kipindupindu
JF-Expert Member
- Dec 16, 2010
- 1,053
- 170
Je tujiulize mwalimu Nyerere alikua anafikiria nini?
Alisema maadui wanaotukabili kama taifa ni watatu yaani UJINGA, MARADHI NA UMASIKINI.
Naamini huu ndio msingi uliomuongoza mwalimu katika kujaribu kuleta maendeleo nchini.
Kwa maoni yangu naamini huwezi kupambana na maadui watatu kwa pamoja halafu utegemee ushindi,kamwe haiwezekani!
Je wanazuoni wafuasi wa mwalimu Nyerere mnaelezea vipi hii falsafa ya Nyerere?
Binafsi naona adui yetu ni mmoja tu -UJINGA.watanzania bado ni wajinga sana wanahitaji elimu,kwa bahati mbaya hata wale wanaoitwa wasomi; wataalamu au viongozi bado ni mbumbumbu mno.
Ukweli huu unanifanya niseme kwamba ni vyema tupambane na adui mmoja yaani UJINGA.Tukifanya hivi tutashinda!
Nawasilisha: