Kamera, mashahidi 11 kutumika kesi ya Jerry Muro

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MASHAHIDI 11 na kamera za kurekodia matukio za Hoteli ya See Cliff ya jijini Dar es Salaam vinatarajia kutumika katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya sh milioni 10 inayomkabili mtangazaji wa TBC, Jerry Muro. Upande wa Mashtaka unaoongozwa na Wakili Stanislaus Boniface, umedai mazungumzo ya kuomba na kupokea rushwa ya sh milioni 10 ya mtuhumiwa namba moja, Jerry Muro, kutoka kwa Michael Wage Karoli ambaye alikuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, yalikuwa yakinaswa na kamera za hoteli hiyo.
Akisoma maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu Genevetus Dudu, Wakili Stanislaus Boniface, alidai ingawa watuhumiwa wanakana lakini kamera za kunasa matukio iliyofungwa kwenye vyumba vya hoteli hiyo ilinasa mazungumzo yao.
"Mheshimiwa hakimu, mazungumzo ya kuomba na kupokea rushwa ya sh milioni 10 yaliofanywa na mtuhumiwa namba moja, Jerry Muro, kutoka kwa Michael Wage Karoli, yalikuwa yakinaswa na kamera za hoteli ya Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam na mashahidi 11 wanatarajiwa kuitwa kuja kutoa ushahidi wa tukio hilo," alidai Stanislaus.
Wakili Stanislaus Boniface, alidai washtakiwa, Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratius Mgasa, wakati wa mahojiano na polisi kwenye Kituo cha Kati jijini Dar es Salaam, walikubali mashtaka hayo lakini anashangaa wanayakana mahakamani.
Wakili Boniface alidai kuwa shtaka la kwanza ni la kula njama kwa mujibu wa kifungu cha 32 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Alidai kuwa mnamo Januari mwaka huu, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote kwa pamoja, walikula njama kwa nia ya kutenda kosa linalohusiana na rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Katika shtaka la pili, wakili Boniface alidai kuwa Januari 29 mwaka huu, washtakiwa wakiwa katika Hoteli ya Sea Cliff, waliomba rushwa ya sh milioni 10 kutoka kwa Wage ili habari zake kuhusu ufisadi, zisitangazwe kwenye kituo cha televisheni cha TBC.
Aidha, shitaka la tatu ambalo linawahusu Kapama na Mgasa ni la kujipachika wadhifa wa uongo.
Ilidaiwa kuwa Januari 29 mwaka huu, katika Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam, washtakiwa hao wakiwa na lengo la kumlaghai Wage, walijitambulisha kuwa ni waajiliwa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), huku wakijua si kweli.
Washatakiwa hao wamekana kuhusika na makosa wanayotuhumiwa nayo na kesi hiyo itaendelea tena leo.



h.sep3.gif
Chanzo ni Kamera, mashahidi 11 kutumika kesi ya Jerry Muro

Tatizo hili la Rushwa kwa hapo kwetu Tanzania limekuwa kama ni donda Kuu lisiloponyeka. Sijuwi Serikali yetu italimaliza lini hili Gonjwa la Kula Rushwa?
 
Back
Top Bottom