Kamati ya Bunge yaidhinisha bajeti Wizara ya Utamaduni

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeridhia na kuidhinisha matumizi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya takribani Bilioni 35.4 kwa mwaka wa Fedha 2023/24.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko amesema kuwa, Wizara hiyo inahitaji kutekeleza majukumu yake ikiwemo ujenzi wa viwanja vya michezo, miundombinu mbalimbali pamoja na kuhakikisha shughuli zote za Utamaduni na Sanaa zinatekelezwa kama zilivyoanishwa kwenye Bajeti.

"Tumepitisha taarifa na Mpango wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2023/24 , nawasisitiza mkatekeleze yaliyopo kwenye Bajeti kwa kuzingatia mtiririko wa fedha katika Kila Idara" amesema Mhe. Sekiboko.

Awali akiwasilisha taarifa ya Bajeti hiyo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Pindi Chana amesema Wizara inatarajia kutumia takriban Bilioni 11.8 katika miradi ya Maendeleo na Bilioni 13. 9 kwa ajili ya Matumizi mengineyo na Shilingi Bilioni 9.6 ni mishahara.

Mhe. Chana ameongeza kuwa, Wizara itaendelea kuratibu Tamasha la Utamaduni, kuazimisha siku ya Kiswahili, Kuratibu na kuandaa Tamasha la Serengeti Festival na Mashindano ya Kimataifa ya Urembo na Utanashati kwa Viziwi.

Aidha, Mhe. Pindi amesema, kwa mwaka ujao wa fedha wizara inatarajia kuratibu ushiriki wa Tanzania katika mashindano ya Kimataifa ikiwemo Mashindano ya Afrika (AAG) na michezo ya Afrika Mashariki, UMITASHUMTA na UMISSETA, Tanzanite Women Festival na Taifa Cup.

IMG-20230324-WA0035.jpg
View attachment 2564099

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom