jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,990
- 22,523
Short and precisely on point👍🏽Ngoja nielezee kwa kitalaamu kipengele cha tatu. kwenye mfumo wa kibepari na kampuni za binafsi pesa yeyote inayotumika kwa mikopo au ujenzi n.k imetoka kwa mwekezaji. Mwekezaji hivyo inategemea kupata faida kutoka kwenye pesa yake aliyotoa.Kwa kampuni zenye hisa wawekezaji ni wenye hisa. Hii hapa ni njia (formular wanayotumia wawekezaji)
Required Rate of Retun = Risk Free Rate + Risk Premium
Maana yake ni kwamba kama mwekezaji anataka 7% (Risk Premium) kwa mwaka na serikali inauza T-Bond zake asilimia 10% (Risk Free Rate) kwa mwaka basi Mwekezaji anahitaji asilimia 17% ili aweze kutoa mkopo. Kama serikali itaongeza T-Bond kutoka 10% mfano mpaka 15% basi mwekezaji atahitaji asilimia 22% ili aweze kuwekeza. Hii ni kwasababu huwezi kupata mwekezaji anayehitaji asilimia 15% maana anaweza kwenda kununua T-Bond ambazo hazina risk na kumvutia ni lazima utoe zaidi.
Nitakuwa naendelea kutoa somo polepole ili nisiache watu.