Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Kamati hii teule ilikuwa na wajumbe 5 ambao ni:
(i) Mhe. Eng. Ramo Matala Makani, (Mb.) - Mwenyekiti
(ii) Mhe. Martha Jachi Umbulla, (Mb.)
(iii) Mhe. Gosbert Begumisa Blandes, (Mb.)
(iv) Mhe. Mch. Israel Yohana Natse, (Mb.)
(v) Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa, (Mb.)
Kamati hii ilikuwa na wajumbe wa Sekretariati wafuatao (kimsingi watendaji wa kamati)
Ndugu Nenelwa Mwihambi-Wankanga
(ii) Ndugu Lukago Alphonce Madulu
(iii) Ndugu Asia Paul Minja
(iv) Ndugu Mswige Dickson Bisile
Kamati hii teule ilipewa muda usiozidi wiki nane (kuanza kazi Sept 5, 2011). Na Kamati hii iliweza kufanya mahojiano na watu wapatao 146 ambao aidha walilazimika kwenda kwenye kamati hiyo au kamati ilikutana nao. Ili kuweza kufanikisha shughuli zake za uchuanguzi wa mambo haya bila ya shaka kamati iliingia gharama mbalimbali. Binafsi ningependa sana kujua kama kiasi kilichotumika kimeendana na huduma ambayo tumeipata kama taifa (value for money). Hasa ni muhimu kujua kama watendaji wote watachukuliwa hatua za kawaida za kinidhamu au kutochukuliwa hatua kabisa na kupewa maonyo tu.
Kwa sababu kama mwisho wa siku hakuna atayeondolewa au hata kufikishwa mahakamani (kustaafu ukiwa na mafao yako siyo adhabu) basi Watanzania watakuwa wamepoteza mara mbili.
a. Wamepoteza kwenye fedha ambazo zinadaiwa kuchotwa kiaina kufuatia agizo la Jairo
b. Wamepoteza mara mbili kwenye fedha za posho na gharama nyingine ambazo Kamati Teule imeingia - hivi wabunge wanapokaa kwenye vikao vya kamati teule wanalipwa posho ya kiasi gani au wanafanya bure?
Tusipoangalia kama taifa tutakuwa tumechezeshwa mchezo wa "chekundu cheusi" a.k.a kuingizwa mjini yaani tumeliwa double hadi "king"!