Karibu tena Prof. Mark Mwandosya...!

Kitendo cha kambi rasmi ya upinzani kupitia zitto kabwe kuungana na bunge kumkaribisha prof.mwandosya ni kitendo cha busara na kama 2kiendelea hivi.hakika 2tafika.naungana nao kumuombea heri mwandosya.

sounds like nonsense

liwalo na liwe
 
Katika kile ambacho kinaweza kuelezwa kuwa ni kumzunguka Spika wa Bunge Anna Makinda kukataa kuongelea mgomo wa madaktari bungeni, Prof Mwandosya amewashauri wabunge kwamba hawawezi kukaa kimya na kujifanya hawaoni tatizo mgogoro wa madaktari unakoipeleka sekta ya afya nchini. Prof Mwandosya amewakumbusha wabunge kwamba japo wao na familia zao wanaweza wakawa wanatibiwa katika hospitali binafsi na kutoathiriwa na mgomo wa madaktari, wanapaswa kuwakumbuka wananchi ambao hawana uwezo wa kwenda hospitali wanazotumia wabunge. Prof Mwandosya amewakumbusha wabunge kwamba ipo siku wao na familia zao wataathirika na kutoshughulikia matatizo ya sekta ya afya yanayokabili taifa hivi sasa, kwa kuwa kuna wakati ubunge wao utakwisha na watakuwa kama wananchi wa kawaida.

Prof akizidi kuchangia hoja ya mgomo wa madaktari, Prof Mwandosya aliongelea pia suala la Lukuvi kupinga hoja za wapinzania kutaka kujadili masuala mbalimbali ya taifa kwa kuomba muongozo kila wakati. Alimkumbusha Lukuvi kwamba hata yeye ni binadamu mtanzania kama wengine ambao suala la afya, elimu na mengine yanayoongelewa na wapinzani yanamgusa.

Prof. Mwandosya aliwakumbusha wabunge kwamba wanapaswa kukumbuka kwamba suala la afya ni muhimu katika kufanikisha maendeleo ya sekta nyingine kama kilimo na elimu. Prof Mwandosya alitoa wito kwa Wabunge na serikali kushughulika na matatizo yanayoikabili sekta ya afya kwa sasa ili kuweza kuiimarisha sekta hiyo na kuipa muelekeo unaofaa wa hapo baadaye. Prof Mwandosya aliwakumbusha wabunge kwamba wabunge wa upinzania wana upendo pia kwa wananchi wa Tanzania, na kwamba inawapasa wabunge wa CCM wasizingatie tu suala la itikadi pale michango inapotolewa na wabunge wa upinzani, bali waichukulie michango hiyo kama inatolewa kwa ajili ya utaifa wa Watanzania.

Prof Mwandosya alimalizia mchango wake Bungeni kwa kuwashukuru wananchi wote kwa ujumla kwa jinsi ambavyo walikuwa na imani kwamba bado angeweza kurudi kwenye afya njema na kuweza kutoa mchango wake kwa maendeleo ya nchi yetu.

Baadaya ya mchango wake huu, Prof Mwandosya alipeana mkono na Naibu kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe, akiashiria kwamba umoja kati ya wabunge wa CCM na upinzani unahitajika ili kuendeleza nchi yetu ya Tanzania.
 
Kaepuka u-chama kajali maslahi na haki za watanzania,ila isiwe nguvu ya soda ikiwezekana ahame kabisa kwa hao magamba
 
nice speech to me haya matatizo yanaikabili seriali hii ya kikwete nmejaribu kuyaangalia n kwamba mengi yake kayarithi kwa waliomtangulia. kwamfano ishu madaktari ni tatizo ambalo ni kubwa na haliwezekani kutatuliwa mara moja kadhalika na yale ya waalim so ni vyema serikali ikaonyesha nia ya kuyatatua hata kwa siku zijazo manake tayari yameshaonekana kuwa magumu.
 
Huu ndio uzalendo bana, si ushabiki tu wakina kichwa cha nywele, lukuvi na mama makinda.
 
nice speech to me haya matatizo yanaikabili seriali hii ya kikwete nmejaribu kuyaangalia n kwamba mengi yake kayarithi kwa waliomtangulia. kwamfano ishu madaktari ni tatizo ambalo ni kubwa na haliwezekani kutatuliwa mara moja kadhalika na yale ya waalim so ni vyema serikali ikaonyesha nia ya kuyatatua hata kwa siku zijazo manake tayari yameshaonekana kuwa magumu.
Mkuu hata hospitali ya taifa nayo ni inshu kuiwekea vifaa vya kisasa, madaktari bingwa kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi! Wangekuwa serious basi wangetoa hata demo moja ya namna ambavyo hospitali zetu zinatakiwa ziwe siyo kuacha kabisa kwa kisingizio cha kurithi matatizo toka awamu zilizopita. Come on Mr. President, we are in 21 century its show time not blah blah time.
 
mungu anawasaidia viongozi wetu,wapinazi wanajaribu kuwaeleza ukweli still hawataki kusikia,haya kawalete mwandosya mtu wa nyumbani kwao,naamin hawatamsikili,wanasuburi Mungu alete malaika labda huyo watamsikiliza????
hongera mwandosya.umetafakari umeamua kufunguka hata kama watachukia bt ulichosema ni kweli.
 
Mwandosya always amekuwa makini sana ktk kuzungumza na kutekeleza majukumu yake, hapendi ushabiki usio na tija, hata jimboni kwake hana ubaguzi ktk shughuli zake
 
Unajua kuna issue za msingi ambazo wabunge wote lazima wasimame kidete na kuacha ushabiki wa chama
Big up Mark my true helo!
 
Mark ni kweli umenena maneno ya busara toka mstari wa kwanza wa hotuba yako nimefurahishwa pia kwa kumuanika wazi mtu ambaye anafanya nchi hii kufika kwenye matatizo haya, ingawa watu wengi labda hawamfahamu ila ni Lukuvi pamoja na mwanasheria wa serekali watu hawa ndio wamepeleka tanzania kuzimu na ninawaombea Mungu awalipe kwa kila maumivu anayopata mwananchi wa tanzania kwenye shida hizi.
Mark Mungu akupe afya na busara katika wakati kama huu ambao asilimia 80% ya magamba wanatumia itikadi kutoa maamuzi kwenye kila hoja za wapinzani huku wakishabikiwa na Madam Spika.
 
well said prof, sasa tunaanza kuona akili kubwa ikianza kujiinua, badala ya kukaaaa kimya na kuruhusu akili ndogo kuharibu nchi
 
Msigwa aliwakumbusha wabunge maneno ya wanafalsafa mashuhuri kuwa:

1. Wasiache akili ndogo kutawala akili kubwa!
2. Problems cannot be solved by the same level of thinking that creates them - akiwa na maana kuwa iko haja kufanya mabadiliko makubwa katika vyombo vyetu vya maamuzi!
 
Waziri Mwandosya ambaye hotuba yake ilikuwa ikikatizwa kwa makofi ya wabunge, aliongeza kuwa moja na la msingi ambalo amejifunza ni kwamba sasa amejua kwamba Wizara ya Afya ni mhimu sana.
“Afya ni mhimu sana, hasa baada ya kuugua…sijui kilimo ndiyo namba moja au elimu, lakini ukiugua kilimo wala elimu huwezi, hata hapa bungeni huwezi kuomba mwongozo wa Spika, kwa hiyo afya kwanza,” alisema.
Aliwashauri wabunge kuendelea kupima afya zao, akisema kuwa kwa miaka 45 alikuwa hajawahi kulazwa hospitalini, lakini amekiona kitanda huko Hadrabad nchini India alipokwenda kutibiwa, maana awali alijiona ni mtu mwenye afya na mazoezi sana.
“ Sasa naomba pia tuangalie afya zetu hata baada ya kustaafu, maana tunajisikia tuko wazima tunapozungumza sana, lakini baada ya kumaliza je, tumeingia mkondo gani wa afya? Katika taratibu za afya nchini ni jambo la muhimu,” alihitimisha Waziri Mwandosya.
Baada ya kuhitimisha,
 
nmeipenda sana speech ya Mh. Mark atleast imeonyesha picha kuwa kumbe ndani ya magamba kuna magwanda big up Mh.
 
Jk hajali huyo
pinda ndo kasema liwalo na liwe
nape anasema chadema wanapandikiza madr!
 
Back
Top Bottom