tunalazimika
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 1,098
- 256
kwa waliofika UDOM, MUHIMBILI University Mpya iliyojengwa Kibamba Dsm, Nelson Mandela University , Maandalizi yaliyokamilika ya Ujenzi wa IFM Msata Pwani -enrollment kubwa kuwahi kutokea kwa Wanafunzi wa Elimu ni ushahidi wa Maendeleo Makubwa uliyoyasimamia kwenye ahadi zako za Uimarishaji wa Sekta ya Elimu. Achilia mbali Ujenzi wa Maabara kwenye shule zote za Sekondari nchini.
Marekebisho makubwa ya MUHIMBILI hospital kufikia uwezo wa kufanya Upasuaji wa Figo na Moyo, Ujenzi wa Hospiotal za Rufaa za Mikoa sehem zote nchini, na maboresho ya Miundombinu na vitendea kazi kwenye Sekta ya Afya ni vitu ambavyo kamwe hatutakusahau wale tunaofuatilia mambo kwa kina.
Kamwe hatutakusahau kwa Uimarishaji wa Sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji, Ujenzi wa Barabara kuu zote nchini kwa takriban mara tatu ya mtandao tuliokuwa nao tangu Uhuru na kuwezesha makao Makuu ya Mikoa yote kufikika kwa Lami ikiwa ni pamoja na Ujenzi wa madaraja makubwa kama lile la malagarasi Kigoma na Mtambaswala Mtwara na Uongezaji wa Ufanisi bandarini kwa kufanya kazi 24hrs kwa siku 7 kumelisababisha Taifa kuongeza mapato kwa kiwango kikubwa.
Ujenzi wa mradi mkubwa wa Maji kutoka ziwa Victoria kwenda Shinyanga, Kahama, Kwimba na sasa Uchambuzi yakinifu wa mradi mwingine utakaotoa maji ziwa Victoria eneo la Busega Mkoa wa Simiyu na kuyapeleka Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu, Singida na hatimaye Dodoma ni kazi nyingine ambayo Watz hatuwez kukusahau. hali kadhalika upanuzi wa Bomba kutoka Ruvu Chini na Ruvu juu kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Dar na Uchimbaji wa visima vikubwa Kigambon ni dhahiri utakuwa umekamilisha utatuz wa kero kwa miji iliyokuwa na adha hiyo.
Ujenzi wa bomba la gesi na Mpango wa Usambazaji wa umeme vijijini ni jambo jingine ambalo hakuna atakayeweza kufuta nyayo zako kwani ni dhahiri Ukuaji wa Uchumi kufika aslimia 7 utafikiwa kutoka na uwezo mkubwa uzalishaj utakaotokana na upatikanaji wa nishati hiyo muda wote na kwa bei nafuu. Tanzania itajaa mwanga na nderemo kwasababu yako na dhana ya maisha bora Watz watajua kwann uliwaahidi.
Upanuzi wa Uwanja wa ndege Dsm kwa kuwahamisha wananchi walioshindika katika zama zote na kuanza Ujenzi, Ujenzi wa Kiwanja kikubwa cha Songwe Mbeya, Kiwanja cha Kigoma na Mafia kamwe Watz wa maeneio hayo hatutakusahau n hakuna atakayeweza kufunga hata gidamu za viatu vyako.
Ujenzi wa Miundombinu kwenye Majiji, Manispaa, Miji na Makao Makuu ya Wilaya imepelekea Miji yetu yote kupendeza, ushahidi leo hii hata mitaa ya Tandale, Kwasokota, Kwa mama Zacharia, Komakoma achalia mitaa ya Kanyenye na Lufita Tabora na sehem mbalimbali nchini leo hii ina lami.
Maboresho makubwa ya Utumishi wa Umma kwa kuboresha mishahara, malipo ya stahiki mbalimbali na Ujenzi wa Maofisi sehemu mbalimbali, Uboreshaji wa Hifadhi ya Mifuko ya Jamii leo hii Kiinua mgongo cha maana siku hiyo hiyo ya kustaafu na mikopo ya nafuu kutoka Mfuko maalum wa Utumishi wa Umma ni ahadi yako iliyotekelezwa kikamilifu.
Uboreshaji wa Mifuko ya Jamii na Sekta binafsi katika Ujenzi wa Miji yetu ni jambo linaloshuhudiwa hata na vipofu na viziwi-Ujenzi wa nyumba nyingi na Maofisi makubwa yanayofanywa na Mifuko hiyo na NHC kwa kushirikiana na Sekta binafsi ni mambo yatakayokujengea heshima millele.
Uwazi kwenye Uendeshaji wa Serikali na kuhakikisha taarifa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali zinajadiliwa Bungeni na kupelekea mafisadi kubainika na kukumbwa na fagio la chuma kwa nyakati tofauti bila ya kujali mitandao na uswahiba , vinaonesha jinsi unavyoumizwa na ubadhilifu wa mali za Umma.
Umeongeza Uwezo wa Mihili ya Taifa hasa Bunge kwa kuwapa muda zaidi wa kutafakar masuala nyeti ya Taifa na kuwapa nguvu Kaamati za Bunge na kuweza kuibua uozo mbalimbali na kuwezesha utekelezaji wa maazimio yao-hakika JK utakumbukwa
Ndugu zangu natumia simu na hivyo mikono imechoka, tutaendelea next time (next episode) ya Kazi nzuri zilizofanywa na mh Jakaya Mrisho Kikwete-Rais pendwa na Watz wenye uwezo wa kuchambua mambo achilia wale wenye chuki zao binafs