Kanusho la habari potofu katika Tanzania Daima - 'JK alinda mawaziri'

Aisee yale yale ya kesi ya Lema, nahisi kurugenzi hii kazi yake ni kukanusha uvumi wa kweli
 
Mbona kwenye bajeti ya safari ya Rais kulikuwa na bajeti ya mawasiliano? Je imekwenda wapi? Kwa nini asingewasiliana nao akiwa huko huko?
 
wewe husomi contents? acha kuuliza maswali ya kitoto

Kama huna jibu kaa kimya! Kwani hujui Kikwete na wenzake hapo wanakanusha habari za ukweli na kuuambia umma habari za uongo? Akiwa kwenye sherehe za maadhimisho ya CCM Dodoma alisema hamfahamu mmiliki wa Richmond wala wa Dowans, lakini kwenye NEC Lowassa akasemaje?
 


SUNDAY, APRIL 22, 2012

KANUSHO LA HABARI POTOFU KATIKA TANZANIA DAIMA AMBALO LEO LINA KICHWA CHA HABARI KISOMEKACHO "JK.ALINDA MAWAZIRI"



download.png



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Tanzania Daima la leo Jumapili Aprili 22, 2012 lina habari katika ukurasa wake wa mbele yenye kichwa cha habari ‘JK alinda Mawaziri’, inayodai kumekuwa na mazungumzo baina ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kuhusu hatua inayopaswa kuchukuliwa dhidi ya mawaziri waliotakiwa kujiuzulu.

Habari hiyo imedai kuwa Mhe. Pinda anataka mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma waondoke ili kuleta uwajibikaji serikalini, lakini, imeendelea kudai habari hiyo, “Rais Kikwete amesema mawaziri hao waachwe waendelee na kazi zao, kwa kuwa suala hili ni la upepo tu, liachwe litapita”.

Tunachukua nafasi hii kuweka bayana kwamba habari katika hilo hazeti la Tanzania Daima Jumapili si za kweli, bali ni za uzushi na upotoshaji mkubwa.

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, amerejea jana Aprili 21, 2012 jioni. Hajaonana wala kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mhe. Pinda.

Hivi sasa Mhe. Rais anasubiri kupata taarifa rasmi kutoka Bungeni Dodoma.

Mhe Rais anawasihi wananchi wasiamini habari hizo za upotoshaji zilizomo kwenye gazeti hilo la Tanzania Daima Jumapili.

Pia ametoa rai kwa wanahabari wasitoke nje ya mstari wa weledi katika kutekeleza kazi zao ili kuendelea kulinda heshima zao binafsi, vyombo wanavyofanyia kazi pamoja na taaluma yenyewe.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Aprili, 2012



Upepo tu! Je upepo huo ni wa Kusi au Kaskazi. Hatujaelewa bado, jipangani mtueleweshe vizuri.
 
Ikulu ni wazushi sana,hapa kuna mawili na ndio yananifanya nitamke kuwa Ikulu ya Dar es Salaam ni wazushi.
1.Kweli Rais na Waziri Mkuu walinena kama taarifa ya gazeti inavyobainisha.
AU
2.Hakujafanyika mawasiliano baina ya waheshimiwa hao.

Kama mawasiliano hayakufanyika kwa nini wasilishitaki gazeti la Tanzania Daima au kulifuta kwa kupotisha umma?
NA
Kama mawasiliano yalifanyika basi tujue hakuna hatua ambayo itachukuliwa juu ya mawaziri,maana kama gazeti tu halijachukuliwa hatua kali sembuse mawaziri waliowekwa barazani na rais!
 
Rais ana uwezo kuwasiliana na watu wa malawi kuliko watanzania
 
Kwanza nataka kusema sitaki kumtetea Kikwete kwa namna yoyote, bali nataka tuangalie matatizo yetu kwa upana zaidi.

Hapa kuona mtu kama Kikwete kapanda ngazi zote hizo na kafika hapo alipo, hata tukimlaumu vipi, tukae tukijua kwamba maana yake ni kwamba matatizo yetu ni zaidi ya Kikwete.

Tuna matatizo katika mfumo wa elimu unaompa mtu shahada ya uchumi bila ya kumpa elimu sio tu ya uchumi, bali hata ya kujieleza kiasi kwamba alipoulizwa "kwa nini Tanzania ni masikini" alikosa jibu na kujibu hajui. You should have seen Bob Geldof - if you haven't, ilikuwa aibu.

Kuna matatizo katika jeshi letu kama mtu bogus kama Kikwete anaweza kupanda ngazi kufika hapo alipo. Vivyo hivyo katika intelligence system, chama, civil society, bunge na mfumo mzima wa siasa.

Ni rahisi sana kumnyooshea kidole Kikwete, ni vigumu kukumbuka kwamba bila mifumo yetu dhaifu Kikwete angeishia kuwa katibu wa chama wa wilaya tu, if that.

Mie mpaka leo nikimsikia Kikwete anajieleza siishi kujiuliza maswali hivi mtu kama huyu amepitapitaje Chuo Kikuu na kupata shahada ya Uchumi? Mwalimu wake alikuwa nani? Au kasoma kama kada wa chama kapitishwa pitishwa, akaingia bungeni viti maalum, kuanzia hapo aka suck up kwa wakubwa na kuwa promoted tu kwa sababu nchi yetu haiko sana katika kuangalia merit? That's the only explanation to me.

Mzee, Kikwete ni mfano tu wa aina ya watanzania wengi walioko sehemu waliko kupitia mfumo wa kiujanjaunja.
Imekuwa bahati mbaya kwa Kikwete kwamba yeye ni rais na anaonyesha udhaifu wake hadharani.
Lakini mzee hakika nakwambia, yeye ni mfano tu wa "uozo" uliopo sehemu mbalimbali, kuanzia kwenye taasisi za elimu ya juu hadi kwenye ofisi na idara mbalimbali za serikali. Hujawahi kukutana na profesa wa kitanzania, ambaye ukimsikiliza huamini kile kinachozungumzwa kinatoka kinywani kwa profesa?

Ndiyo maana kuna profesa mmoja pale UDSM alishawahi kuniambia kwamba, kuna maprofesa wa kitanzania anawafahamu wakienda Ulaya na Marekani katika mikutano na mihadhara mbalimbali, uwa hawajitambulishi kama maprofesa, pengine watajibanza na title ya "udaktari".

Kwa hiyo ni vyema kwamba umechokoza mada ya msingi sana.
 
Back
Top Bottom