KANISA KATOLIKI halitamualika E. Lowasa - ASKOFU NZIGILWA

Mbona ni kanisa hilo hilo katoliki ndio lilituambia Kikwete ni chaguo la mungu! je wameshawahi kuwaomba radhi Watanzania kwa mateso wanayoyapata kutoka kwa chaguo la mungu?

ile ilikuwa ni kauli binafsi ya askofu kilaini na haukuwa msimamo wa kanisa, na alisema vile kwa kuwa kikwete kipindi kile alikuwa anakubalika sana. Hivyo basi kauli yake ikatokana na quote ya kibiblia kwa sauti ya wengi ni sauti ya mungu.
 
sasa mnaanza kuwapa masifa wakati wahajasema kuwa watakualika ama hawatamualika?
 
Mizambwa wanasema mambo ya kanisa katoliki tuyajadili wakatoliki wenyewe na kuyamaliza ndani.. hongera kwa aliyeuliza swali. lakini hili tatizo inamaana hawakuliona siku zote hizo? EL alishiriki harambee ya kanisa katoliki nyakato mwanza ambapo askofu wake ni Rwaichi (rais wa TEC), hii imekaa kama tamko binafsi la Askofu Nzigilwa
 
EL alishiriki harambee ya kanisa katoliki nyakato mwanza ambapo askofu wake ni Rwaichi (rais wa TEC), hii imekaa kama tamko binafsi la Askofu Nzigilwa

Ndugu hapa kuna wasiwasi kuwa Askofu alijibu vile baada ya kupewa lile swali; na kweli inaweza kuwa tamko binafsi ikifika kwa wenzake katika baraza wakapinga, ndio maana nilitoa ANGALIZO: Kuwa Askofu Nzigilwa asije kanusha kauli yake kama alivyofanya Waziri Mkuu Pinda kuhusu mgomo wa Madakitari.

Mimi ni muumini Mkatoliki na nashukuru kwa viongozi wetu walivyoliona hili, kwani kama nilivyochangia katika THREAD ya awali kuwa "MIMI NILINYIMWA HAKI YANGU YA IMANI YA IBADA YA MISA KATIKA JUMUIYA YANGU NA PAROKO, KISA TULIMUALIKA MBUNGE WA ENEO LETU" Kwa maelezo kuwa imekatazwa na Cardinary PENGO kualika Viongozi wa Kisiasa katika shughuli yoyote ya Kikanisa.

IWEJE LEO HII TENA NDANI YA JIMBO KUU LA DSM LA ASKOFU PENGO MWENYEWE. IMEKAAJE HII!!!!!!!!!

Ndio maana binafsi nilipinga sana katika ile THREAD kuhusu jambo hili, vinginevyo tupewe maelezo ya Ufafanuzi toka baraza la Maaskofu.

Nami siongei majungu hata kama nikihitajika kutoa maelezo zaidi nipo tayari kweli ilituuma sana wanajumuiya wote KWA KUNYIMWA HAKI YETU YA MSINGI KIIMANI.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Ni Vyema ukirudi Darasani ukasome tena Kiswahili.


Pia katafute Gazeti Tumaini Letu, au Piga Simu Radio Tumaini watakuwa na habari kamili.

Askofu amekataa kuwa hawawezi katika shughuli kama hii kumpa mwaliko kongozi yeyote wa Kisiasa. NDIVYO ALIVYOSEMA KAMA KUNA MENGINE MIMI SIJUI.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Mkuu, ujue thread yako uliandika kama ilivyo hapa chini, sasa imekuwaje uongeze mengine wakati hukuyaweka awali? wachangiaji watajuaje kuwa askofu aliongea na mengine? Kwa nini uweke habari nusu halafu uanze kuwahukumu wachangiaji ambao kimsingi wanachangia kutokana na habari iliyopo? Ulikuwa unakurukupukia wapi kuwa wa kwanza kuweka humu wakati huna uwezo wa kuweka habari yote? Wa kupimwa wewe, hebu angalia kipisi ulichoweka mwanzoni:
Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la DSm (Askofu Nzigilwa) amesema kuwa "Kanisa Katoliki halijamualikwa Mh. E. Lowasa katika Harambee ya kuchangisha pesa kwa ajili ya sherehe za Uzinduzi wa Jimbo Katoliki la Ifakara kama ilivyoripotiwa hapo awali.

Askofu Nzigilwa aliyasema hayo alipokuwa akijibu shwali toka kwa mmoja wa viongozi wa Parokia walioshiriki katika kikao cha pamoja cha Tathimini ya Mavuno 2011, Msimbazi Centre DSM.


MY TAKE: TUNASHUKURU SANA KANISA KATOLIKI KWA KULIONA HILI na viongozi wa kanisa Katoliki kwa kupitia mada zetu hapa JF. Hongera pia kwa kiongozi aliyeuliza hilo swali kuhusu mwaliko wa Mh. E. L kanisani kwa moyo wako wa ushujaa.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kuna viongozi wa kanisa walikwenda kufanya uzinduzi wa kitabu cha mke wa EL mara baada ya kujiuzuru uwaziri mkuu. Tunafikiri ilitokea tu au ilikuwa ni kuonyesha ulimwengu huyu tuko naye pamoja?
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/27230-mke-wa-lowassa-azindua-kitabu-8.html

Mimi binafsi picha ninayoipata hapa ni kuwa kanisa Katoliki halijakataza Mwaliko wa Viongozi wa Kisiasa katika shughuli za Kikanisa, au viongozi wa kanisa kualikwa katika shughuli za kijamii.

kwa sababu tumeshuhudia mara nyingi Kiongozi wa Kisiasa anaalikwa katika Sherehe za madaraja ya UASKOFU.

Isipokuwa tatizo kuna baadhi ya viongozi wetu wa Kanisa katoliki ndio wanaweka hizi tofauti (yaani wanachanganya DINI na SIASA) kisha wanatoa kisingizio kuwa ni tamko toka kwa Cardinary Pengo.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mbona ni kanisa hilo hilo katoliki ndio lilituambia Kikwete ni chaguo la mungu! je wameshawahi kuwaomba radhi Watanzania kwa mateso wanayoyapata kutoka kwa chaguo la mungu?

waliwatajia jina la huyo mungu?
lazima mlikurupuka mazima.
wenzenu walimaanisha mungu baali!!!!!! nyie kuingia kingi.
 
Alieyasema hayo tayari amechukuliwa hatua za kikanisa na ulikuwa msimamao wake bianafsi na si kauli rasmi ya akanisa.......au ushawahi kumsikia au kumuona Dari Salama(Safe Roof)?
Kwa sasa huyo Askofu anakula matoke KILAINI huko kwao Kagera,Dar anaisikia tu kama anavyoisikia Roma!!
 
Kweli mashujaa wamekwisha, ina maana mtu kuuliza swali kanisani ni ushujaa!!??
Ushujaa unaoongelewa hapa ni ule wa kulitetea kanisa, ujasiri wa kuona ni kwa jinsi gani kanisa litajichafua kwa Hela itakayotolewa na Mheshimiwa huyu! Hureeeee Maaskofu kwa kumtosa!
 
Mizambwa wanasema mambo ya kanisa katoliki tuyajadili wakatoliki wenyewe na kuyamaliza ndani.. hongera kwa aliyeuliza swali. lakini hili tatizo inamaana hawakuliona siku zote hizo? EL alishiriki harambee ya kanisa katoliki nyakato mwanza ambapo askofu wake ni Rwaichi (rais wa TEC), hii imekaa kama tamko binafsi la Askofu Nzigilwa
Kufanya makosa si kosa, Kosa ni kurudia makosa!
 
Alieyasema hayo tayari amechukuliwa hatua za kikanisa na ulikuwa msimamao wake bianafsi na si kauli rasmi ya akanisa.......au ushawahi kumsikia au kumuona Dari Salama(Safe Roof)?
HAIJALISHI KITU KUALIKWA AU KUTO ALIKWA NI MKRISTU WA LUTHERAN ANAWEZA KUCHANGIA HARAMBEE TU LKN ISIWE YA MASHARTI TU.:decision:
 
Back
Top Bottom