Uchaguzi 2020 Kampeni ni mipango, mikakati na akili, CHADEMA wamepungukiwa na vyote

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Tangu kuanza kwa Kampeni nimekuwa nikifuatilia timu za Kampeni za Chama Cha Mapinduzi na zile za Upinzani, ukifuatilia utaona tofauti kubwa zinazodhihirisha uwezo mkubwa na maarifa ya kupanga na kuratibu mikakati ya ushindi kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi na UPUNGUFU MKUBWA wa mikakati na mipango ya uratibu wa Kampeni.

Kuhusu ujengaji wa Hoja (Sera)
Mgombea wa CCM ameendelea kunadi sera na mikakati ya kuliinua Taifa kiuchumi, kuwalinda na kuwatetea wanyonge na kuahidi kesho yenye matumaini zaidi na maendeleo. Anataja aliyokwishafanya na anafafanua amefanya nini na kwanini aliyafanya na kwamba anaomba muda zaidi wa kufanya makubwa zaidi, watanzania wanamuelewa.

Hali ya kuwa kwa Upande wa CHADEMA kuanzia siku ya ufunguzi mpaka sasa, katika kila mkutano CHADEMA wanalalamika, wanalia, wanalaani, wanatukana vyombo vya ulinzi na kutia huruma. ACT Wazalendo wao wameendelea na hoja mfu na vitisho, Wanazungumza uongo wa wazi na kuahidi kurudisha Kangomba ili watu waendelee kuibiwa Korosho zao, wanasema hawatokusanya kodi na kwamba kila kitu nchini kitakuwa bure..NI UONGO.

Kusalimia na kufanya mikutano vijijini
Ni
vile kuwa CCM ina ngome zake maeneo ya Vijijini, tafiti zinaonyesha hivyo na ukweli ndio huo, Wanyonge wa nchi hii wanaitumainia CCM, wanasemewa na CCM na wanatetewa na CCM. Wanajitokeza katika mikutano ya CCM na Viongozi wa CCM wametambua hivyo, wanasimama vijijini, wanatatua kero on spot wakati wa Kampeni. Chadema wanafanya mkutano mmoja kwa siku tena maeneo ya mijini TU, hawasalimii wala kusimama kijiji chochote,na kumbuka hawana ofisi vijijini na waligomea Serikali za Mitaa, hivyo hawana hata mjumbe wa Serikali ya Kijiji, nani anawasemea.? WANAFELI.

Coverage
Kosa kubwa la kiufundi ni kuingia ugomvi na vyombo vya habari wakati wa Kampeni, kisha hawana miundombinu ya kusambaza habari zao. Wapo wanaoamini msimamizi wa habari CHADEMA anawahujumu, nadhani sio hujuma ni upungufu wa maarifa na mipango. Hawaonekani mtandaoni, magazetini, redioni wala kwenye runinga, hawapo popote. Hawawezi hata kustream live kwa simu, ni KICHEKESHO.

Hamasa katika mikutano
CCM wamejipanga katika hamasaWalipodhani kuwa watu wengine woooooote hawana maana nchi hii, na kwamba wao ni kila kitu wakadharau waandishi, jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama na wakadharau wasanii na kazi zao. wakawabeza, wakawatoa akili na kutotambua mchango wao, leo hii hakuna msanii anayejielewa anapanda jukwaa la CHADEMA, hata Ney wa Mitego nae kawakimbia kwenda ACT Wazalendo, ni jambo la kusikitisha kuwa imefikia hatua CHADEMA wamekosa watu kwneye mikutano mpaka wanasambaza picha za mwaka 2015. AIBU KUBWA..

Mgawanyo wa timu za kampeni
CCM imejipanga vyema, Mgombea wa Urais ameanza Dodoma kuelekea Kanda ya Ziwa (Nyumbani) Mgombea Mwenza anaelekea (Mashariki) na wamejipanga ambapo Waziri Mkuu ameanza Manyara (kasikazini), Nape anaunguruma (Kusini) Mzee Pinda (nyanda za Juu Kusini) na Mzee Kinana kaanza na Arusha na kwenye benchi wapo Mzee Kikwete, Mzee Makamba, Kibajaji, Mwigulu, January na wengineo...CHADEMA wameweka mayai yao yote kwenye kapu moja, msafara mmoja kuna kila mtu Mgombea, Mbowe, Kamati Kuu ya Chadema, Sekretarieti, wajumbe wa Serikali za Mitaa wote wanazunguka pamoja.

Nimalize kwa kuwapa msaada kwenye tuta, mkizidiwa sana anzeni kupika UGALI na TEMBELE, maana kupika WALI KUKU ni kujitafutia ugomvi na HASHIMURUNGWE, na nawashauri, HASHIMU sio mtu wa kugombana nae wakati huu..anawazidi sana maarifa.
 
Ccm wana sera au feedback?

Coverage ipo ni wewe tu na uvivu wako wa kufuatilia unataka uwekewe TBC.

Mikakati unayosema ulitaka chadema wazunguke na Linah Sanga na Sholo Mwamba na Zuchu?
 
CHADEMA hawana misingi wala hoja kumshawishi mwananchi ni dhahiri kama ni kura watapata kwa wanachama wao ambao wamepungua hivi sasa, kueneza chuki, sera zisizo na strategy hawawezi kufika popote, huna machinery katika vijiji na kata na unafanya kampeni kwa ndege, it doesnt make sense
 
Welcome back Dude! Kwakuwa umeshapita bila kupingwa, utakuwa na muda wa kutosha kuandika kama hivi. Hongera na kila la heri katika harakati zako za kurejea Barazani.
Tunazo video zake kadhaa ambazo anamtukana magufuli na ambazo hujawahi kuzisikia, baada ya siku chache tutazianika hadharani bila huruma yoyote, jipangeni, kama mnadhani yamekwisha mnajidanganya
 
Ukweli ni kwamba kampeni huwa hazina maana watu huwa na wagonbea wao kichwani hata ufanye kampeni vipi haibadilishi akili au maamuzi ya wapiga kura wengi ,pili mwaka huu hata kampeni za ccm zimepoa sana zaidi ya kubebwa na media for coverage ila hakuna hamsha hansha ya miaka yote
 
1. Kwa issue ya Media kweli wamepwaya sana ila kuwazingua TBC ilikua halali kabisa. Huwezi weka live alafu unakata kata picha na sauti haina maana kabisa.

2. CHADEMA hawakususa Serikali za Mitaa bali 90% ya wagombea walienguliwa!! Sasa wangeshiriki na 10% pekee.

3. Mikutano ya CHADEMA ipo kwa ratiba ya NEC. Yye ameanza kutambulishwa kwa kanda zote then ndio ataanza kampeni majimbo ambapo mbeya atafanya mikutano 8 ndani ya siku 2.

4. Kuhusu kugawanyika kasome ratiba ya NEC Mnyika,Mwalimu na Lissu watakua majimbo tofauti wakimaliza ziara kanda ya pemba huko. Na siyo CHADEMA tu hta ACT na NCCR watafanya hivyo kwahyo sio initiative ya CCM kma unavyodai.

5. Kuhusu picha za 2015 nadhani sio msimamo wa chama ila mahudhurio ya shinyanga yalikua mazuri so hakukuwa na haja ya cover up kma unayotaka kuforce hapa.

6. Kuhusu sera mbona Lissu amenadi au hujasikia hotuba kuanzia Mwanza kagusia Bima,Mfumo wa kodi,Kilimo,biashara, wavuvi na wafugaji, Elimu n.k ama upo biased tu kuwa walikua wanatukana/lalamika. Let's be objective kidogo.

CCM walichoizidi CHADEMA ni rasilimali pesa tu basi otherwise sijaona innovationa ya CCM ya kutisha, hata kudesign App kma CHADEMA imewashinda!!
 
Wapinzani wakipata wabunge 10 mwaka huu wakatambike
Then wewe itakusaidia nini? Checks and balances zitazingatiwa vipi hasa kwenye vyombo vya uwakilishi?

Ushabiki wa vyama unaua uwezo wetu wa kufikiria mbali. Hvi unadhani bila nguvu ya upinzani CCM wanaweza kuwa serious na hii nchi?
 
Mimi chadema wamenikera kitendo cha kumpa bendera ya taifa mtu ambaye ni wakala namba moja wa mabeberu. Lisu mara zote amekua akitetea maslahi ya mabeberu mbele ya rasilimali zetu. Yaani ukimuuliza Lisu anataka 2040 aone Tanzania ya aina gani hakika hawezi kujibu maana ametumwa na mabeberu kuja kumthibiti Magufuli ndio maana sera zake zote ni kupinga yale Magufuli amefanya, sasa kupitia yeye tunakwenda kuwajibu wote waliomtuma.
 
Then wewe itakusaidia nini? Checks and balances zitazingatiwa vipi hasa kwenye vyombo vya uwakilishi?

Ushabiki wa vyama unaua uwezo wetu wa kufikiria mbali. Hvi unadhani bila nguvu ya upinzani CCM wanaweza kuwa serious na hii nchi?
Sasa kama wapinzani wenyewe hawako serious angalau kupata wabunge 10 unataka mimi nifanyaje mkuu!?

Mimi nmeelezea uhalisia wa hali ilivyo
 
Back
Top Bottom