Kapinga
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 727
- 13
Nafikiri tuendako tunahitaji Zero tolerance. Kuna mafisadi na vifisadi.
Ukimchunguza saana Mwakyembe utagundua kuwa kama angelipata nafasi nzuri, mhhhh.........
Kwa habari ambazo mie nimeshazisikia tayari ambazo mwakani zitaanikwa hadharani wakati wa uchaguzi, jamaa si mzuri kiasi hicho.
Hivi kwa nini asingelikuwa ni MFANO WA KUIGWA kama alivyo Dr. Slaa? Kwani anashindwa nini kuwa msafi na hasa ukichukulia alisoma sheria? Kuna vitu anajiingiza kichwa kichwa hadi unamhurumia. Wengi wanamkubali Mwakyembe kwa uwezo wake mkubwa na kama asingelikuwa na papara na akawa ametulia, sasa hivi angelikuwa kashamziba hata Dr. Slaa na nafikiri ndani ya CCM angelikuwa tishio kubwa sana na siyo sasa kila siku yuko busy kujibu mapigo. Mara huku umeme wa upepo, mara kateka watu, mara kagombanisha watu mara kagombana na mkuu wa Mkoa, mara kagombana na madiwani mara kaficha data za bunge..... Mara moja, mbili sawa ila sasa inakuwa too much hadi mtu unaanza kuamini kuwa huyu na yeye mhhhhhhh......
Ila nashindwa kufahamu kuwa hawa watu wa tume, walichaguliwa wale ambao pia wana makosa? Maana wao inakuwa rahisi sana kuwatisha (tishia ya Hosea) kuwa "mkinitenda, ntakutendeni...." Alipomparamia RA, alipigwa kishock cha umeme kidogo tu, akawa akilalamika kila sehemu. Ukweli ukabaki wazi kuwa alitumia data alizozipata kwenye utafiti na yeye akataka kuanzisha kampuni ya kuzaa umeme wa upepo ili na yeye afyonze. Mtu mwenye mapenzi ya nchi yake, lazima angelifahamu kuwa swala la energy, inabidi libaki mikononi mwa nchi milele na hasa kwa nchi masikini.
Mkuu hacha kupotosha watu...unajua wanaohusika IPTL, Songas, Kiwira, Richmond, Artumas, Na project ambazo zimekwama kama Wind-Eetc etc. Unajua ma director wa Tanesco vizuri na nani wanahakikisha watu wao wanawekwa? Issue ya Umeme haipo mikononi mwa wananchi...power pool ya mwakyembe ni briefcase company ambayo hata tender haijapata kokote, it was an idea in its early stages unacompare na Richmond?? Acha kupotosha jamii.