Zitto NA WENGINEO,
Naomba kuuliza ili kuepekana na hizi policy za serikali hasa katika pension funds na marupurupu ya kujilimbikizia kwanini wakurugenzi (directors) na utawala wasiwe wanapewa contract za miaka 5. Na katika contract za miaka 5 malipo yao kuwepo na mshahara (lump sum), na incentive based on PERFORMANCE???
Swali jengine ni malipo ya wakurugenzi wakuu wa hizi pension kwanini SSRA isiweke kipengele kuwa kila mwaka malipo haya yatolewe in public ijulikane?
Nauliza tu kutaka kufahamu.
Swali zuri, ila katika nchi hii ya Tanzania ambayo mshahara wa Rais na marupurupu yake ni "SIRI" nadhani hili jambo ni gumu. Henu tuanze kudai kwanza kujua mishahara ya viongozi wakuu wa nchi kama Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Spika wa Bunge, IGP, CFD, DG wa usalama wa taifa, DG wa PCCB, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, etc ndiyo tuhamie wakuu wa mashirika ya umma kama PPF, NSSF, BoT, TIB, TRA, nk