J.K.Rayhope
JF-Expert Member
- Oct 26, 2011
- 316
- 31
Baadhi ya maneno ya Mwl.Nyerere kwa serikali ya CCM ya sasa yanaonekana kuwa makali kuliko mkaa wa moto,na baadhi ya viongozi huzima hata redio kwani wakiyasikia huwachoma kweli na huwasuta nafsini mwao.Misingi ya utawala bora na demokrasia ya kweli imekiukwa,Mfano yanayoendelea Arusha leo ni kama kansa inayosambaa tartiibu mwilini mwa mgonjwa.CCM leo imepoteza majimbo mengi na muhimu kwao.Kama ni maziwa ya ng'ombe fresh tayari yamechanganywa maji.Ubungo,Kawe,Ilemela,Nyamagana,Arusha mjini,Maswa,Moshi mjini,Rombo,Mbeya n.k.Yamekwenda upinzani.Wapo baadhi ya Wanaccm wamediriki kusema bora kupoteza majimbo hata 60 (vijijini) kuliko haya zaidi ya 20(mijini) yaliyokwenda upinzani...Ushauri,CCM iache mara moja tabia ya visasi na siasa za chuki,Kama kweli tuliiweka madarakani,ipambane na majukumu mazito ya kuleta maendeleo.Hii ni nchi ya kidemokrasia,raia wake wako huru kusikilizwa,kuishi popote kwa kufuata sheria lakini dola hutumiwa kichama zaidi.Bila CCM,CHADEMA,CUF n.k Nchi yaTanzania ipo daima tu.Mbona nchi haikupata uhuru na CCM?Nawasilisha