Kanuni za mpira tulipokuwa watoto

Me nilikuwa nafuma mipira , wakiniuzi nilikuwa nakimbia na mpira, nilikuwa nacheza kipa au forward, nikiwa forward nalala kwenye goli la wapinzani nikisubiri mpira uje , ukija tu nikutupia kambani mana hakuna offside
Nikiwa goli kipa nilikuwa naweza kujianzishia mpira na kukimbiza mpaka kwenye goli la wapinzani na kufunga
 
Nakumbuka kuna siku "gozi" letu kuna mchizi alipiga shuti mpira ukaenda dondokea kwenye nyumba ya mzee katili.
Wazee wetu walikua makax kichizi. Akaenda mjukuu wa mzee kuomba mpira, mzee akakaza ikabidi twende timu nzima ila jamaa aliepiga shuti alikimbia.

Kufika kule mzee akaagiza kisu, akauchana mpira katikati aisee, gozi letu jipya mzee akalitusua. Tuliumia mwisho tukaishia kucheka tu.
Uzuri huyo mjukuu wake ndo alikua mfuma mipira, kesho tu rambo kibao zishatafutwa pira jipya likasukwa.
 
Sijui ni kwa nini wazazi wa kiafrika walikuwa makatili sana kwa watoto wanapocheza. Hata siku hizi bado kuna wengi tu wanakaripia au kuwachapa watoto wanapocheza. Nakumbuka kijijini kulikuwa na watoto wa jirani walikuwa wanachota maji wanamwaga kwenye kilima, kunakuwa na uteleza halafu wanakaa kwenye makarai na kuteleza kwa kwenda chini. Basi walikuwa wanapigwa sana ili wasifanye huo mchezo japo walikuwa hawaachi. Aisee nilikuja kushangaa nilipoenda Ulaya nikakuta watoto wanateleza kwenye sehemu yenye kilima cha barafu kwa kutumia makarai huku wazazi wao wako nao kuwasaidia. Wazungu huwa wanaacha watoto wao wanacheza mchezo, mingine ya hatari lakini huku kwetu wazazi wanakataza.
 
Waafrika tumelelewa kikatili sana
 
Mzazi anawaza ukivunjika, gharama za kukutibu ni zake ndio maana hataki ucheze na afya yako.
 
Hairuhusiwi kucheza na viatu pia ikiwa mkubwa huchezi labda muwe wawili mmoja timu hii na mwingine timu hii..mwenye mpira ndo anaamuwa sabu zote hupaswi kumnyima pasi mwenye mpira hata kama kazungukwa na maaduwi.

Hapo kwenye sub nafikiri kaka ulishakuwa mkubwa sheria ilipobadilishwa.. ndondo ya utoton haina sub

Mnagawanyika kwa usawia ukija ww huingii hadi aje mwingine mwingie pande tofauti hata mkiwa 15 kwa 15 poa exception pekee ni ikiwa mchezaj mpya ni mdogo hapo ataruhusiwa kucheza bila kusubiria mwenzie wa kuingia nae

Kiwanja kikiwa kidogo mko wengi mtatengeneza team tofaut mcheze mtoano

Kiwanja kama Kidogo sana au mko wachache sana chini ya watu sita kila team basi mtacheza magoli madogo au one touch
 
Mmesahu kulikuwa na lala salama hapo ni kukanyagana tu

Ukimfanyia faulo mwenye mpira boli limeisha hapo hapo

Golikipa anaweza hamisha goli na ukashindwa kufunga , ubishi ndiyo alikuwa refa wa mechi atakayeshinda imetoka.

Golikipa Bora ni yule aloyekuwa anajua kubinuka na kukanyaga washambuliaji.
 
1. Mtoto mnene daima alikuwa mlinda mlango.

2. Mmiliki wa mpira ndiye anayeamua na niacheza.

3. Kama hukushiriki kutengeneza mpira, huchezi mechi.

4.Mwenye mpira akikasirika, mchezo unakwisha.

5. Ukigonga vidole vyako kwenye jiwe na damu inatoka, unafunika eneo la jeraha kwa mchanga kama huduma ya kwanza na mchezo unaendelea.

6. Humpigi chenga sana mmiliki wa mpira, hii inaweza kumsababishia kuchukua mpira wake na kumaliza mchezo.

7. Hakuna kuotea.

8. Hakuna refa.

9. Kuna kosa tu ikiwa kosa ni kubwa.

10. Wachezaji bora wawili hawawezi kuwa kwenye timu moja, kila mtu anachagua wachezaji wake.

11. Mchezaji bora uwanjani daima yupo kwenye timu moja na mmiliki wa mpira.

12. Daima kuna nyumba ambapo mpira ukidondoka huko, tulijua mchezo umemalizika. Hivyo lazima mjilinde usiende huko mpira!

13. Kutofautisha timu, moja ya timu inavua mashati yao.

14. Mchezo unamalizika wakati wa giza na hatuoni mpira vizuri, tunatawanyika katika makundi tukichekeshana hadi tunapofikaView attachment 2858131

Sent using Jamii Forums mobile app
Huruhusiwi kupiga mpira na dole gumba utafumua mpira
 
Back
Top Bottom