Kamanda wapolisi saidi mwema na polisi wako wananchi watawamalizeni

lifeofmshaba

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
867
219
GP Mwema atema amwaga cheche

Makamanda wa wilaya zote kufundwa
Serikali za mitaa wakae `mkao wa kula`
DC ajitosa kuendesha ibada ya mazishi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema, akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa ofisa wa Polisi, Joseph, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake wilayani Nkasi mkoani Rukwa jana.
Siku chache baada ya wananchi wa kijiji cha Mwakashahala kata ya Puge wilayani Nzega, mkoani Tabora, kumuua askari polisi mwenye namba E6530 Joseph Millinga.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jenerali Said Mwema, ametema cheche na kusema kuwa makamanda wa polisi wa wilaya zote nchini wanakutana mjini Dodoma kuandaa mkakati wa kuimarisha ushirikiano baina yake na wananchi.
Alisema lengo ni kujenga ushirikiano wa dhati baina ya jeshi hilo, serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla ili kujenga uwanja mpana wa upatikanaji wa haki pindi wananchi wanapokwenda polisi.
Akizungumza baada ya mazishi ya marehemu Millinga yaliyofanyika katika kisiwa cha Manda Kerenge kilichopo katika kata ya Kirando wilayani Nkasi mkoani Rukwa, IGP Mwema alisema hatua hiyo inakusudia pia kupunguza kasumba ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Aliongeza kwamba jeshi la polisi limeweka mikakati endelevu ya kulinda maisha ya wananchi na mali zao ikiwa ni pamoja na kupambana na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya kuwa na hasira kali na kuvunja sheria za nchi.
Alisema kuwa “ni kifo cha kusikitisha kilichomkumba kijana wetu akiwa katika kulinda usalama wa wananchi kutokana na madhara makubwa yanayowapata wananchi wengi mara baada ya kutumia madawa hayo ya kulevya aina ya bangi sasa jeshi likitaka kuokoa maisha ya wananchi na wananchi wenyewe wanakatisha uhai wa askari wetu jamani tutafika wapi kwa hali hii?...juzi tu nimepata habari juu ya msiba mwingine uliotokea katika kijiji cha Miombo katika wilaya yenu ya Nkasi huku Tabora nako wakamuua askari wetu.”
Alikumbusha kwamba “hakuna jambo lolote linaloshindikana katika sheria hivyo kama kuna mtu anaona hakufuata utaratibu basi jitahidini kufuata utaratibu wa kisheria kuanzia ngazi ya mtaa, kijiji kata wilaya mkoa na hata taifa na si kujichukulia sheria mikononi.”
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Joyce Mgana, amelazimika kuendesha ibada ya mazishi, baada ya Kanisa Katoliki kukataa kumzika marehemu huyo kwa maelezo kwamba hakuwa anatimiza masharti ya kikanisa wakati wa uhai wake.

source ippmedia

MY TAKE: saidi mwema bado ujasoma ramani na nyakati hakuna raia anayetaka kuua mtu, awe ameiba au polisi aliyelindoni,
imefikia hatua matatizo yanayo izunguka jamii yetu yatatuliwe kwa kuchimba mzizi wake,
moja suhala la kufuata sheria nchi hii ni kama kucheza kamali na mbaya zaidi watu wanafanya makosa wanapelekwa polisi kesho yake wako mtaani wanatamba au wanakwenda mahakamani polisi wanachezea kesi kwa kuweka ushahidi dhaifu
mbili chanzo cha watu kukosa imani na polisi ni ninyi polisi kwa kupenda kwenu rushwa
mwisho kama mtaendela kucheza na wananchi , mimi si support mtu kua mtu lakini haya yatakuwa matukio ya kila siku mpaka polisi watakapoelewa somo.
tendeni haki kumaliza mgogoro
 
Back
Top Bottom