Kampeni ya "Magufuli Baki" yaanzishwa. Yeyote atakayepinga atachukuliwa hatua

Ninaandika andiko hili kwa masikitiko makubwa.
Uroho wa matumbo ya wachache utatuponza wengi ambao hatuna hatia yamkini hata na vizazi vyenu.
Hivi mnawaza nini kumfanyia mtu kampeni za kutawala milele "et kisa ananyoosha nchi"
Mnadanganywa kua muda si mrefuu mambo yatakaa sawa jamaa anasafisha mafisadi....mbona hao mafisad hawashtakiw na wakishtakiwa dpp anaishia kufuta kesi?
Hivi haya maisha magumu nayaona peke yangu?
Dola leo ni tsh 2250 inaniathiiri peke yang? Maana mtaniambia mm n fisadi...
Bei ya kubwa ya sukari, mahindi, unga wa dona unaniathiri mimi peke yangu?
Nauliza hauwaathiri hawa vihere here wanaoomba sizonje aongezewe muda?
Au mnafurahia kwa sabab "anawaadabisha matajiri" nanyi mnafurahia kwa sabab soon na wao wataishi kishetan?

Fikirien watoto na wajukuu zenu njaa ya siku moja isiwatoe utu .



Sent from my SM-N9005 using JamiiForums mobile app
 
sawa tu maana mkubwa hakosei, ila na sisi waturuhusu tufanye ya UKUTA
Unapokua na watato wako wawili wa kuzaa mmoja unampa chakula mwingine unamnyima nini unategemea kitokee. Mimi naona moja anayenyimwa chakula lazima afe na atakufa kwa kumwachia laana unayempa chakula na hiyo laana lazima iangamize kizazi chake chote
 
John-Pombe-Magufuli-750x375.jpg

Rais John Pombe Magufuli ameendelea kupongezwa na wananchi pamoja na Taasisi za kiraia mbalimbali kutokana na misimamo yake na kazi kubwa anayoifanya ya kupigania rasilimali za nchi, kwa masilahi ya wanyonge na masikini.

Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo, Julai 17, 2017 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Masjid Ridhwaa, Alhaj Suleiman Seif Nassor na aliyekuwa mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Sengerema kupitia kura ya maoni, Laurence Mabawa.

Wakati akizungumza na wanahabari, Alhaj Nassor amesema bodi hiyo imemamua kumpongea Dkt. Magufuli kutokana na kazi nzuri anayofanya tangu alipoingia madarakani.

Kwa upande wake Mabawa, amesema licha ya kumpongeza Rais Magufuli, ameandaa kampeni kabambe inayojulikana kama ‘Magufuli Baki’ inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa yote nchini, ambapo kupitia mikutano wananchi wenye nia njema watamuomba rais abaki katika msimamo wake wa kuwatetea wanyonge na masikini.

“Kampeni ya Magufuli Baki itahusisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia wananchi wakiwemo wanafunzi wa sekondari kwa kufanya mikutano yenye nia njma ya kumwomba Rais abaki kwenye msimamo wake, kampeni hii itawapa fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wake iwe kwa kupongeza au kukosoa,” amesema.

Katika hatua nyingine, Mabawa amelaani baadhi ya wanasiasa na wananchi wanaotoa lugha za maudhi na kejeli kwa watu wanaojitokeza hadharani kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.

“Niombe TCRA kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatolea maneno ya kejeli na kuudhi watu wanaojitokeza kumpongeza Rais,” amesema.
Haki huinua Taifa......
 
Somebody somewhere is controlling our mind.tunawaomba viongozi wa dini muache unafiki MNA mzigo mkubwa kuokoa nchi hii. Naamini MNA maono na mnajua kinachoendelea. We are not s. A. F. E.
Intarahamwe wamevamia nchi.
Tupo na tutayaona
 
Mwanza kuna watu wanakula sababu ya hizi siasa za maji taka. JPM sio mjinga kiasi hicho akaanza kucheza na katiba.
 
Mwanza kuna wana siasa wana Njaa kweli. We all know about that
Kote kuna wanasiasa wana njaa, hakuna mtu asiye na njaa.

Ukianza kuhusisha habari za siasa na mikoa unaleta ukabila.Ukabila ni sumu.

Mwanza kuna wanasiasa wa kila aina na kila mrengo, kuzungumzia wa aina moja kama hao tu ndio wapo huko ni kutowatendea haki wengine.
 
Kote kuna wanasiasa wana njaa, hakuna mtu asiye na njaa.

Ukianza kuhusisha habari za siasa na mikoa unaleta ukabila.Ukabila ni sumu.

Mwanza kuna wanasiasa wa kila aina na kila mrengo, kuzungumzia wa aina moja kama hao tu ndio wapo huko ni kutowatendea haki wengine.
Uzuri si muhubiri labda wewe hapo

Kwanini iwe Mwanza na sio Dar? Ndio ukabila?
 
Back
Top Bottom