HT
JF-Expert Member
- Jul 29, 2011
- 1,897
- 414
mimi ni Mtanzania mwenzenu ambaye baada ya kuona mwelekeo wa nchi yetu nimeona ni vema niwakumbushe wana wa Tanzania. Ndugu zangu watanzania, kuna kansa ambayo imetokea, imeota na sasa inaelekea kukomaa. Kansa hii inaangamiza taifa na kutufanya tuwepo hapa tulipo, imeleta majanga ya kiuchumi tuliyo nayo na imetufikisha hapa tulipo. Ndugu zangu Watanzania, tusipoiangalia na kuitibu kansa hii tunaelekea pabaya sana. Tuanelekea ktk rima refu ambalo kutoka kwake ni neema za Mungu tu.
Kansa ninayoiongelea hapa si ufisadi, wimbo ambao unaimbwa sana. Ufisadi ni sawa na maumivu ambayo kama kidonda kipo lazima yawepo. Siongelei ushabiki wa kisiasa, maana kama umepanda mti, lazima matawi yatamea tu. Ninaongelea kupoteza utambulisho wetu, Utanzania wetu na uzalendo wetu.
Ndugu zangu watanzania, ninyi ni mashahidi jinsi ambavyo watu wengi wamepoteza utambulisho wa wao ni akina nani, hawakuishia hapo wakatupa kando uzalendo na kujisahaulisha wanatoka wapi. Kwa sababu hiyo wakawaona watanzania wenzao ni mtaji wa kujinufaisha na wakasahau nchi ya uzalendo wao, hata wakatajirisha nchi nyingine wakipatia umaskini kwao. Laiti wangelijua wao ni watanzania na ya kuwa watanzania wengine ni ndugu zao, wakatunza uzalendo wao: wangeijenga nchi yao.
Ndugu zangu watanzania, tazama wanasiasa na wafuasi wao walivyopotoka. Wamesahau kuwa wao ni watanzania na kuwa hata wanaopingana nao kisisasa ni watanzania pia. Kama wangelikumbuka walau hili wangewachukulia kwa heshima. Ni nani asiyejua kuwa watanzania ni watu wa staha? Lakini kwa kupoteza utambulisho wetu hatueleweki ni watu wa aina gani na taifa gani. Tunaenenda kama watu wasio na taratibu. Tumedharauliwa na mataifa mengine kwa kuwa si wazalendo tena. Mzalendo huilinda nchi yake na ndugu zake. Kwa kukosa hilo tunatumika na wageni dhidi ya ndugu zetu na nchi yetu.
Vijana mashuleni wanasoma ili wachukue chao mapema. Haya ndiyo matunda ya mfumo wa elimu usiojenga uzalendo. Hatuthamini bidhaa zetu tena maana hatuna uzalendo.
Bado hatujafika hatua ambayo hatuwezi rudi tena, bado tunaweza kubadilika. Wapenzi ndugu zangu, turudishe moyo wa uzalendo na mapenzi kwa nchi yetu. Hebu uamue kufanya kitu kwa ajili ya nchi yako na watu wako. Usiangalie faida utakayopata kwanza, bali angalia neema utakayoleta kwanza. Ndugu zangu watanzania, tutangulize utanzania wetu kwanza kabla ya siasa. Hebu tuijenge nchi yetu kwanza, maana sisi ndio wana wa Tanzania. Si mwamerika wala mwarabu wala mganda hata mkenya atatujengea nchi yetu. Wao wana nchi yao nasi tuna Tanzania yetu
vijana wa Tanzania, tuamke na tuanze kujivunia nchi yetu. Hata kama ina matatizo na tujivunie huku tukitafuta suluhu halisi na sio politics. Anza kujivunia utanzania wako maana hata kama ukibadili uraia kimaandishi na kimaeneo, bado Mungu alikuweka Tanzania na daima utabaki Mtanzania.
Niwatie moyo wanawake na wanaume wa nchi hii, nchi yetu ni tajiri na bado tunaweza kuichukua juu. Mungu tusaidie wana wa Tanzania tuamke na kuipenda nchi nzuri sana uliyotupa, tusimame na kujivunia.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania,
nawapenda wote,