Karibuni tuoneshane Dawa za Kiasili za kabila lenu Kwa Picha au maelezo ya Maneno

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,052
71,360
Inawezekana uko Mjini ndio, sema Simatifoni siku hizi hadi vijijini zimezagaa, embu mwambie aliyeko Kijijini akutumie picha ya Mmea wa Kiasili ambao Kikwenu, mnatumia kujitibu kitu fulani.

1. Majani ya Mpapai
Aiseee, ukitaka kuongezea Damu kwa wingi na Kwa Gharama ndogoooo, chukua Majani ya Mpapai, chukua matatu au manne yaoshe vizuri, yakatekate vizuri, Kisha chukua maji Nusu Lita changanya, weka Jikoni yachemke mpaka maji yawe ya rangi ya kijani.

Epuaaa, Kisha acha yapoe. Kunywa Kwa mtu mzima, kunywa Kwa siku nusu Lita ila mtoto anywe mls 10-20 Mara tatu Kwa siku.

Pia inasaidia sana kuimarisha kinga ya mwili, Kwa wanaume inaimarisha mzunguko wa Damu hivo kufanya Mashine Kusimama inakua kama Jiwe

Utanishukuru.

papaya-tree-leaf-1296x728-header~2.jpg




2. Huu Mmea jina nmeusahau, ila picha yake ni hii
Ikitokea unahisi Umekula au umekunywa Chakula kisichofaa yaani Kina dalili za Sumu, tumbo linauma, kuharisha, kichefuchefu basi hii kitu kiboko.

Watajiuliza, mbona kwenye Chai tumemuwekea sumu lakini ni mzima.

Mmea ni huu, unakua na tumaua kama huyo. Huu Mmea ni Kiboko ya Sumu za kulishwa /Kunyweshwa!

Alafu faida yake ingine inaimarisha Uwezo wa nguu za kiume, mashine Inakua nga ngaaa.

IMG-20230507-WA0007.jpg


Uchukue majani hayo na Maua yake, OSHA, Kisha unaweza kubrendi au kama una kakinu kadogo twanga. Baada ya hapo changanya na maji yako safi kabisa ya kunywa halafu kunywa Asubuh-Jioni Glasi Moja Moja.

Kwanza utaanza kujambaaa balaa, Kisha tumbo lako unaponaa, Kwa wengine ambao wameathirika zaidi, wanaweza hata kuharisha.

Ila Sasa ilivyo chungu πŸ˜‚πŸ˜‚, mwarobaini ukasomee!

Karibuni Wakuuu!
 
Kuna demu leo alikuwa amepelekwa hospital na jamaa yake kaambiwa eti hana damu ukizingatia demu Huwa anakula sana tembele chukuchuku na juice ya rozela kesho nampa hii atafute majani ya mpapai 🀣🀣🀣
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ , Tembele ukitaka likuongezee Damu usilipike.


OSHA, Kisha brendi, changanya maji, kunywa !!!.
 
Back
Top Bottom