Elections 2010 Kampeni za kidini zazua kizaazaa Bukoba

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Nimepata habari kwamba jana mchana kumetokea mapigano kiasi cha waumini kukimbia ovyo katika msikiti mmoja mjini Bukoba. Msikiti huu maarufu kama msikiti wa waarabu uliopo katika eneo la Omukigusha ndiko inasemekana kutokea kisa hiki.
Inasemekana kiongozi wa msikiti wakati wa ibada alichomeka kampeni na kumuita mgombea ubunge Lwakatare kwamba ni kafiri. Jambo hili liliwaumiza baadhi ya waumini na kuwa chanzo cha vurugu na mapigano.
Watu wengi walionekana wakikimbia ovyo kutoka msikitini hapo kuyapisha mapigano hayo.
 
hhaaaaaaa watatwangana sana mwaka huu....yaani kuna kila dalili za kuawaaambia vijana wangu hapa nyumbani 'Kawulethi umshini wange"=bring me my machine gun
 
Mwaka huu watatumia kila mbinu chafu. Ila kila mtu na dini aelewe kuwa vita ya ufisadi haina dini na maisha bora hayana dini. tuungane kuyapate wote.
 
Kazi ipo.
Kikwete's family inajitahidi kutumia jukwaa la masheikh kupata kura za maimamu.

Nimejifunza kitu kimoja kwenye kampeni hizi. Kiongozi bora mkristo anapaswa kutoka ccm na sio upinzani. na kama ikitokea ccm ina mgombea mwislam anagombea dhidi ya mkristo aliye maarufu basi zitaanza propaganda za udini mpaka ionekane kwamba wakristo wanamtaka mpinzani mkristo.
Watanzania tuache kudanganywa. Tunamtaka MTANZANIA mmoja aongoze dola hatumchagui kwa misingi ya dini yake wala kabila lake.

Kuna zile tetesi kwamba Nyerere alisema kuna baadhi ya makabila hayafai kuongoza nchi. Je katiba na sheria zetu zinasemaje?

CCM acheni propaganda maana ninyi mlitumia pesa za umma kwenda kusomea propaganda huko nje na sasa mnazitumia kuichanganya nchi. Elimu yenu ni BURE kabisa
 
hhaaaaaaa watatwangana sana mwaka huu....yaani kuna kila dalili za kuawaaambia vijana wangu hapa nyumbani 'Kawulethi umshini wange"=bring me my machine gun

Kauli kama yako ndio zinawastua waislamu,badala ya kuwasifu waliokataa siasa msikitini mpaka kuanzisha vurugu wewe unasema 'watatwangana sana' ?
 
Back
Top Bottom