Kanusho: Aliyepigwa na Ndugai afariki dunia!

Status
Not open for further replies.
Aliyekuwa Naibu Speaker Job Ndugai amempiga Fimbo ya Kichwani Mtia nia Dkt Joseph Chilongani eneo la Kata ya Ugogoni na amekimbizwa Hospitali ya Kongwa
Mkuu wa Wilaya na Katibu wa CCM Kongwa wamekimbilia huko kumuona !!!!!!!


Hatimaye Mheshimiwa Ndugai amechimbia kaburi la kisiasa baada ya kumshambulia Mgombea mwenzake aitwae Dr Joseph Elieza Chilongani kwa gongo katika mkutano wa kuomba kupigiwa kura za maoni CCM

Hayo yametokea leo mnamo saa saa 10 jioni katika kitongoji cha ugogoni mjini Kongwa.

Katika kile kinachoonekana ni kuishiwa sera na kutumia ubabe na ukorofi ili kutetea nafasi yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, Mheshimiwa Naibu Spika wa Bunge La Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa alipiga kwa gongo ambalo amekuwa akitembea nalo huku wasimamizi wa uchaguzi wakifumbua macho kitendo cha mgombea kutembea na silaha hiyo kwenye kampeni.

Inadaiwa na mtu aliyefuatilia kwa karibu tukio hilo mkutanoni kuwa Kuna mgombea mmojawapo (mkazi wa Kongwa aitwaye ngatunga) Alisimama kuuza sera zake na kudai kuwa Kongwa kuna madini jimbo halijafaidika na chochote kutoka kwa wachimbaji wa madini... Mara moja Ndugai alimtishia kuwa anyamaze la sivyo angemuonesha kazi kwa kile anachodai kuwa ni kuongea upuuzi..

Wakati wagombea hao wakiendelea kujibizana suala hilo ndipo ghafla mheshimiwa alipomuona Mmojawapo wa wagombea aitwaye Dr Joseph Chilongani ameshika simu na kutahamaki kuwa alikuwa akimrekodi kwa kuvunja taratibu.

Ndipo Job Ndugai alipoamka na kumwambia "Tena wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana, unanirekodi na makamera yako na leo utanitambua mimi ni nani."

Mara Ndugai akakusanya nguvu na kumpiga Dr Chilongani kwa fimbo hiyo. aidha hata baada ya kuanguka chini Ndugai alimfuata na kumrukia kumkanyaga tumboni akiwa na hasira na nia ovu ya kutaka kumdhuru zaidi..

Baadae wananchi walipata hasira na kutaka kumshughukilia kwa kichapo Mbunge huyo na ndipo alipopanda haraka gari lake haraka na kukimbi Eneo la Tukio..Inasadikiwa yule mgombea mwingine alijaribu kumnyanyua Dr. Pale chini, jambo ambalo baadhi ya wananchi walilichukulia ni kama kutaka kumdhuru zaidi hivyo walianza kumpa kichapo huyo mgombea mwengine kiasi hadi watu wengine walipoamulia.. Baada ya tukio hilo ovu mkutano ulivurugika.

Ndugu zake Dr. Chilongani kwa kusaidiana na watu walimbeba akiwa amezimia na kumkimbiz hospital baada y kupata PF 3 toka polisi.

Hadi reporter anaondoka hospitalini Dr alikuwa bado hajazinduka na madaktari walikuwa wanaendelea na harakati za kuokoa maisha ya mgombea huyo.

Shuhuda mmoja wa tukio anasema kuwa tukio hilo lilirekodiwa na pengine ushahidi huo utatumika katika kumuengua Ndugai katika kinyanganyiro cha ugombea ubunge kwa ticket ya CCM hasa baada ya watia wengine kuweka pingamizi mara mbili lakini bado uongozi wa chama ulikuwa unafumbia macho.

Baadhi ya wanachama wa CCM walidai kuwa kama haki itatendeka Ndugai atakuwa amejichimbia kaburi la kisiasa na kushuhudia KIAMA CHAKE RASMI KATIKA SIASA ZA JIMBO LA KONGWA..
 
Si wamezoea, mkuki kwa ngurue kwa binadamu mchungu. Sasa segrea ileeeeeeeeeeeeeeeeeeee afungwe tu kwasababu hakuna namna
 
Kwani hy kesi ni ya CCM huo ni ukosefu na kutokuwa mvumilivu lbd upepo aliona hauendi vizuri
 
Jamani vijana mwenzangu tuliopo Dare salaam tukajiandikishe ili tuwang'oe haya MACCM mabakaji ya Democracy
 
yote haya ya kupigana ameyataka mzee pinda, pale 'aliposema mtapigwa tu'! dah!kaazi kwelikweli jamaa ameamua kuua kabisa
 
Hizi habari zipo humu kwa zaidi ya lisaa limoja.. Ni vizuri sasa kama zingekuwa confirmed kama ni rumours au ni kweli.. Maana nilivyoona breakingi news hapa nikadhani mleta uzi amepata uhakika kumbe na huyu nae ameziokota mitandaoni..

Ipo Vido kabisa inambaza whatapp.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom