Kampuni ya mabasi ya Shabiby ni wahuni

Shabiby wameanza lini root ya dar -Arusha?
Mara ya mwisho walitangaza wanauza magari yao maana mengine yapo kwenye meli yanakuja. Sikuona wakitangaza root mpya.
 
Pole Sana Ila napenda kukufahamisha kwamba hakuna Basi la Shabiby la kutoka Dar kwenda Moshi au Arusha. Hilo basi kuna kampuni moja ya Mvungi ndio wametoka kununua hilo basi la kampuni ya Shabiby T132 DLC.Ili kudhihirisha hilo naamini hata tiketi uliyopewa sio ya Shabiby. Ila Pole Sana kwa Usumbufu
Mkuu...Asante... ndio nagundua hapa hii ticket kweli imeandikwa Mvungi Safari maana nilipanda ndio nikapewa na nikaitia tu mfukoni...naomba kama unamawasiliano na Shabiby wawaambie wabadilishe jina itawachafua sana maana kuharibu brand ni fasta sana kwa jinsi wanavyoendesha kipuuzi hawa wa mvungi
 
Ukweli ni kua gari hiyo ilishauzwa so muuzaji kaamua kubeba abiria bila kibali cha Sumatra. Nmeongea na mtu wa karibu wa shabiby. Mtoa mada ulipewa tiket imeandikwa kampuni ipi, kama utaweza tuwekee tiket hapa [sorry sio kwa nia mbaya]
Ndio maana wanaendesha kipuuzi kuwaharibia wenzao jina....Sawa ngoja nipate mwanga nipige picha ticket..ni kweli imeandikwa mvungi japo haibadili ukweli kwamba wote tulijua tumepanda shabiby na ndio hata sabau nikapanda
 
Haina haja ya kumavha kupanda hiyo basi tatizo lako wewe badala ya kwenda kudai haki yako kama abiria sehemu husika, wewe unakuja kulalamika jf hahaha
 
Shabiby hana route ya Dar Arusha... Base yake ni Dom.. Anaanzia Dom kwenda At, Mby, Nrb, Dar, moshi... Huo ni uongo kiwango cha lami
 
Hakuna kitu nachukia kama unasafiri halafu mara mshushwe sijui mfaulishwe bila sababu ya msingi.
Kuna siku tunatoka dar kwenda kilimanjaro ile kufika njia panda wanataka watufaulishe wapite mizani, nilikuwa na bro tulileta zogo na utingo balaa walishuka wengine wakapunguza na mizigo lakini hatukushuka. Hiyo siku ndo niliamini watanzania sio wapole ni waoga tu yani kalipa nauli, anafokewa na konda na bado anashuka!
 
Basi ni uhuni ambao hata management inajua....bora wangetufaulisha kwenye basi la maana na lenye nafasi kuliko kutusimamisha kwenye mngalangala tena limefungwa tv ya chogo
Ningekuwa mimi ningewaita traffic haraka watupe majibu ya huo upuuzi.

Au mngegoma kushuka hadi wawarudishie nauli kamili ya kutoka dar. Makubaliano ni kutoka dar kwenda arusha.
 
Tatizo hatukujua wanatupeleka kwenye mngalangala uliojaa....kufika kule tukawa tushagawanyika wengine wakashuka kutafuta usafiri mwingine huku wakitukana...mi nimeamua zangu nigonge moja mbili kwanza hapa Redstone huku nikitafakari walichotufanyia then ntaamsha badae....ila pakinoga nikikamatia kitu kizuri arusha wataniona kesho...
Kwanza mlitakiwa msishuke kabisa hadi Sumatra na Polisi waje kuwaambia nini kinaendelea.

Natamani ningekuwepo ninunue kesi.
 
Hao abood wenyewe route ya Dar - Mwanza ni wahuni vibaya, kipindi flani nilisafiri nao tulipofika Moro wakaingia gereji kwao, wakatusubirisha zaidi ya 1h , baada ya kuwalalamikia sana ndo tukaendelea na safari. But Abood Dar to Moro ni confortable sana
Wanajaza hadi mlangoni
 
Kuna bro wangu anafahamiana na Boss wa Shabiby,Nimemtumia hii taarifa kampigia simu hapa hapa nkiwa naye.Yule boss kasema hilo basi washaliuza siku nyingi sema wale jamaa hawajabadilisha jina wala rangi.Ishu ya kuwashusha watu ni kwamba wale jamaa walikuwa wanaogopa SUMATRA kukamatwa.
Huyo aliesafirisha watu alitumia TLB gani?

Shabiby bado yupo liable kama hilo bus lingepata matatizo.
 
Kweli kabisaa,wote wangeamua moja na kukomaa wangefika mbona huko Arusha,wasingekubali kushuka huku wengine wakiwasiliana na kituo cha polisi hapo walipo,haya mambo ya kihuni sio wakati wake huu sasa kwa karne hii asee,.
Moro-Mwanza, tuliondoka saa 12 kwa nyehunge kama ilivyo ada. Tumemaliza dumila twaitafuta Gairo nadhani (nilikua siti za katikati sikujua shida nini) dereva wetu alimchezea rough STL. Yule driver wa STL alikua na bosi wake ndani, ikawa anataka tusimame ana-overtake na kusimama mbele ya bus almost ×4 alivyoona driver wetu hasimami ikabidi aende mbele kwenye trafiki, mbele tukapigwa mkono.
It was funny, abiria wote tulishuka. Trafiki hawezi kukosana na STL cz boss alikua ndani at the same time kasoma mob psychology ya abiria kwa wakati huo. abiria wote wamemzunguka "Boss" kumbe yeye na driver wake wamekunywa na wanawahi kikao Dodoma. Fair game askari aliwaita mashahidi(abiria wawili) driver wa nyehunge n STL wakaandika maelezo safari ikaendelea
 
Hakuna kitu nachukia kama unasafiri halafu mara mshushwe sijui mfaulishwe bila sababu ya msingi.
Kuna siku tunatoka dar kwenda kilimanjaro ile kufika njia panda wanataka watufaulishe wapite mizani, nilikuwa na bro tulileta zogo na utingo balaa walishuka wengine wakapunguza na mizigo lakini hatukushuka. Hiyo siku ndo niliamini watanzania sio wapole ni waoga tu yani kalipa nauli, anafokewa na konda na bado anashuka!
Mkuu umenikumbusha wakati wa balehe ndio nauli inatoka 50 kwenda 100 kwa wanafunzi . Wakati Sumatra wako kwenye majadiliano na walaji tayari hiace zimeanza kutoza 100. Kuna hiace ilileta matata tukaandika number plate tukaenda kwa RTO, kufika pale desk maafande wanashangaa wanafunzi wanawezaje RTO katusikiliza akaagiza wale "vodafasta" wakaenda kumbeba driver na gari lake maana konda aliona soo akakimbia.
Ni kweli, watz tu waoga pesa yako lakini unainyenyekea
 
Hii kampuni nilikua naamini ni kampuni inayojiheshimu ila leo ndio nimewadharau na sitokaa nipande tena mabasi yao. Leo nimesafiri na basi lao namba T 132 DLC toka Dar kwenda Arusha cha ajabu tumefika moshi wakatuweka kama nusu saa kisha wakatuambia wameahirisha hawafiki Arusha wanaishia Moshi. Wakatufaulisha kwenye libasi libovu limetoka vijijini na bahati mbaya basi lilikua limejaa tukabishana nao sana wakadai tusimame asietaka ashuke. Kuna wamama walikua na watoto wamelalamika mno na wengine wakaamua kutafuta usafiri mwingine. Binafsi pia niligoma kusimama basi limejaa mno.
Kudhihirisha sio bahati mbaya ni uhuni kwanza walituchelewesha sana pale Same baada ya abiria kwenda kulalamika kwa polisi wamelipa nauli mara mbili na wqmegoma kurudishiwa. Hao abiria walikua wanne mmoja aliwalipia wenzake watatu na wao bila kujua wqmelipiwa wakalipa tena baadae walipogundua wakadai refund Shabiby wakagoma ndio kisa cha kutuchelewesha tena lisaa lizima pale Same. Hawa jamaa ni wahuni kupitiliza tofauti na wanavyoonekana na basi zao kuvutia.
Mimi kwanza kabisa nikudharau wewe pamoja na abiria wenzako mliokubali kufaulishwa kama mzigo kwenye bus lingine. Hii taarifa unayoitoa hapa ni kama unatwanga maji kwenye kinu, bali ulitakuwa utowe SUMATRA au POLISI, ili bus hilo luchukuliwe hatua. Na kizuri ni kwamba, siku hizi namba ziko kwenye kila bus zimebandikwa na ni bure kupiga.
 
Umeshapata sababu ya kulala nje sasa
Tatizo hatukujua wanatupeleka kwenye mngalangala uliojaa....kufika kule tukawa tushagawanyika wengine wakashuka kutafuta usafiri mwingine huku wakitukana...mi nimeamua zangu nigonge moja mbili kwanza hapa Redstone huku nikitafakari walichotufanyia then ntaamsha badae....ila pakinoga nikikamatia kitu kizuri arusha wataniona kesho...
 
Wabongo bana! Wadau wamishasema basi hilo sio la shabiby bali la kampuni ingine iliyouziwa na shabibi, ebu Pitieni comments zote hadi chini ya uvungu ndo mchangie.sio kulalama tu
 
dar arusha panda Kilimanjaro express,dar lux au marangu coach..hao wengine ni upuuzi mtupu
 
Mkuu umenikumbusha wakati wa balehe ndio nauli inatoka 50 kwenda 100 kwa wanafunzi . Wakati Sumatra wako kwenye majadiliano na walaji tayari hiace zimeanza kutoza 100. Kuna hiace ilileta matata tukaandika number plate tukaenda kwa RTO, kufika pale desk maafande wanashangaa wanafunzi wanawezaje RTO katusikiliza akaagiza wale "vodafasta" wakaenda kumbeba driver na gari lake maana konda aliona soo akakimbia.
Ni kweli, watz tu waoga pesa yako lakini unainyenyekea
Hatuna umoja kwenye kudai haki zetu, sasa kama hapo gari inatoka dar inabidi mwisho wa safari iwe arusha lakini inafika moshi mnashushwa tena kwa lazima na kweli vidume vinashuka!
 
Hii kampuni nilikua naamini ni kampuni inayojiheshimu ila leo ndio nimewadharau na sitokaa nipande tena mabasi yao. Leo nimesafiri na basi lao namba T 132 DLC toka Dar kwenda Arusha cha ajabu tumefika moshi wakatuweka kama nusu saa kisha wakatuambia wameahirisha hawafiki Arusha wanaishia Moshi. Wakatufaulisha kwenye libasi libovu limetoka vijijini na bahati mbaya basi lilikua limejaa tukabishana nao sana wakadai tusimame asietaka ashuke. Kuna wamama walikua na watoto wamelalamika mno na wengine wakaamua kutafuta usafiri mwingine. Binafsi pia niligoma kusimama basi limejaa mno.
Kudhihirisha sio bahati mbaya ni uhuni kwanza walituchelewesha sana pale Same baada ya abiria kwenda kulalamika kwa polisi wamelipa nauli mara mbili na wqmegoma kurudishiwa. Hao abiria walikua wanne mmoja aliwalipia wenzake watatu na wao bila kujua wqmelipiwa wakalipa tena baadae walipogundua wakadai refund Shabiby wakagoma ndio kisa cha kutuchelewesha tena lisaa lizima pale Same. Hawa jamaa ni wahuni kupitiliza tofauti na wanavyoonekana na basi zao kuvutia.
Mfuate bungeni ukamlalamikie huenda hajui yanayotokea barabarani.
 
Mbona hapo stendi ya Moshi polisi wapo muda wote! Ilikuwaje mlishindwa kuwajulisha sakata hilo?
 
Hatuna umoja kwenye kudai haki zetu, sasa kama hapo gari inatoka dar inabidi mwisho wa safari iwe arusha lakini inafika moshi mnashushwa tena kwa lazima na kweli vidume vinashuka!
Kwwli mkuu hiyo ni changamoto, kuna siku natoka Kigoma kuna mama mmoja wa kikongo akawa anawapigia makelele dereva ashuke akachimbe dawa ilipita like 1h ndio driver akasimama basi gari kusimama vidume karibu vyote navyo vikashuka kuchimba dawa, maza aliwamind sana akawaambia kwa kuwa mabubu
 
Back
Top Bottom