Kamati hii ya CDM isiyojumuisha akina mama; IKO WAPI?

kuanzia lini chadema wakatupa kipaumbele sisi wanawake? hiyo ni sera ya ccm imekubarika sana miongoni mwa sisi akina mama. wao chadema watasema JK anatembea na sisi wanawake wote.... ndio jibu lao kwa wepesi. hata wafuasi wa chadema hawaoni umuhimu wetu wanawake angalia mchango wao kwenye thread hii utagundua kuwa wanatutumia tu baadhi yetu ili wafike wanakotaka kufika

kwani wewe uliumbwa kwa ajili gani?
 
Msiwe wajinga nyie.... Chadema wanakwenda kumwona rais ili asi saini muswada huu na kuwa sheria, unahitaji watu wangapi kumshawishi rais na huyo mwanamke atatumia kipi ambacho hawa viongozi hawana... Ooooh! nimeelewa mnataka kumpelekea vipapi shosti..

Chadema wanachodai ni kwa maslahi yetu sote ili muswada urudishwe bungeni na kufanyiwa marekebisho ambayo ni muhimu kwetu sote. Sasa mwanamke, Padre na Sheikh wanatakiwa wafanye nini? Chadema wanakwenda kumwona rais asipitishe muswada huu na kuwa sheria ili wanawake, Masheikh na Mapadre mpate nafasi ya kushiriki, tena basi inaweza kuwa wazo zuri sana tukiteua tume kutoka makanisa na miskiti, asisi za wanawake kukusanya mawazo ya wananchi..
 
Mkuu Ikulu siyo bungeni kwamba ni lazima upeleke uwakilishi wa makundi,make baadae mwingine atahoji mbona hamna mjumbe wa bavicha ama kwanini haikwenda kamati kuu yote?kule panahitaji watu wachache sana ili wakawasirishe mambo ya msingi na hili wala halihitaji Popular democracy ama Proportional Representative

Umeelewa ?Mods wanaelewa ndo maana walikusaidia kufuta ujinga ule
 
kuanzia lini chadema wakatupa kipaumbele sisi wanawake? hiyo ni sera ya ccm imekubarika sana miongoni mwa sisi akina mama. wao chadema watasema JK anatembea na sisi wanawake wote.... ndio jibu lao kwa wepesi. hata wafuasi wa chadema hawaoni umuhimu wetu wanawake angalia mchango wao kwenye thread hii utagundua kuwa wanatutumia tu baadhi yetu ili wafike wanakotaka kufika

Kumbe wewe ni mwanamke

Basi safari ijayo tutakufikiria,usijali
 
Matatizo ya kijinsia ni suala ya kimfumo. Utamaduni - mila na desturi, sheria vinamzuia mwanamke au mwanamme kukosa haki zake za kiraia na za asili. Suala muhimu ni kuangalia maslahi ya mwanamke yanazingatiwa km ajenda muhimu kwenye majadiliano na rais. Sidhani uwepo wa wabunge wanawake wengi bungeni umeweza kuwakilisha maslahi ya wanawake wa kitz. Hivi Sophia Simba alipokuwa waziri wa utawala bora aliwakilisha wanawake vizuri wkt akifumbia macho ufisadi? Aliwakilisha na kutetea mfumo dume
 
kwa watu wanaojua kufikiri vema na kusoma alama za nyakati ilikuwa ni muhimu sana chadema chama cha magwanda kuchagua kamati yenye angalau wanawake wawili kwenda kumuona mwenyekiti wa magamba

Nini kinahitajika kuongea na kikwete.......Jinsia? Hapa Hatuongelei USAWA, Tunaongelea Haki! Tusiwe watumwa wa USAWA! Tuangalie mambo gani yanatakiwa Kujadiliwa! Unadhani mwanamke akiwepo ndo atatabasamu kwa kikwete ili abadili kamati ya Katiba? Hoja ya Mtoa hoja si hoja ya msingi
 
Upumbavu tena ni upumbavu wa hali ya juu ndio mnaoujadili, naona leo JF hakuna topic ya maana
 
Back
Top Bottom