Kampuni ya Urusi kuchimba uranium Namtumbo

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
Chilolo(2).jpg

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Diana Chilolo


Serikali inatarajia kufungua mgodi wa uranium wa Mkuju River (Mbamba Bay), katika wilaya ya Namtumbo, mkoani

Ruvuma kwa kuingia mkataba na kampuni ya Urusi ya ARMZ Uranium Holding.
Akipokea taarifa hiyo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na

Madini, Diana Chilolo, alisema mradi huo unatajia kuunufaisha taifa, kupitia Sheria ya madini ya 2010 na utakuwa mradi mkubwa wa kwanza wa madini nchini.

Alisema katika mkataba baina ya Serikali na kampuni hiyo, hakutakuwepo na migogoro ya kutokana na Serikali kujipanga katika malipo ya wakazi wanaoishi karibu na mradi huo.

“Tumeitaka Serikali iwape haki za msingi wakazi wa maeneo hayo, kwa kuwapa fidia ya mali zao, ikiwemo mashamba, nyumba, hatutarajii kuona migogoro ya ardhi inatokea kama Mwadui, Geita,” alisema.

Naye Waziri kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, aliitaka Serikali ichukue hatua zaidi za ukwepaji kodi na kuongeza mapato kwa serikali kwa mwaka wa fedha 2011/2012 kwa wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wizara nyingine

Alisema mgodi huo, utaongeza ajira za kudumu kwa wakazi wa wilaya hiyo sambamba na utoaji wa elimu inayohusu masuala ya madini.




CHANZO: NIPASHE

HAYA TENA WARUSI ULAJI HUO TOKA KWA WALALA HOI WADANGANYIKA ALALAE USIMUAMSHE HATA KIDOGO.
 
Sehemu kubwa ya eneo lenye uranium lipo katika hifadhi ya SELOUS kuna umbali kama wa kilometa 4 hadi kufika wanapokaa raia.
Najiuliza Watz wamekuwa wanapata madini ktk hifadhi wanafukuzwa kama wavamizi lakin kwa hili la uranium serikali yenyewe ilituma maombi UNESCO kuhakikisha zoezi la uchimbaji Uranium ndani ya Hifadhi unaruhusiwa.

Sababu ya kutuma Unesco ni kuwa SELOUS ni mojawapo ya hifadhi za Dunia.
 
Tatizo la wanahabari wetu nao hawako informed na mambo yanayotakiwa kufuatwa kwa ajili ya vitu mbalimbali. Sasa mbona waziri haongelei matokeo ya tathmini ya mazingira na maoni ya wataalamu waliohusishwa? Huwezi ukasema tu mradi mkubwa! Aongelee madhara na maoni kama wataalamu walivyosema, kiasi cha uranium kinachotegemewa kupatikana, process zake (kama processing itafanyika ama la), soko, faida tutakazopata na jinsi gani tumewaandaa watu wetu kunufaika na project hii. Mfano kwa wenzetu ungekuta sponsor zinatolewa vijana wakasome mambo ya uranium na radiation energy kitambo! Mwenyekiti anatuuzia chai kama wapiga kura wake! Crapy!
 
hayo ndo maoni yke, tambua kila kukicha Bush yuko bongo na mshkaji wake JK, je ni rahis warusi kuja kuchimba uranium wakti hwaivi na wamarekani? hizi ni ndoto.
 
Back
Top Bottom