Kashfa ya Jairo: Malipo ya zaidi Billioni 1 kusaidia Bajeti ipitishwe - Adai MP Beatrice Shelukindo

Status
Not open for further replies.
Uko sahihi kabisa, hata hivyo, orodha ikipatikana, naamini kabisa kuwa wale wa CDM ndio watakuwa wengi, ndio walengwa wa fungu lile ili walegeze msimamo.
Mungu asaidie wafahamike, mtapata mshangao wa kufa mtu. Usishangae kumkuta JJ M**&ka kwenye list.
Hehehe, hata mimi nahofia sana hilo. Maana hao ndiyo walikuwa target ya ile hongo. Maana wa CCM huwa ni bendera kufuata upepo tu, lakini hawa wa upinzani ndo siku zote huwa wapo kinyume. So inawezekana jamaa wakawa waliwakati hawa wa upinzani ili wapunguze kelele. Na ukiangalia katika wachangiaji, wa CHADEMA yupo mmoja tu. Wasijekuwa waliambiwa wasiseme lolote. Nawaambieni utakuwa ni mshangao hapa.
 
Tatizo CCM wameshindwa kusoma alama za nyakati issue iko motomoto wataka izima kwa rushwa.Najua ni tabia yao kuhonga ili issue zao zipite ila kwa hili walibugi ndo maana wamekamatwa kama mfano

Jamani mnyonge mnyongeni, lakini haki yake apewe. Hapa sijui CCM wanaingiaje. Tukio zima limefanywa na watumishi ambao ndio watendaji tunaowategemea kuitumikia nchi bila ya kujali Chama kilichoko madarakani. Jamani tushughulikieni tatizo la msingi na tusitafute wa kumtupia lawama. Ingekuwa suala hili ni la CCM, Mbunge wake asingelibumbuluwa.
 
Kwangu mie jazba aliyoonesha Mbunge B. Shelukindo jana, nimejaribu kuitafakari nje ya boksi and dwelt the worst case scenario kwamba issue inawezekana sio tu machungu yanayohusu nchi kuwa gizani na giliba za Jairogate bali pia Jimbo la Bumbuli. Sote tunakumbuka yaliyojiri hapo hadi mumwewe Beatrice akafikia ukomo wa uwakilishi wake. Kwa hiyo the buck does not stop with Jairo but rather, ought to stop with Makamba (Junior). Mlengwa anaweza kuwa yeye pia. In the end visasi bana!! Huyu Beatrice ni mojawapo wa watetezi wa ile ya Richmonduli kwa domo lake mwenyewe.

Furthermore, ukubwa wa Jairogate, over a billion madafu unamaanisha neema kubwa kwa wahusika. Lazima wengine walipoyajua haya, ikawauma. Mimi nasema, sio kwa uzalendo tu, bali kwa gia ya GERE! Mbona madudu mengine hao hao wa magamba kwa wingi wao wanayakingia kifua?

Ati leo wamagamba ankerwa na madudu ya Wizara ya Serikali ya Magamba? Utter contradiction and rubbish. Na ya IPTL, KAGODA et al? If I am wrong, well then I am!
 
Kama kampuni iliyopewa dhabuni ya kuhonga inajulikana tatizo liko wapi?serikali ifuate hiyo kampuni then itatoa list ya majina ya watu waliopewa hongo.easy.
Tatizo ni huo uwezekano wa serikali kuamua kufanya hivyo. Ndiyo maana nafikiri kwamba shinikizo hili litoke kwa wale wabunge waliokosa huo mgao. Na zaidi ya yote hiyo kampuni iliyokubali kupewa zabuni ya kuhonga ifutwe kabisa. Hii nchi ina vioja sana, ina hadi kampuni zilizosajiliwa kwa ajili ya kuwaibia wananchi? Sijawahi kuona wala kusikia popote. Na bado utakuta waziri mkuu hajiuzuru. Kwa kuwepo tu kwa hiyo kampuni ya kugawa rushwa, kunatosha kabisa kwa Pinda na Mkurugenzi wa TAKUKURU kujiuzuru.
 
Mimi ninaona vingozi wote wa juu wa hii wizara wasimamishwe, iteuliwe kamati ya kusimamia kila wilaya ili uchunguzi ufanyike. Hapa kuna madodoso makubwa sana yamejificha. Hapa ndipo pa kuanzia maandamano yasiyo na kikoma mpaka watuambie waliochukua hizo posho ni akina nani.
 
Nafikiri sio Wizara ya Nishati peke yake, hii inaonekana ndo kawaida ya wizara zote............

Yap ... K_H umenena : Alichokosea DJ ni kuandika waraka - wengine wanaagiza bila kuandika na michano inakusanywa...

Mara zote huwa nashangazwa na 75% ya wafanyakazi wa Wizara kwenda Bungeni wakati wa Bajeti - kumbe huwa kuna Bilioni moja ya mgao!
 
A public petition should be signed and sent to Parliament for action that those who received should resign and be taken to court.
 
Ni huyu huyu aliyekuwa naibu waziri wakati kina KARAMAGI wanajiuzuru, aliachwa, hakuwajibishwa na kama haitoshi mkubwa wa nchi akampandisha cheo na kumpa WIZARA aongoze, tena wizara nyeti katika nchi! haikuwa bure, kuna kitu!!!! sasa nadhani madhara yanaonekana! aliyetakiwa kuwasilisha bajeti ni waziri au katibu mkuu? je pana uwezekano waziri alikuwa hajui nini kinaendelea? hata kama akienda kurekebisha bajeti bado kuna tatizo! HAPA INAPASWA WAZIRI, NAIBU NA WATENDAJI WAKUU WENGINE WAJIUZURU! BABA WA TAIFA alisema ''aliyetoa rushwa na aliyepokea rushwa wote mazi ga nyanza (yaani wote ni yaleyale!) '' kama ni hukumu waliotoa hiyo michango nao wawajibishwe!
 
Hivi Tanzania kuna TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA!!!??

MIMI NAJUA KUNA TAASISI YA KUWAKINGA NA KUWALINDA WALA RUSHWA +

Pamoja na Kampuni ya Kugawa giza nchini aka TANESCO
 
Katika taarifa za habari kutoka magazeti mbalimbali zinaonyesha kwamba Jairo alifanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwahonga wabunge, na fedha hiyo tayari ilishakabidhiwa kwa kampuni ya kuhonga wabunge iliyopewa zabuni. Kwa mjibu wa taarifa za wizara hiyo, kampuni hiyo ya kutoa hongo imeanza kufanya kazi ya kugawa fedha hizo wiki tatu zilizopita. Tunataka kujua ni wabunge gani waliopokea hiyo fedha, na iwapo kweli walipokea basi na hao pia wajiuzuru, hata kama ni mia moja. Ni bora kufanya uchaguzi upya kuliko kuwa na wabunge wanaohongeka kirahisi.

Ni wazo zuri sana hili. Wote waliotoa rushwa na waliopokea wanastahili kufukuzwa. Lakini wale TAKUKURU taasisi nyingine ambayo ni janga kwa Taifa letu hawatafanya lolote maana kufukuzwa kwa Wabunge hao itakuwa ni pigo kubwa kwa magamba kwani katika uchaguzi wa kupata wabunge hao (kama wanatoka majimboni) basi CCM haitakuwa na hakika kama itapata hata 50% ya majimbo yale. Kwa hiyo watajibaraguza huku na kule na hivyo hao Wabunge wala rushwa hawatachukuliwa hatua zozote zile.
 
Nina wasiwasi Jairo anaweza kujitetea kuwa hiyo ni desturi ya idara kuwachangia maofisa wanaokuwa dodoma wakati wa kusoma budget.

Kigumu hapa ni kiasi cha pesa kinachotakiwa ni kikubwa mno atashindwa kujustify na pia kiasi hicho kinatoka katika fungu lipi la idara husika? Hii pia itaifanya wizara ionekene ina hela nyingi za kuchezea ili hali wanalia hela za maendeleo.

Kwa vyovyote vile wizara nzima imeoza wanatakiwa kusafishwa toka waziri,naibu na makatibu wote. Wakurugenzi wanaweza kuachwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom