Kashfa ya Richmond: Lowassa, Karamagi na Dkt. Msabaha Wajiuzulu

NILIWAITA MAKATIBU WAKUU kutaka kuvunja mkataba wa Richmond lakini Mwanasheria Mkuu Ndugu Mwanyika aliporudi kutoka nje alisema kuwa nimepokea simu kutoka mamlaka ya juu kuwa mkataba usainiwe. Mwisho wa kunukuu. Sisi kama waumini wa CCM tumefadhaishwa na maneno haya na hivyo tunaomba maneno haya yakanushwe katika vyombo vya habari, magazeti na hata kwenye redio vinginevyo huku mitaani hakukaliki.
Sababu za kutaka kukanushwa ni nini ??
1. Kasema uwongo..??
2. Au muda umepita kiasi cha kuufanya uwongo umekuwa kweli..??
3. Hakuwaita hao makatibu wakuu..??
4. Au hakukuwa na amri ya kutokuuvunja mkataba..??
 
Pia ingependeza angeleta nakala za ajenda ya hicho kikao.maana haichekewi kuwa hicho kiao hakikuwahi kufanyika,na kama lilifanyika basi ajenda hazikuwa hiki anachokiongea sasa.

Wanasiasa sio wa kuwaamini kabisa.
 
Mtu mwadilifu siku zote husimama katika ukweli na haki.Kama aliona mkataba wa Richmond una matatizo kwa nini hakugoma kusaini? Na hata kujiuzulu kama aliona watu wanataka asaini ili kulinda hadhi yake ya uadilifu na kulinda mali za umma?

Kusema alishinikizwa kusaini alishinikizwaje? Alishikiwa bastola au? Madhara ya kusaini kisheria si anayajua? Aliyesaini ndiye mhusika mwenyewe au hilo halijui.Kwa taratibu za kikazi hakuna kitu kinachoitwa kushinikizwa kusaini.Mtu anayesaini ana uhuru wa kukubali kusaini au kukataa na hata kujiuzulu akiona kutia sahihi huko kutampa matatizo huyo aliyesaini.

Kama aliidhinisha RICHMOND kusikizia kuwa alipata shinikizo toka juu ni uongo na utapeli mkubwa angegoma kusaini na angejiuzulu na akaeleza sababu za kugoma kusaini na kujiuzulu kuwa ni kwa sababu hataki Richmond leo hii angekuwa shujaa wa kimaadili.Kusaini kunaonyesha mzee mzima alikula pesa aache uongo.Zigo la Richmond analo.
Wewe sio kila wakati unatumia akili ndogo utabaki maskini wa fikra daima.
Unapokuwa kiongozi kuna maslahi ya taifa na maamuzi binafsi.Suala la Richmond halikuwa la maamuzi binafsi kbs.Kusema angegoma unadhani hilo ni suala la kifamilia la kuamua jioni kusipikwe maharage au nyama.Amka usingizini wewe na achana na mawazo mgando.
Pia Ripoti ya Richmond ukisoma hakuna ushaidi wa ofisi ya W/Mkuu kwa nini ilikuwa hivyo mpk akasign.Next time utumie akili kubwa kutafakari.
 
Save that bullcrap to some CDM kid not me please.

Yani unataka mtu aliyeficha uovu wa CCM kwa miaka 8 baada ya kufahamu,if that was the case anyways,ndio apewe nchi?do u even listen to yourself?

Wakati slaa anamwita Lowassa Fisadi hakujua haya unayobwabwaja hapa?wakati viongozi wenu wakuu wooote walipotumia kodi zetu kuzubguka jukwaa baada ya jukwaa kumuambia Lowassa na marafiki zake hamkuyajua hayo?what changed?

Msifanye watu hatunazo.

ivi unaweza kumsema vibaya rais pindi akiwa madarakani ndio mana hata leo ameshindwa kumsema moja kwa moja amebali kusema mamlaka ya juu ndio uelewe hivyo acha unoko elewa haraka uclete mahaba
 
Wadau nadhani tumekuwa na tabia ya kusahau. Kuna wanasema iweje Lowasa amtaje leo mhusika mkuu wa Richmond baada ya kutoka? Ukweli ni kuwa Lowasa alikwisha kulisema hilo ndani ya kikao cha Halmashauri kuu (NEC) kile kinachoitwa kuwa kilikuwa cha mapinduzi ya mwenyekiti na ni Mzee Mkapa aliokoa jahazi kwa kushauri mjadala huo usiendelee.

Ni kuwa Lowasa alisimama na kumuuliza mwenyekiti kwa nini anaruhusu vijana wake wakina Nape na wengine wanazunguka nchi nzima kumwita Gamba na fisadi kwa sababu ya Richmond? Jee yeye binafsi haujui ukweli wa Richmond? Nakumbuka mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga akasimama na kusema kambo hilo lijadiliwe na wote, na wajumbe wengi wakaridhia.

Kwa kuona hatari iliyo mbele yao Mzee Mkapa akamshauri JK asikubali jambo hilo lijadiliwe hadharani kwani linaweza kumuumbua na kusababisha wajumbe kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye ambayo ipo kikatiba ndani ya chama. Mkapa aliona kuwa yale yaliyomtokea Rais Mbeki wa Afrika kusini yaweza kutokea hapa.

Mjadala ukazimwa na kuanzia wakati huo neno Gamba likajifia kifo cha kawaida kisicho na maswali zaidi. Hapo ndio pa kujiuliza, kwanini hawakuendelea kuzungumzia Richmond na kujivua Gamba? Nikuwa kumbe muhusika hakuwa Lowasa bali "Untouchable"
Tatizo la Lowasa ni kama alivyosema Mbowe, ni mkimya sana na hapendi kujibishana jibishana mambo hasa kama anasakamwa. Ana fanya mambo yake kwa kutumia Busara na hekima na sio mkurupukaji ila anahasira. Ndio maana hata mwandishi mmoja jana aliyeleta swali la kishabiki alijibu kwa hasira kidogo.

Sasa ni wazi Richmond sio ya Lowasa ila ina wenyewe na amewaachia wenyewe.
 
Hapa kuna visasi ,kwa ngazi ya Waziri Mkuu ,huwezi kukwepa eti ngazi za juu zimeamuru wakati wewe mwenyewe ni sehemu ya hiyo ngazi! Huyu jamaa hafai amuogope Mungu

Najuwa una uwezo mdogo mno wa kuelewa pamoja na huo udogo wa uwezo unasumbuliwa na tatizo la kukataa kuukubali ukweli unaouona. Yaani unataka kujiaminisha kwamba nafasi ya Waziri mkuu iko sawa na nafasi ya rais? Je unakumbuka sakata la Jairo na ishu ya Pinda? Kama Rais asipotaka kufanya Waziri mkuu anachokiona ni sahihi je waziri mkuu anaweza kumlazimisha? Je Pinda alisemaje bungeni? Na rais aliporudi akafanyaje? Tumia ubongo kufikiri.
 
Unajua mamlaka ya mwanasheria mkuu lakini?

Unajua anaripoti wapi?

Unajua hawezi kuhojiwa wala kushtakiwa kwa ushauri wake?

vyovyote ilivyo uamuzi huzingatia siasa na hali halisi lowasa alijua richmond ni matapeli alikuwa na haki na mamlaka ya kukataa ushauri
 
Ili iweje? hakuyasema hayo alipopewa nafasi ya kujieleza bungeni, badala yake akasepa na kutangaza kujiuzulu? leo nani atamwamini mpenda madaraka huyo?

Watz wanamwamini na wewe peke yako huwezi kubadili huu upepo!!
 
Ili iweje? hakuyasema hayo alipopewa nafasi ya kujieleza bungeni, badala yake akasepa na kutangaza kujiuzulu? leo nani atamwamini mpenda madaraka huyo?

Utaongea sana, ila tukutane October 25 ndo utajua nini maana ya hiki ulichoandika!
 
"Nilitaka kuvunja mkataba wa Richmond baada ya kugundua kuna mashaka ya Upatikanaji wake, Alie husika kuingia mkataba aliomba Lisaa limoja na alipo rudi alisema haya nimeambiwa na mamlaka ilio juu ya ofisi ya Waziri Mkuu nisivunje" .

"Mwenye ushahidi aende mahakamani kama huuna ushahidi plz shut up and keep quite.

#Edward Lowasa
#zuiaGoliLaMkono2015

Mkiendelea kuuliza tunamwaga ugali wote.

Mwambieni nape goli la mkono mwisho bafuni.
 
Save that bullcrap to some CDM kid not me please.

Yani unataka mtu aliyeficha uovu wa CCM kwa miaka 8 baada ya kufahamu,if that was the case anyways,ndio apewe nchi?do u even listen to yourself?

Wakati slaa anamwita Lowassa Fisadi hakujua haya unayobwabwaja hapa?wakati viongozi wenu wakuu wooote walipotumia kodi zetu kuzubguka jukwaa baada ya jukwaa kumuambia Lowassa na marafiki zake hamkuyajua hayo?what changed?

Msifanye watu hatunazo.

Tumia akili unapo argue. Kulieweka hadharani jambo kubwa kama hilo linahitaji uwe na platform sahihi kwa wakati sahihi na haswa ukizingatia mwizi mwenyewe ndiye aliyeshikilia mpini. Hata Mwakyembe mwenyewe alipofika mamlaka ya Waziri mkuu, alipochungulia na kukuta kumbe barabara haishii pale ilibidi afunge breki za mbuzi!
 
Lowassa: Nilipeleka documents kuwa kampuni ya Richmond haikuwa halali. Hizo documents nilizipeleka kwa mwanasheria mkuu Johnson Mwanyika. Lakini baada ya siku tano nilipoona mwanasheria mkuu hatekelezi niliamua kuitisha kikao kilichoongozwa na katibu mkuu kiongozi pamoja na makatibu wakuu wahusika akiwemo mwanasheria mkuu. Tuliongea mengi ila mwanasheria mkuu akaomba pumziko la masaa mawili. Alitoka nje kuongea na simu na aliporudi ndani akasema kuwa mamlaka ya juu imeagiza kuwa Richmond ni halali na kila kitu kiendelee kama ilivyokuwa. Mimi Lowassa ningeongea tena nini?

Sasa huyu lowassa si asema wazi kuwa Richmond ni ya kikweta
 
Back
Top Bottom