Kwa ninavyojua mimi neno "kanjaja" ni msimu (slang?) ulioibuka wakati wa serikali ya awamu ya 3. Neno hili lilitumiwa na Rais Mkapa kuwabeza/tukana waandishi wa habari. Kwa kutumia neno "kanjanja" alimaanisha mwandishi alisiyepikwa vema i.e asiyemahiri kwenye taaluma yake-mbabaishaji, "msanii". Hapa lilitokana na waandishi wa habari waliokuwa wanaandika habari tu bila kujielimisha kuhusu mada husika na hivyo wanajikuta wanaandika taarifa zisizo sahihi ambazo hazijafanyiwa utafiti wa kutosha aghalabu kwa sababu mwandishi hajui taaluma yake vizuri. Hakuna umakini. Basi akawaita waandishi wa Tz makanjanja. Ni kama neno "kihiyo" lilivyoibuka.
Kanjanja=mtaaluma feki, msanii, "incompetent".
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.