zigii
JF-Expert Member
- Apr 28, 2017
- 516
- 210
Jitahidi uhudhurie mikutano ya chadema kwa maelezo yako inaonyesha hujafika ktk mikutano yao .Chadema hawajashika nchi vipi waseme wamejenga kitu?Tangu kuanza kwa Kampeni nimekuwa nikifuatilia timu za Kampeni za Chama Cha Mapinduzi na zile za Upinzani, ukifuatilia utaona tofauti kubwa zinazodhihirisha uwezo mkubwa na maarifa ya kupanga na kuratibu mikakati ya ushindi kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi na UPUNGUFU MKUBWA wa mikakati na mipango ya uratibu wa Kampeni.
Kuhusu ujengaji wa Hoja (Sera)
Mgombea wa CCM ameendelea kunadi sera na mikakati ya kuliinua Taifa kiuchumi, kuwalinda na kuwatetea wanyonge na kuahidi kesho yenye matumaini zaidi na maendeleo. Anataja aliyokwishafanya na anafafanua amefanya nini na kwanini aliyafanya na kwamba anaomba muda zaidi wa kufanya makubwa zaidi, watanzania wanamuelewa.
Hali ya kuwa kwa Upande wa CHADEMA kuanzia siku ya ufunguzi mpaka sasa, katika kila mkutano CHADEMA wanalalamika, wanalia, wanalaani, wanatukana vyombo vya ulinzi na kutia huruma. ACT Wazalendo wao wameendelea na hoja mfu na vitisho, Wanazungumza uongo wa wazi na kuahidi kurudisha Kangomba ili watu waendelee kuibiwa Korosho zao, wanasema hawatokusanya kodi na kwamba kila kitu nchini kitakuwa bure..NI UONGO.
Kusalimia na kufanya mikutano vijijini
Ni vile kuwa CCM ina ngome zake maeneo ya Vijijini, tafiti zinaonyesha hivyo na ukweli ndio huo, Wanyonge wa nchi hii wanaitumainia CCM, wanasemewa na CCM na wanatetewa na CCM. Wanajitokeza katika mikutano ya CCM na Viongozi wa CCM wametambua hivyo, wanasimama vijijini, wanatatua kero on spot wakati wa Kampeni. Chadema wanafanya mkutano mmoja kwa siku tena maeneo ya mijini TU, hawasalimii wala kusimama kijiji chochote,na kumbuka hawana ofisi vijijini na waligomea Serikali za Mitaa, hivyo hawana hata mjumbe wa Serikali ya Kijiji, nani anawasemea.? WANAFELI.
Coverage
Kosa kubwa la kiufundi ni kuingia ugomvi na vyombo vya habari wakati wa Kampeni, kisha hawana miundombinu ya kusambaza habari zao. Wapo wanaoamini msimamizi wa habari CHADEMA anawahujumu, nadhani sio hujuma ni upungufu wa maarifa na mipango. Hawaonekani mtandaoni, magazetini, redioni wala kwenye runinga, hawapo popote. Hawawezi hata kustream live kwa simu, ni KICHEKESHO.
Hamasa katika mikutano
CCM wamejipanga katika hamasaWalipodhani kuwa watu wengine woooooote hawana maana nchi hii, na kwamba wao ni kila kitu wakadharau waandishi, jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama na wakadharau wasanii na kazi zao. wakawabeza, wakawatoa akili na kutotambua mchango wao, leo hii hakuna msanii anayejielewa anapanda jukwaa la CHADEMA, hata Ney wa Mitego nae kawakimbia kwenda ACT Wazalendo, ni jambo la kusikitisha kuwa imefikia hatua CHADEMA wamekosa watu kwneye mikutano mpaka wanasambaza picha za mwaka 2015. AIBU KUBWA..
Mgawanyo wa timu za kampeni
CCM imejipanga vyema, Mgombea wa Urais ameanza Dodoma kuelekea Kanda ya Ziwa (Nyumbani) Mgombea Mwenza anaelekea (Mashariki) na wamejipanga ambapo Waziri Mkuu ameanza Manyara (kasikazini), Nape anaunguruma (Kusini) Mzee Pinda (nyanda za Juu Kusini) na Mzee Kinana kaanza na Arusha na kwenye benchi wapo Mzee Kikwete, Mzee Makamba, Kibajaji, Mwigulu, January na wengineo...CHADEMA wameweka mayai yao yote kwenye kapu moja, msafara mmoja kuna kila mtu Mgombea, Mbowe, Kamati Kuu ya Chadema, Sekretarieti, wajumbe wa Serikali za Mitaa wote wanazunguka pamoja.
Nimalize kwa kuwapa msaada kwenye tuta, mkizidiwa sana anzeni kupika UGALI na TEMBELE, maana kupika WALI KUKU ni kujitafutia ugomvi na HASHIMURUNGWE, na nawashauri, HASHIMU sio mtu wa kugombana nae wakati huu..anawazidi sana maarifa.
Wao kazi yao kuelimisha watu kwa yale ccm imekosea na kuahidi nn watafanya km HAKI, UHURU na MAENDELEO YA WATU jitahidi uwafuatilie vinginevyo una hasira mikutano ni ya wazi kila mtu anafuatilia hata huku vijijini tunaona mikutano yote