Kardinali Protase Rugambwa, hadithi ya wanawali kumi, na teolojia ya utunzaji wa rasilimali

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478


Katika homilia yake ya kwanza kama Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Tabora, Kardinali Rugambwa, amehusianisha hadithi ya wanawali kumi na utunzaji wa rasilimali za nchi katika namba yenye kufikirisha sana. Nitajaribu kueleza nilichoelewa kutokana na homilia yake.

"Wanawali Kumi" ni mojawapo ya hadithi za Yesu katika Agano Jipya la Biblia, hasa katika enjili ya Mathayo 25:13.

Katika hadithi hii Yesu alisimulia kuhusu wasichana kumi walioenda kwenye harusi. Walimngoja bwana harusi aje na kuwakaribisha ndani. Hawakujua ni saa ngapi angekuja.

Wanawake wale kumi walikuwa na taa za mafuta. Watano kati yao walikuwa na busara. Walikuwa wamebeba mafuta ya ziada kama akiba.

Wanawake wengine watano walikuwa wapumbavu. Walikuwa na mafuta yaliyokuwa ndani ya taa zao pasipo akiba.

Bwana harusi alisubiriwa lakini hakuja kwa muda mrefu. Mafuta ndani ya taa yaliisha. Wanawake watano wenye busara waliokuwa na mafuta ya ziada ya wakaweka ndani ya taa zao.

Wanawake watano wapumbavu walilazimika kwenda kununua mafuta ya ziada. Walipokuwa wameenda, bwana harusi alikuja. Aliwakaribisha wanawake watano wenye busara kwenye harusi.

Wakati wanawake watano wapumbavu waliporejea, mlango ulikuwa umefungwa. Hawakuweza kuingia kwenye harusi.

Kwa mujibu wa tafsiri ya Kardinali Rugambwa, hadithi inatoa somo lifuatalo kwa viongozi waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi:

"Maendeleo ya kitaifa katika Afrika" ni kama bwana harusi katika hadithi hii.

"Serikali za mataifa ya Afrika" ni kama wale wanawake kumi.

Na "rasilimali" za nchi ni kama mafuta katika hadithi hii. Kazi ya kutafuta "maendeleo" ni kama kazi ya kumsubiri bwana harusi.

"Serikali za mataifa ya Afrika" zitakazogawa kiholela rasilimali za watu wake kwa wageni hazitakuwa na akiba inayoziruhusu kukesha kwa muda wa kutosha wakati zikisubiri kumwona bwana harusi mtarajiwa, yaani "Maendeleo ya kitaifa."

Nawaslisha.
 
Tunaendelea kusubiri matokeaya maamuzi ya viongozi wetu, huku tukiwa na marejeo ya matokeo ya viongozi walio tangulia.
Kwa kua jana sio leo na kesho sio leo pia , huwenda matokeo ya jana kwenye maamuzi tulio nayo leo yakawa tofauti kabisa na matokeo ya leo ifikapo kesho.
 
Back
Top Bottom