samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Kampuni ya simu za mkononi ya tiGO ambayo imejizolea wateja wengi kuanzia mwaka 2005 baada ya kuanza kushusha garama za kupiga simu iko katika hali mbaya na huenda muda wowote ikafa na kuacha kampuni za voda na zain/airtel zikiendelea kutamba. Taarifa zaidi zinaeleza kua kampuni hiyo (tiGO) ambayo imetamba kwa muda mrefu na kuzipiga bao kampuni nyingine za simu za mkononi hapa nchini kwa kua na garama nafuu zaidi kwa kipindi kirefu hivi sasa imeshindwa kuendana na kasi ya ajabu ya kampuni mbili za vodacom na airtel ambazo nazo zimeamua kupunguza garama na kusababisha wateja wengi waliokua ama wameasi au wamepunguza kasi kutumia mitandao hiyo kurejea kundini kwa kishindo na kuanza kuuponda mtandao wa tigo. Inasemekana kampuni ya voda imekua ikikusanya fungu kubwa la pesa kupitia huduma ya M-PESA ambayo imesambaa zaidi vijijini tofauti na huduma ya tigo pesa ambayo iko zaidi maeneo ya mijini. Kitendo cha voda kuzindua huduma ya kupiga simu kwa garama ya nusu shilingi kwa sekunde kuanzia dakika ya kwanza kwa muda wa masaa 24 kumeishtua kampuni ya tigo ambayo inatoa huduma ya kupiga simu kwa nusu shilingi baada ya dakika ya kwanza tena kwa muda wa masaa 20. Wadau wa mitaani wanasema nusu shilingi ya tigo ina mipaka mingi kwa sababu inambana mtu kujiachia kuanzia mida ya sa 11jioni hadi sa 4 usiku vilevile haithamini mazungumzo ambayo hayazidi dakika moja. Wanasema tigo imeshagundua kwamba imeanza kukimbiwa na wateja ndo maa imebandika mabango yanayosomeka "usiache mbachao kwa msaala upitao". Taarifa nyingine zisizo rasmi zinadai tigo wameuza minara mingi na hivi sasa wanatumia garama nyingi sana kukodi minara hiyo kitu ambacho kitaharakisha kuanguka kwa tiGO... Source: habari za street...