SuperFeo ya Songea-Arusha-Moshi huduma zenu ni mbovu mabasi yenu yamechoka

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,158
Hii kampuni ya SuperFeo ruti tajwa hapo juu mabasi yake yamechoka. Yutong ya tangia mwaka 2020 mpaka leo tunaelekea 2024 unategemea nini.

Halafu hawa mabasi ya kutosha, fikiria basi lililotoka jana Moshi saa 12 na kufika Songea saa 8 usiku, saa 10 leo igeuze tena kwenda Moshi. Kweli tuko serious na maisha ya watu? Na hayo mabasi kuharibika njiani ni kawaida hasa basi la kila Alhamisi.

Halafu huduma ni mbovu mtu unaamka saa 9 usiku mpaka saa 05.30 basi haionekani. Vyombo vyetu vya LATRA na polisi wanaona haya wanawaogopa eti ni kampuni ya viongozi wa serikali.

Baba wa Taifa mwl. Nyerere mara zote alikuwa anatuambia hakuona kosa lolote ktkt azimio la Arusha maana ni azimio la utu, lilikuwa linakataza kiongozi wa serikali kuwa na kampuni binafsi na kuendesha biashara, aamue kimoja utumishi wa umma au biashara.

Ona sasa wanavyotutesa, wanaongeza nauli mpaka sh. Elfu 10 kwa ruti. Wana mishahara mikubwa na marupurupu bado ndio wamiliki wa vyombo vya usafiri na wanajipangia nauli watakavyo.

Wanaendesha biashara watavyo, wanalipa kodi watakavyo. Watanzania kuna haja ya kuchukua hatua tujikomboe tuko kwenye ukoloni bora ya Mzungu
 
Achana nalo wewe na hao wengine. Lakini mukiendelea kulitumia halafu siku likipata ajali mutakuja kulalamika kuwa basi lilikuwa bovu tutawashangaa.
 
Hii kampuni ya SuperFeo ruti tajwa hapo juu mabasi yake yamechoka. Yutong ya tangia mwaka 2020 mpaka leo tunaelekea 2024 unategemea nini.

Halafu hawa mabasi ya kutosha, fikiria basi lililotoka jana Moshi saa 12 na kufika Songea saa 8 usiku, saa 10 leo igeuze tena kwenda Moshi. Kweli tuko serious na maisha ya watu? Na hayo mabasi kuharibika njiani ni kawaida hasa basi la kila Alhamisi.

Halafu huduma ni mbovu mtu unaamka saa 9 usiku mpaka saa 05.30 basi haionekani. Vyombo vyetu vya LATRA na polisi wanaona haya wanawaogopa eti ni kampuni ya viongozi wa serikali.

Baba wa Taifa mwl. Nyerere mara zote alikuwa anatuambia hakuona kosa lolote ktkt azimio la Arusha maana ni azimio la utu, lilikuwa linakataza kiongozi wa serikali kuwa na kampuni binafsi na kuendesha biashara, aamue kimoja utumishi wa umma au biashara.

Ona sasa wanavyotutesa, wanaongeza nauli mpaka sh. Elfu 10 kwa ruti. Wana mishahara mikubwa na marupurupu bado ndio wamiliki wa vyombo vya usafiri na wanajipangia nauli watakavyo.

Wanaendesha biashara watavyo, wanalipa kodi watakavyo. Watanzania kuna haja ya kuchukua hatua tujikomboe tuko kwenye ukoloni bora ya Mzungu

Wapumbav sana,na nauli wamepandisha toka 70 elf mpaka 82 elf
 
Back
Top Bottom