto lakini sikusikia akimtukana Mbowe au Dr Slaa wakati huo. Hizi ni siasa tuu huijui kesho yako ndugu yangu.Leo CCM ni ya Magufuli lakini kesho hujui itakua ya nani,Leo CHADEMA ni ya Mbowe lakini pia hujui kua kesho itakua ya nani.
 
Back
Top Bottom